Ni kwanini mtu ukifanikiwa au ukipiga hatua fulani katika maisha ndugu na jamaa ndo huanza kukutafuta

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Katika hii dunia kuna watu huwa hawaeleweki ukiwa katika maisha msoto hutosikia ndugu na jamaa wanakutafuta hata unapojaribu kuwatafuta hata salamu msalimiane kila mtu anajifanya yupo bizee wengine hata simu zako hawataki kuzipokea ,

Ila sasa Mungu akijalia ukavuka hatua flani katika maisha na kuanza safari ya mafanikio ndo unaona mijitu inaanza kukutafuta. Simu kila saa za mtu anataka muonane, mwingine Mara akualike kwene kikao cha harusi, mwingine Mara Ohoo Mimi mjomba wako upande wa mama yako, mwingine Mara Ohoo Mimi sijui ndugu yako upande sijui nani nani ,
Yaani mtu unakuta ana force mjuane.

Wakati kipindi cha msoto alikuwa hana muda na wewe ivi tatizo mini

Mtu akutafute pale anaposikia wewe sio yule wa jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kwangu ilikuwa ni vita,hata mshahara sijajua kiasi gani baba wadogo,waliwahi kunisaidia wakaaanza nikabidhi watoto wa kuwasomesha....kila shida breki ya kwangu. Nikaona usinichezee nikabadili namba. Nimewafundisha wadogo zangu kutokutegemea sana ndugu au kuishi kwa ndugu bila sababu za msingi. Likizo ikifika rudi home.Watu wanakuwa kama wanawekeza
 
Hii ni kawaida sana kwenye jamii zetu, Lakini jibu ni moja tu. Kwamba hali ni mbaya nawewe ndo unakua kimbilio lao, lakin sometimes kwa mtu anaejitambua hawezi kukusumbua. Mzazi au ndugu hta kma alikusaidia ukavuka hatua moja kwenda nyingine akiwa mstaarabu hasumbui anajua alitekeleza wajibu wa kukusaidia japo hukumuomba au ulimuomba na akijua baada ya hapo ulipofikia unamajkum yako ya kujijenga. Kuna rafiki yangu mzazi anampngia hadi matumiz kisa tu anajua kipato chake wakati mwanae anajiandaa kuwa na familia.
 
Katika hii dunia kuna watu huwa hawaeleweki ukiwa katika maisha msoto hutosikia ndugu na jamaa wanakutafuta hata unapojaribu kuwatafuta hata salamu msalimiane kila mtu anajifanya yupo bizee wengine hata simu zako hawataki kuzipokea ,

Ila sasa Mungu akijalia ukavuka hatua flani katika maisha na kuanza safari ya mafanikio ndo unaona mijitu inaanza kukutafuta. Simu kila saa za mtu anataka muonane, mwingine Mara akualike kwene kikao cha harusi, mwingine Mara Ohoo Mimi mjomba wako upande wa mama yako, mwingine Mara Ohoo Mimi sijui ndugu yako upande sijui nani nani ,
Yaani mtu unakuta ana force mjuane.

Wakati kipindi cha msoto alikuwa hana muda na wewe ivi tatizo mini

Mtu akutafute pale anaposikia wewe sio yule wa jana

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na aina ya ndugu. Ukiwa na ndugu mimi hata uwe na private jet kama tulikuwa hatupo karibu tutaendelea na hali hiyo hiyo hadi kieleweke.
 
Kwani we ukiambiwa uwe unapigiwa simu na kuombwa au uwe unapiga kuomba wewe,utachagua lipi,kiuhalisia kwenye kutoa inapunguza ulichonacho ila kiimani kutoa utaongezewa,dogo saidia watu,huezi ombwa lift ukiwa na huna usafiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom