Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 23,489
- 70,276
Lobbying kwa lugha rahisi ni kitendo cha mtu au kikundi cha watu kujaribu kushawishi serikali au mwanasiasa/wanasiasa kadhaa waweze kupitisha jambo/sera fulani kwa manufaa ya watu kadhaa.Lobbying ni mini maana yake boss,nitoe tongotongo
Mfano: Dangote ana pesa na anataka kuwekeza Tanzania lakini hana ushawishi au hana uzowefu na sera na mifumo ya uwekezaji wa hapa Tanzania.
Lakini Dangote anafahamiana na Obasanjo ambae anaifahamu Tanzania na ana ushawishi kwakuwa alishakuwa rais wa Nigeria.
Hivyo Dangote anamtumia Obasanjo kufanya lobbying na serikali ya Tanzania ili kumtengenezea mazingira rahisi katika uwekezaji wake.
Nadhani utakuwa umepata mwanga mkuu.