Ni kwanini haukutumia pesa ya boom kujenga au kuendesha biashara kubwa?

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
803
1,000
Kichwa cha habari tajwa hapo juu ni moja kati ya maswali pendwa sana ambayo wahitimu kutoka vyuo mbalimbali huulizwa. Miaka minne iliyopita baada ya kutoka chuo niliulizwa swali hili na baadhi ya ndugu wa karibu wasiowahi kufika chuo. Wengi walihoji kuhusu pesa niliyokuwa nikiipata na wakati huo wakinipa mfano wa watu waliofanikiwa kupitia pesa ya boom na kufanya vitu vikubwa.

Kwangu, swali kama hilo sikutaka kulijibu maana ningelijibu lingenifanya nionekane sina nidhamu. Ninashukuru kwa sasa maisha yanaenda japo sijawahi kutumia pesa ya boom kufanya vitu vikubwa tofauti na kufungua miradi midogomidogo na kuishia kudhulumiwa au kukosa waendeshaji walio wema. Mafanikio yangu leo yanatokana na juhudi zangu binafsi na wala sio zile pesa za chuo ambazo huzuzua vijana wengi.

SWALI: Ni kwa nini haukutumia pesa ya boom kujenga au kufanya miradi mikubwa ya kimaendeleo? Tatizo ni kula bata? Pesa ni ndogo kuliko uhitaji? Majukumu ni mengi kuliko ndoto zako?

Karibuni kwenye mjadala......
 

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
803
1,000
Inategemea faculty gani unasoma.
Kuna course zingine zinahitaji sana fedha ili uweze ku-deliver vizuri projects mbalimbali na presentations.

Hivyo unaweza kuta hata fedha ya boom isitoshe kwa lolote.

Lakini si loan board huwa wanatoa mikopo kwa watu kulingana na uhitaji? Means kama unasoma Petroleum engineering basi utapata boom kulingana na course yako na kama ukisoma BAED pia utapata kulingana na uhitaji.
 

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
803
1,000
Aiseee, nadhani hii ndiyo inasababisha sasa hivi vijana wapewe kwa asilimia.Kumbe zinatosha kuporomoshea mijumba.

Sijawahi kuona mtu kafanya hivyo ana kwa ana ila kwa kupitia ushuhuda wa watu wengine.
 

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
13,537
2,000
Yani 250k kwa mwezi unataka utumie Kufungua biashara au???? Kikubwa cha maana nilimtumia bi mkubwa tu vihela flani..Nikajununulia PC na Smart phone.. Mwaka wa 3 nikaenda kupanga kitaa.. Nikanunua Kitanda..friji..TV na Sofa include viitu vingine vya ndani lakini hapo nilikuwa na Demu mmoja tuLaiti kama ningekuwa mtu wa gambe na mademu ooho hela ile ningeitumbua yote
 

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
803
1,000
Yani 250k kwa mwezi unataka utumie Kufungua biashara au???? Kikubwa cha maana nilimtumia bi mkubwa tu vihela flani..Nikajununulia PC na Smart phone.. Mwaka wa 3 nikaenda kupanga kitaa.. Nikanunua Kitanda..friji..TV na Sofa include viitu vingine vya ndani lakini hapo nilikuwa na Demu mmoja tuLaiti kama ningekuwa mtu wa gambe na mademu ooho hela ile ningeitumbua yote

Mbona kuna wengine shuhuda zao huonesha walifanikiwa kupitia pesa ya boom?
 

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
13,537
2,000
Mbona kuna wengine shuhuda zao huonesha walifanikiwa kupitia pesa ya boom?
Hizo story tu mkuu...!! Ile hela hata sio kitu ukitaka ufanye kitu angalau kionekane lazima Ujinyimee sanaa yani sanaaa unakondeana balaa..

By the way ni kwa watoto wa maskini tu watoto wa wenye pesa Anapata Bumu kama hela ya ziada kwao anapewa pesa ndefu tu ya matumiziiu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom