Ni kwa sababu gani hatusheherekei Uchaguzi Mkuu?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Waungwana

Siku ya Uchaguzi Mkuu huwa siku maalum ambapo shughuli zote za kikazi zilizo rasmi husitishwa kwa muda, ili kuwawezesha Watanzania wenye haki ya kupiga kura, na waliojiandikisha kupiga kura, waweza kwenda kupiga kura kwenye vituo ambapo wameandikishwa.

Tangu Uhuru, Watanzania wamepiga kura kwa miaka mingi sasa, kuanzia zama za chama kimoja hadi zama hizi za vyama vingi. Lakini kabla ya zama za chama kimoja kulikuwa na vyama vingi pia, kwa hiyo suala la vyama vingi sio geni kama linavyoonekana.

Haki ya kupiga kura ni haki iliyoainishwa kwenye Katiba, kwa hiyo ni haki ya msingi kabisa kwa kila Mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18. Lakini cha kushangaza, haki hii ni kama vile imedharauliwa, kwani hakuna mtu yeyote mwenye fikra kwamba siku ya Uchaguzi Mkuu inapaswa kuwa sherehe kama siku nyingine, lakini si kwa mtazamo wa kuadhimishwa, bali kusheherekewa, haswa baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika ifikapo saa 12 jioni, ambapo vituo vya kupiga kura hufungwa na hatua ya kuhesabu kura huanza na kukamilika.

Je, ni kwa sababu gani sisi Watanzania hatusheherekei siku hii muhimu kwetu wote?

Asanteni.

-> Mwana wa Haki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom