Ni kwanini CCM wasitumie ule msemo unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Kuna msemo maarufu wa Kiswahili unaosema kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza

Msemo huo una maana sana kwa sasa kwa jinsi siasa zetu zinavyofanyika, kwa kuwa CCM wanaamini kuwa wanawafanyia mazuri sana wananchi wa nchi hii ambayo hayajawahi fanyika huko siku za nyuma na kwa kuwa wao pia wanaamini kuwa wapinzani ni watu wa kupiga domo tu wananchi watakuwa weshajua kuwa hao ni wapiga domo tu, kwa maana hiyo hawatajishughulisha nao na badala yake watawapuuza.

Kwa maana nyingine CCM hawapaswi wajisumbue na wanachoongea wapinzani kwa kuwa wananchi watang'amua kuwa hao ni wapiga domo tu na wanachoongea ni cha uongo, wananchi watawapuuza na kuendelea kuwa na Imani na wao CCM

Lakini kinachofanyika ni tofauti sana na msemo huo kwa kuwa wao CCM ndiyo pekee ambao wanaruhusiwa kufanya siasa nchini na wapinzani wamezuiwa hadi mwaka 2020

Na wakithubutu kufanya siasa hiyo kwa kuwa Kikatiba wanaruhusiwa, basi Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu hapa nchini, ataagiza majeshi "yake" ya Polisi yapige, yaue, na wawakamate viongozi hao wa upinzani na kuwafungulia mashitaka wapinzani kutokana na kukiuka "agizo" lake la kutofanya siasa hadi mwaka 2020!

Wakati hao Polisi wanajishughulisha mno na kuwadhibiti wapinzani wasifanye shughuli zao za kisiasa, wamekuwa wakiwaachia wenzao wa CCM wafanye shughuli zao za kisiasa kadri wanavyotaka!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi hawa CCM hawaujui huo msemo unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?

Kwa kuwa mateso wanayopata viongozi wa upinzani, hususani wa Chadema hivi sasa ni TOO MUCH

Mungu ibariki Tanzania
 
Hatawakifanya mikutano watuhawaendi watuwamesusia mikutanoyao
Sasa ni kitu gani kinachofanya CCM wawapige stop wapinzani kufanya siasa hadi mwaka 2020?

Wakati wao wanaccm wanafanya siasa nchi nzima?
 
Ninaamini kuwa hivi sasa hata wanaccm wenyewe, wengi wao watakuwa hawaridhishwi na mfumo unaoendeshwa hivi sasa hapa nchini, kwa kuwa unajenga visasi vya hali ya juu sana kati ya wanaccm na wale wa upinzani

Kwa kuwa watanzania tumeondoka kwenye utamaduni wetu kama Taifa kwa kujiona wamoja bila kujali tofauti zetu za misimamo ya kisiasa
 
Wanachama wengi wa huko wanaogopa hata kuitwa wanaCCM

Kwasababu wanaonekana tayari ni Wauaji wa watu wasio na hatia.
 
Miaka 56 ya Uhuru binadamu anachangia maji ya kunywa ya kidimbwi na mifugo...
 
Back
Top Bottom