Ni kwanini Makonda anakagua miradi iliyotekelezwa na Serikali na kisha kuikabidhi kwa CCM?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,498
26,992
Ndugu zangu, au mimi tu sielewi hii kitu!

Nauliza ili nipate kujua, nimekuwa nikishangaa huu mkakati wa Paulo Makonda, RC Dar es Salaam. Sijawahi kuona kabla, pengine ni kwa vile sijui!

Kama hiyo haitoshi, anatumia nafasi hiyo kuwadhihaki watu na kuwananga ikiwa mbunge wa eneo la mradi hatokani na chama chake.

Pamoja na ukweli kuwa serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya chama chake, ni nini kinawapa umiliki namna hii?

Miradi ya maendeleo, miradi ya serikali, ni vipi inakabidhiwa kwa chama? Je, ni mali ya chama?

Maendeleo hayana vyama!

Wasalaam,

Ncha Kali.
 
Back
Top Bottom