Ni kwanini mji wa Moshi hauna taa za barabarani za kuongoza Magari?

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,413
10,636
Wakuu imebidi niuize ili nijue.

Ni kwanini mji wa Moshi ambao ndio makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro hauna taa za kuongozea magari, ili hali miji midogo kama Singida, Shinyanga na Babati naona wameweka taa za kuongoza magari.

Ifahamike kuwa mpaka sasa Manispaa ya Moshi ndio manispaa inayoongoza kwa kuwa na mtandao mpana wa barabara ukiondoa majiji machache yalioyopo Tanzania, hii ni kwa mujibu wa TARURA. www.tarura.go.tz

Nini kinashindikana kuziweka hizi taa?

======================================
Ni kweli mji wa Moshi hauna taa za barabarani licha ya kuwa mji muhimu unaoiunganisha kanda ya Kaskazini.
Mji huu hauna taa za barabarani kwa sababu zifuatazo:
1. Mpangilio mzuri wa mji. Wengi mtakubaliana na mimi kuwa Moshi ndio mji pekee uliopangiliwa vizuri zaidi..... Njia zote ndani ya mji zinaungana.
2. Mji wa Moshi una mizunguko kwenye maeneo muhimu ya makutano. Mzunguko wa mnara wa mwenge ukitokea au kwenda Arusha, mzunguko wa YMCA unaunganisha njia ya DSM, KCMC, Arusha na kuingia Moshi mjini. Mzunguko wa Clock tower, mzunguko wa Stand ya mboya, mzunguko wa police line.
3. Kuwepo kwa barabara ya njia nne (double roads) katikati ya mji. Magari yanapita mengi kwa wakati mmoja na pia ni rahisi kukatiza kwenye makutano.
4. Mtandao mpana wa barabara. Barabara za Moshi zote zina njia mbadala ikiwa moja itakuwa na foleni na zote zinawezesha kutoka au kuingia mjini.
5. Uelewa mkubwa wa matumizi ya barabara. Wakazi wengi wa Moshi wana uzoefu mkubwa wa kutumia barabara na ni nadra sana kuona "road rage" Moshi. Hata kipindi cha mwezi wa 12 wageni wanapokuwa wengi haijawahi kuwa changamoto.
6. Matumizi ya public transport. Wakazi wengi wa Moshi hutumia zaidi usafiri wa umma (vibasi) kuliko usafiri binafsi. Sio ajabu kukuta tajiri wa moshi akiwa kwenye bajaji akienda ofisini. Hii ni kwa sababu za kiuchumi zaidi 😂
7. Uwepo wa huduma muhimu nje ya mji. Mji wa Moshi sio kila huduma imerundikwa mjini. Huduma nyingi kama mahoteli, hospitali na masoko yako pembeni au nje ya mji.
 
Back
Top Bottom