Ni kwanini kila tunapozungumzia sababu Kuu za Umasikini hii huwa tunaificha / hatuisemi?

Kuna kitu kinaitwa rasilimali watu ndio hatuna,ukiwa na rasilimali watu bila madini,vivutio wala bandari na bado utakuwa na maendeleo tu lakini ukiwa na hivi vyote bila kuwa na watu wa aina hii, ndio kama tanzania leo wenye elimu zao wanakuja kuchukua wanapeleka kwao
Kweli kabisa.......yaani watu ni maboksi haijawai kutokea.......na miaka inavyozidi kusonga na utashi wa raia unazidi kushuka kila uchao.....
 
Mkuu GENTAMYCINE , hata hili la kuzaa sana mimi nitaitupia lawama serikali. Hivi umeshawahi kuchunguza na kujiuliza ni kwa nini mafukara huzaa zaidi ya matajiri?

Hili ni suala la KIMFUMO na KIELIMU. Ukosefu wa elimu ndio humuongoza mtu kuishi kijima. Kwa jinsi ujima ulivyo, watu ndio nguvu kazi ya kwanza. Mimi nayaona maisha ya kijijini kuwa sababu ya watu kuwa walivyo. Huduma za afya huko sifuri, nani atakuwa amewahi kuongea nao juu ya uzazi wa mpango?
Jami iliyoendelea kielimu inaanza kuzaa baadaye kwa sababu muda mwingi unatumika kwenye elimu kuanzia primary mpaka chuo. Mtu anaanza kuzaa akiwa karibu na miaka thelathini baada ya kumaliza chuo.

Jamii ambayo elimu si kipaumbele watu wanaanza kuzaa hata na miaka 16.

Kuna tofauti ya miaka 14 hapo.

Solution ni kuwapa watu nafasi za elimu.
 
Back
Top Bottom