Ni kwanini kila tunapozungumzia sababu Kuu za Umasikini hii huwa tunaificha / hatuisemi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,947
2,000
Hivi ni kwanini kila kukicha tu Watanzania tunalalamika kuwa maisha ni magumu na wengi wetu kuitupia lawama Serikali / Watawala kuwa ndiyo sababu Kuu ya Umasikini tulionao wengi wetu lakini hapo hapo ama tunajisahaulisha kwa makusudi au hatupendi kusema ukweli kuwa moja ya sababu Kubwa ya wengi wetu kuwa masikini na hali hii ngumu ya maisha ni kupenda Kuzaa hovyo kama Sungura pasipo mpango?

Hivi kwa mfano unakuta Mtu anafanya Kazi ya Mshahara wa Tsh 240,000/ kwa mwezi halafu hapo hapo anakimbilia Kuoa na kuanza Kufyatua Watoto bila mpangilio na kufikia kuwa na Watoto 3 au 4 hali ambayo inapelekea kuanza kushindwa kuwahudumia na maisha yake kuzidi kuwa magumu. Je hapa Serikali / Watawala wanastahili lawama juu ya Umasikini wako uliojitakia?

Leo nitaomba mnipe majibu yenu Kuntu / Mujarab kabisa ni kwanini Watanzania wengi ukweli huu kwamba moja ya sababu Kubwa kabisa ya Umasikini / Maisha magumu tuliyonayo ni kwasababu ya kupenda Kuzaa zaa hovyo kama Sungura bila mpangilio na wengi wetu tukija na sababu za Kipuuzi / Kiupupu kabisa kuwa kila Mtoto anakuja na baraka zake?

Nawasilisha.
 
Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
896
500
Hi kweli Mkuu hiyo yaweza kuwa sababu mojawapo kubwa,lakini upande mwingine yawezekana kuwa masikini amebanwa mno kimaisha kiasi kuwa raha pekee anayoweza pata ni ngono na mkewe,na hivo akauzidisha umaskini wake kwa majukumu kuongezeka. Uchumi wa nchi unaponyanyuka umaskini hupungua kwa kuwa anakuwa na njia nyingine za kustarehe kama tv,smartphone,pombe na kadhalika.huduma za mpango wa uzazi vijijini ngumu kupata na hata zinapopatikana uelewo ni mdogo.
 
Ighombe

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
907
500
Wengi wanaamini kwenye msahafu na bible .Kwamba mungu aliagiza kuwa tuzae,tuongezeke tuijaze dunia,Imani nyingine in ya kuwa uzeeni watoto wanakuwa mkombozi kwa wazee wasiojiweza na hivyo kuwafanya kama raslimali ya siku za uzeeni. Ukichanganya sasa na hiyo dondoo kwamba kila mtoto huja na riziki take ndo kabisa tunazaa hadi watoto 10.Niliwahi kutembelea kijiji Fulani nikakuta hakuna zahanati ,wanaleta mobile clinic lakini kila mama anayekjja ana watoto watatu mmoja mgongoni,mwingine kifuani na wa tatu anatembea.Nikiandika sana nitaambiwa naingilia imani za watu. Msininukuu vibaya!!
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,934
2,000
Kwa waliosoma historia ya Tanzania, miaka ya mwanzo ya Uhuru serikali ilijitahidi sana kupanga mipango ya maendeleo ya miaka mitano mitano.

Serikali ikawa inafikia malengo fulani. Lakini ikajikuta haikidhi kujikomboa kiuchumi, kwa sababu ilianza kwa kupiga hesabu za watu milioni 10 na ikawa haijaweka kwenye umuhimu mfumuko wa watu. Wakati mpango wa miaka mitano unaisha, mfumuko wa watu unakuwa umezidi mahitaji ya huduma za jamii kwa mfano.

Mfumuko wa watu ni tatizo kubwa kiuchumi, hususan katika nchi ambazo hazijajiandaa kwa hilo.
 
Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,123
2,000
Mkuu GENTAMYCINE , hata hili la kuzaa sana mimi nitaitupia lawama serikali. Hivi umeshawahi kuchunguza na kujiuliza ni kwa nini mafukara huzaa zaidi ya matajiri?

Hili ni suala la KIMFUMO na KIELIMU. Ukosefu wa elimu ndio humuongoza mtu kuishi kijima. Kwa jinsi ujima ulivyo, watu ndio nguvu kazi ya kwanza. Mimi nayaona maisha ya kijijini kuwa sababu ya watu kuwa walivyo. Huduma za afya huko sifuri, nani atakuwa amewahi kuongea nao juu ya uzazi wa mpango?
 
Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,546
2,000
Miaka ya 90 au mwanzoni mwa 2000 serikali ya india ilikuwa inatoa TV bure kwa familia masikini ili kupunguza kuzaana.
 
Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,120
2,000
Hivi ni kwanini kila kukicha tu Watanzania tunalalamika kuwa maisha ni magumu na wengi wetu kuitupia lawama Serikali / Watawala kuwa ndiyo sababu Kuu ya Umasikini tulionao wengi wetu lakini hapo hapo ama tunajisahaulisha kwa makusudi au hatupendi kusema ukweli kuwa moja ya sababu Kubwa ya wengi wetu kuwa masikini na hali hii ngumu ya maisha ni kupenda Kuzaa hovyo kama Sungura pasipo mpango?

Hivi kwa mfano unakuta Mtu anafanya Kazi ya Mshahara wa Tsh 240,000/ kwa mwezi halafu hapo hapo anakimbilia Kuoa na kuanza Kufyatua Watoto bila mpangilio na kufikia kuwa na Watoto 3 au 4 hali ambayo inapelekea kuanza kushindwa kuwahudumia na maisha yake kuzidi kuwa magumu. Je hapa Serikali / Watawala wanastahili lawama juu ya Umasikini wako uliojitakia?

Leo nitaomba mnipe majibu yenu Kuntu / Mujarab kabisa ni kwanini Watanzania wengi ukweli huu kwamba moja ya sababu Kubwa kabisa ya Umasikini / Maisha magumu tuliyonayo ni kwasababu ya kupenda Kuzaa zaa hovyo kama Sungura bila mpangilio na wengi wetu tukija na sababu za Kipuuzi / Kiupupu kabisa kuwa kila Mtoto anakuja na baraka zake?

Nawasilisha.

!
!
Kama na wewe ulijua atasema [HASHTAG]#sisiem[/HASHTAG] Gonga like. Atajua idadi yetu kwenye idadi ya likes
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom