Ni kwanini Akili yangu inazitafsiri hivi Tawala ( Awamu ) zote za Uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Hv bdo wajane wa mwendazake mnarusharusha miguu???ukwl umeshadhihiri
Rusha mabomu leta defenda ila legacy ya magufuli haitopotea kwenye vichwa vya watanzania mfano mzurii nakuomba kasome comment za watanzania wakiskiaTamzania imepata mkopo mahali then njoo unipe jibu
 
Awamu ya Nyerere

Ya Kujenga Misingi na Maadili mema ya Kuwakomboa Watanzania kutoka kwa Wakoloni na Kuzalishwa Kizazi cha Watu Werevu sana.

Awamu ya Mwinyi

Ya Kuharibu Misingi yote iliyowekwa na kusababisha nchi kuanza Kuyumba Kiuchumi huku Rasilimali nyingi za nchi zikinyakuliwa na Wachache ambao waliiweka nchi Mfukoni.

Awamu ya Mkapa

Ya Kuiimarisha Tanzania Kiuchumi na Kielimu huku Taifa la Tanzania likisifika zaidi Kimataifa kwa kuwa na Serikali imara iliyojua kutatua Changamoto za Watanzania huku hata Thamani nzima ya Pesa ( Shilingi ) ikiwa imeimarika sana.

Awamu ya Kikwete

Ya Kuharibu kabisa Uchumi wa Tanzania, uliozalisha Wezi ( Majangili ) na Mafisadi wengu huku pia Serikali ikiwa ndiyo Kimbilio Kuu la Magenge ya Wauza dawa za Kulevya.

Pia ndiyo Awamu iliyozalisha Watanzania wengi ' Goigoi ' na hata ' Mashoga ' wengi waliibukia hapa hapa.

Na ndiyo Awamu ambayo ililemaza Akili za Watanzania wengi huku wakipenda Kupata Pesa kirahisi ( kwa Kupiga Dili ) na Kusababisha Watanzania wengi ( japo siyo wote ) kupenda zaidi Starehe na siyo Kufanya Kazi.

Lakini pia ndiyo Awamu iliyozalisha Chuki za ' Kidiplomasia ' hasa na Mataifa Jirani kama Malawi na Rwanda kiasi cha hata kutaka Kuigharimu nchi ( Tanzania ) kwani Nguvu ya Malawi na Rwanda Kijeshi na Kiusalama zinajulikana na Tanzania ndiyo ingeathirika zaidi.

Awamu ya Magufuli

Ya Kuimarisha zaidi Miundombinu ya nchi, Kurudisha Nidhamu iliyopotea katika Awamu mbovu na ya hovyo ya Rais Kikwete.

Pia ndiyo Awamu ambayo iliwafungua zaidi Akili Watanzania wengi kujua Thamani zao lakini pia kujua Kiwango kikubwa cha Utajiri Tanzania Iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Na ndiyo Awamu ambayo ilijikita zaidi Kuimarisha na Kuboresha ' Kivitendo ' zaidi Ndoto ' Pevu ' za Awamu ya Kwanza.

Hivyo hivyo ndiyo ilikuwa Awamu Bora kabisa iliyoweza Kupambana vyema na Mafisadi na pia Kuwamaliza vyema tu Wahalifu nchini kama Majambazi na hata Wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya.

Vile vile ndiyo Awamu iliyomfanya Mtanzania aweze Kujiamini popote pale, Kujitambua vyema na hata Hadhi ya Elimu nchini kuanza Kuimarika tena.

Na ndiyo Awamu ambayo haikupenda sana ' Kujikomba ' kwa Marafiki ' Wanafiki ' kama ' Wakenya ' ila ikahakikisha inarejesha Uhusiano mwema na Majirani zetu wa ' Kimkakati ' kama Malawi na hasa hasa Taifa ' lililobarikiwa ' zaidi na Mwenyezi Mungu Barani Afrika la Rwanda pamoja na mengineyo tofauti na Awamu mbovu ya Kikwete ambayo iliharibu na ingeigharimu zaidi Tanzania.

Awamu ya Samia

Hii nitawaomba nanyi pia muichambue.
Hakuna awamu ya sita. Kuna Rais wa Sita.
 
Nashangaa sana tunaona aibu kusema huyu ni Rais wa sita tu anayeongoza awamu ya 5. Watu wanataka kupoteza maana ya awamu ya 5 ili watusahaulishe JPM.
 
Kiashiria rahisi kuliko zote
Mwinyi alipaiza inflation rate hadi 56% mwaka 1994
Mkapa akaishusha hadi 20% awamu yake ya kwanza ya mwaka 2004 na baadaye aliporudi akaishusha hadi below 4% mwaka 2009
Kikwete alipokuja ilipanda karibia na 40% mwaka 2014
Magufuli akaishusha hadi arround 4% mwaka 2021

Inflation rate ndio kiashiria pekee ambayo inaonyesha faida au madhara ya uchumi kwa watu wa kawiada kwa sababu inaadhiri bei za vitu na vyakula kwa matumizi ya kila siku

Kwenye miundo mbinu Mkapa ndie aliyeasisi ujenzi wa miundo mbinu nchini na kuweka mifumo dhabiti ya kukusanya kodi na kubana matumizi ili pesa nyingi ziende kwenye usalishaji na huduma za jamii
Kitu ambacho Mwinyi alishindwa kabisa kukusanya kodi na pia Kikwete
Magu alikuja kurudisha huo utamaduni wa kukusanya kodi na kubana matumizi ya serikali ili pesa ziende zaidi kwenye kujenga uchumi kitu ambacho mwinyi na kikwete walishindwa kabisa

Mfano mmoja, kulikuwa na mkutano wa marasi nchini Martekani ezni ya Mwinyi kwa ajili ya kujadili naman ya kupunguza matumizi ya nishati yenye kuongeza hewa ya ukaa kwenye ozone layer
Wawakilishi wa nchi mbalimbali duniani matajiri ikiwemo Marekani yenyewe walikaa kwenye hoteli za kawaid na kwenda na wawakilishi wachache ila mzee wetu mwinyi kwanza alizoa watu wengi kwenye deligation na walilala kwenye hoteli za kifahari mpaka wamerekani wenyewe wakashikwa na butwaa
Tunajua kabisa Kikwete kafanya nini kwenye safari za nje na matumizi ya serikali ambayo ni makubwa kiasi cha kushindwa kutekeleza miradi mikubwa na huduma za jamii kama afya, maji nk. Ukusanyaji wa kodi hafifu na rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Naomba Mungu hii isijirudie tena kwenye hii awamu na zitakazokuja baadaye maana tutarudi kwenye poor country na kusahau uchumi wa kati tulioingia tu majuzi

Tuache siasa Tanzania tunahitaji marais ambao ni strong kama Mkapa na Magu, hata Nyerere hakuwa Strong kama Mkapa na hasa Magu

Magu katuumiza wengi kwa maamuzi yake, hata mimi nimeumizwa sana sehemu fulani na maamuzi yake lakini UKWELI utabaki kuwa UKWELI

We need a strong president like Magu

Kuuona huu ukweli kunahitaji uwezo mkubwa wa kuweka maslahi binafsi pembeni na wa kuona beyond today. Most people will learn it the hard way, sooner or later!
 
Nashangaa sana tunaona aibu kusema huyu ni Rais wa sita tu anayeongoza awamu ya 5. Watu wanataka kupoteza maana ya awamu ya 5 ili watusahaulishe JPM.

Mimi naona acha tu ikae hivyo hivyo inavyowekwa. It’s meaningless kuchanganya time-tested strong leadership ya JPM na hii experimental leadership!
 
Back
Top Bottom