Ni kwamba Watanzania wengi tuna roho mbaya au wivu na husuda tu? Lini tutabadilika?

Marias

Member
Apr 6, 2018
61
158
Habari zenu wanabodi,

Kuna jambo niliobserve kwa muda sana na leo nimejikuta natype hapa ili kushare na wenzangu ambao wamewahi kulifikiria hili .

Miaka ya hivi karibuni husasani kipindi hiki cha awamu wa 5 na hasahasa sasa hivi kumekuwa na trend za tumbuatumbua na kuhoji watumishi na viongozi wengine hadharani huku wananchi wakipiga kelele kuonesha either mtumishi huyo au kiongozi husika hafai na kama ilivyotokea leo huko nachingwea mtu alipopewa fursa ya kuongea alisema yeye anachotaka ni mtu kutumbuliwa tu.

Nimekuwa nikipitia post mbalimbali hususani pale mtu anapotumbuliwa au kushtakiwa unakuta wengi wanasema huyo ni mhujumu uchumi etc etc lakini ukija in details unakuta mtu huyo wala sio mbaya na wengi wanaocomment wala hawamjui zaidi ya kumsikia siku hiyo, ila unakuta ndiyo kwanza wanataka asulubishwe asulubishwe.

Najiuliza hii mob ya wapiga kelele kwenye mikutano na mitandaoni huwa haina ndugu ambao ni watumishi wa umma? Haina jamaa na marafiki huko kwenye utumishi? Kwa nini inahukumu bila ata kujua ukweli uko wapi? Likimpata mtu ambaye mpiga kelele au watoa hukumu hao wana vinasaba naye, will it be the same?

Hiki kitu nashindwa kuelewa ni notion iliyopandikizwa kuwa kila mtu anayedhalilishwa ni mwizi kweli au ni wivu wetu tu sisi Watanzania? Ni husda au ni chuki tu na watu ambao ata hatuwafahamu muda mwingine?

Kuna muda binafsi huwa najikuta naumia na kushangaa kwa nini tunafika hapa. Naomba mawazo yenu wanabodi kuhusu hili jambo, ni nini hiki kimetufanya hivi? Tunafurahia matatizo yanapompata mtu hata kama hatumjui?
 
Jiwe anajenga chuki na uhasama tu, hukuna kitu anafanya akae pembeni tu inatosha yaani
IMG_20191015_010450.jpeg
 
Actually ni roho mbaya tu na chuki. Hili jambo limeanza zamani hata kipindi cha JK. Kama unakumbuka siku Prof. Tibaijuka anang'olewa na JK pale Diamond, umati wote ukifurika kwa shangwe bila kujali kuwa yule mama alipewa "visenti" tu ukilinganisha na mzigo uliochukuwa Escrow. Hivyo, waTZ wengi wana husda, roho mbaya na chuki kwa watu wanaonekana kufanikiwa kidogo.
 
Mkuu, ulianzia mbali mno. Ebu tuangazie tu huku mitaani kwetu yaani mtu ukipata off ya wiki moja au ka-likizo ka ghafla watu wanafurahi wakidhani umefukuzwa kazi, kila wakikuona utaskia vipi mbona hauendi kazini siku hizi jamani?? Yaani huku ametabasamu kabisa shubaamiti mkubwa....
 
Hayo ni yale ma-loser ambayo wakati mwingine hata nauli ya daladala yanakuwa hayana!

Sasa ma-stress ya njaa, kukimbiwa na mademu kwavile hawana ubavu wa kutoa matunzo (chunguza tu, wengi ni wanaume wenye hizo tabia), na mambo mengine kibao kama hayo, yanawafanya yawe na mioyo iliyojaa chuki, wivu, inda na husuda mbaya!!!
\
Matokeo yake, yakisikia mtu kapatwa janga, yenyewe yanafurahia!! Yanafurahia kwa kuamini hatimae na wao watakuwa kwenye msoto yeye bila kufahamu aliyekutangulia kakutangulia tu!!

Na lingine ni hii mijitu ambayo imezaliwa na roho za kimaskini! Hii ni ile ingawaje yenyewe haina shida lakini inapenda kuona wengine wakiwa na shida! Na kwa kawaida hawa wanakuwa wale ambao hata kama sasa wana pesa lakini walikulia kwenye maisha ya umaskini wa kutupwa, huku pia wakiwa na mioyo ya kimaskini!!

Hii ni ile mijitu ambayo haiamini katika own hustles!

Na ndio hiyo hiyo yakiona mtu kapiga hatua, basi lazima yatauhisha na uchawi, Freemason, wizi na upumbavu mwingine kama hayo! Kwavile yenyewe imeshindwa kuwa na akili angalau ya kuwapatia ugali wa uhakika, basi inadhani kila mtu ana akili mbovu kama zake!

Amini amini nakuambia... kupoteza kuku mmoja pale Soko la Kisutu, ni hasara kubwa kwa taifa kuliko kupoteza mijitu 100 ya aina hii!
 
Wengi wa wanatanzania tumeingia kwenye umasikini na mdidimio wa kiuchumi hivyo ikitokea kuna member mpya anaetaka kujiunga nasi haswa aliekuwa juu kuna ile kufurahi na kujiona hatupo peke yetu kweny hii dhiki na huwa tunafurahishwa kuona kuna mwingine anataka kushushwa na kujiunga nasi.
IN SHORT ROHO ZA MASIKINI NA WALIOKATA TAMAA NDIVYO ZILIVYO NA NDIYO MAANA HATUBARIKIWI NA TUNAZIDI KUOZEA KWENYE DHIKI.
 
Yatupasa kuzikemea hizo roho za kimasikini kwa nguvu zote,kila mmoja kwa dini yake!
 
Hah
Mkuu, ulianzia mbali mno. Ebu tuangazie tu huku mitaani kwetu yaani mtu ukipata off ya wiki moja au ka-likizo ka ghafla watu wanafurahi wakidhani umefukuzwa kazi, kila wakikuona utaskia vipi mbona hauendi kazini siku hizi jamani?? Yaani huku ametabasamu kabisa shubaamiti mkubwa....
hahahahhaha na kuanza kutangaziana fulani katumbuliwaa
 
Actually ni roho mbaya tu na chuki. Hili jambo limeanza zamani hata kipindi cha JK. Kama unakumbuka siku Prof. Tibaijuka anang'olewa na JK pale Diamond, umati wote ukifurika kwa shangwe bila kujali kuwa yule mama alipewa "visenti" tu ukilinganisha na mzigo uliochukuwa Escrow. Hivyo, waTZ wengi wana husda, roho mbaya na chuki kwa watu wanaonekana kufanikiwa kidogo.
Nimekumbuka ile Siku,Poor us Tanzanians
 
Hayo ni yale ma-loser ambayo wakati mwingine hata nauli ya daladala yanakuwa hayana!

Sasa ma-stress ya njaa, kukimbiwa na mademu kwavile hawana ubavu wa kutoa matunzo (chunguza tu, wengi ni wanaume wenye hizo tabia), na mambo mengine kibao kama hayo, yanawafanya yawe na mioyo iliyojaa chuki, wivu, inda na husuda mbaya!!!
\
Matokeo yake, yakisikia mtu kapatwa janga, yenyewe yanafurahia!! Yanafurahia kwa kuamini hatimae na wao watakuwa kwenye msoto yeye bila kufahamu aliyekutangulia kakutangulia tu!!

Na lingine ni hii mijitu ambayo imezaliwa na roho za kimaskini! Hii ni ile ingawaje yenyewe haina shida lakini inapenda kuona wengine wakiwa na shida! Na kwa kawaida hawa wanakuwa wale ambao hata kama sasa wana pesa lakini walikulia kwenye maisha ya umaskini wa kutupwa, huku pia wakiwa na mioyo ya kimaskini!!

Hii ni ile mijitu ambayo haiamini katika own hustles!

Na ndio hiyo hiyo yakiona mtu kapiga hatua, basi lazima yatauhisha na uchawi, Freemason, wizi na upumbavu mwingine kama hayo! Kwavile yenyewe imeshindwa kuwa na akili angalau ya kuwapatia ugali wa uhakika, basi inadhani kila mtu ana akili mbovu kama zake!

Amini amini nakuambia... kupoteza kuku mmoja pale Soko la Kisutu, ni hasara kubwa kwa taifa kuliko kupoteza mijitu 100 ya aina hii!
Hahahahaha hakika wala hujakosea, kupoteza kuku mmoja kisutu ni hasara kwa taifa kuliko mijitu 100 ya aina hii” This statement speaks volume
 
Mtu masikini (hasa mwafrika) siku zote anafarijika sana akiona mtu mwenye uwezo anataabika, awe amefanya kosa ama la. Inaleta hali fulani ya usawa kwamba tunateseka wote.
Kuna mtaalamu mmoja wa Karne ya 15 mfaransa Philippe Duvour alisema kuwa mtu ambaye hufurahia kuona mtu mwenye uwezo akitaabika au muonea Wengine hupata majibu maeneo yafuatayo la kwanza aweza pigika kiafya kwa maradhi mabaya yeye binafsi au wanafamilia,pili Watoto wake kutofanikiwa ,na yeye kutoishi maisha ya furaha .
 
Back
Top Bottom