Ni kwanini Commando huwa ni jasusi mzuri kuliko yule mtu wa kawaida tu aliyepitia mafunzo ya Usalama wa Taifa?

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,629
Nimesikia mahala kuwa COMMANDO (si lazima awe wa Tanzania) ana uwezo wa kupata taarifa nyeti hata kuliko Mwana Usalama Taifa mwenyewe. Kwa mfano; COMMANDO wa Malawi anaweza akaenda nchini Zimbabwe katika maeneo yao muhimu na akapata akitakacho na wala asishtukiwe, lakini kwa Usalama wa Taifa wa Malawi anaweza kwenda ila atagundulika kwa haraka sana tu.

Wajuvi wa haya Masuala mliojazana hapa Jamvini JamiiForums, karibuni mtuelimishe na sisi akina Mzukulu ili nasi tuwe na Maarifa kama nyie pia.
 
Kama unaona Mada ni nzito Kwako kutokana na aina ya Ubongo Tofali ulionao tafadhali waachie walioielewa Wachangie ili nawe Ujifunzie hapo.
Lengo langu ni kuelekea hukohuko katika kutolea ufafanuzi hicho ulichokiwasilisha hapa lakini kabla ya hilo nimependa kuuliza kwanza swali hilo kiutafiti ndiposa tuelekee katika ufafanuzi.
 
Unaona ni upuuzi kwa sababu umesoma kipuuzi. Ungesoma kwa nia ya kutaka kuelewa ungejua nini namaanisha.

Content ya Kipuuzi na iliyotoka pia kwa Mpuuzi inaweza ikaeleweka kwa Mwerevu / Kipanga? Yaani najilazimisha Kukuelewa bado nashindwa tu.
 
Sijawahi kuwa karibu na hao watu. Hivyo siwezi kujua ubora wao katika hizo shughuli zao. Miziziology inahusika kwa hao wenye uwezo wa kupotea katikati ya upepo.
 
Content ya Kipuuzi na iliyotoka pia kwa Mpuuzi inaweza ikaeleweka kwa Mwerevu / Kipanga? Yaani najilazimisha Kukuelewa bado nashindwa tu.
Majibu ya namna hii yanafanya watu wapuuzie uzi wako mkuu, tupingane kwa hoja..mbona jamaa anareply kwa hekima
 
Huyo ni mtu mmoja, huwezi kuwa afisa usalama kama sio komando, kwaiyo unazungumzia mtu mmoja katika kazi tofauti kama ffu na traffic police

Duh....hii ya Leo nayo Kali. Ndugu kumbe hawa Maofisa Usalama wa Taifa wote mfano kutoka TISS ni Makomandoo kwa mujibu wa ulichokisema?
 
Huyo ni mtu mmoja, huwezi kuwa afisa usalama kama sio komando, kwaiyo unazungumzia mtu mmoja katika kazi tofauti kama ffu na traffic police

Mkuu hii comment imenifanya nicheke sana. Maana kuna dogo hapa anapenda kuvaa jezi za Yanga anasemaga yeye ni usalama wa taifa! Kwa hiyo atakuwa ni commando!?
 
Nimesikia mahala kuwa COMMANDO (si lazima awe wa Tanzania) ana uwezo wa kupata taarifa nyeti hata kuliko Mwana Usalama Taifa mwenyewe. Kwa mfano; COMMANDO wa Malawi anaweza akaenda nchini Zimbabwe katika maeneo yao muhimu na akapata akitakacho na wala asishtukiwe, lakini kwa Usalama wa Taifa wa Malawi anaweza kwenda ila atagundulika kwa haraka sana tu.

Wajuvi wa haya Masuala mliojazana hapa Jamvini JamiiForums, karibuni mtuelimishe na sisi akina Mzukulu ili nasi tuwe na Maarifa kama nyie pia.
Kakwambia nani?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom