Ni kwa nini Watanzania hasa vijana tunapenda kuwa vijiweni mada kuu huwa ni mpira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwa nini Watanzania hasa vijana tunapenda kuwa vijiweni mada kuu huwa ni mpira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dosama, Mar 22, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Great thinker

  Watanzania hivi tumelogwa tunapenda starehe kuliko kazi hapa napopita nakutana na vijana mbaya zaidi ni karibu kila mtaa bapopita kufika nakoishi vigenge vya vijana huvikosi cha ajabu kikubwa ktk mazungimzo yao ni mpira tena vilabu vya Uingereza na Hispania wanavyopanga vikosi na kuonyesha kauli za umiliku wa timu kama vile wao ni mameneja wasaidizi wa timu hizo.

  Vijiwe vya watu wazima na makamoni habari za wake za watu na kufumaniana

  Tutafika kweli?

  Najiuli
   
 2. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sasa weye mkuu, utaweza kubadiri hobby na tabia za watu wawe kama weye?
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,524
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Siku hizi kuna vijana wameanzisha style mpya. Wanashinda kwenye nyumba za ibada, shule hawaendi kazi kufundishana kuchukia wengine
   
 4. K

  Koffie JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  halafu tunalalamika maisha bora
   
 5. zagalo

  zagalo Senior Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  we unataka wajadili nini?
   
 6. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wafanye kazi
   
 7. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hakuna starehe kama mpira,siasa kwa nchi kama yetu nikujipa stress tu,mimi m1 wao napenda story za soka sana hasa la wenzetu,mpira wa ulaya ndio wenyewe sio wa kibongo majungu tu na kupiga marefa,
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Well, wewe hapa upo kwenye kundi gani?........maana huwezi kuyafahamu haya kama wewe si miongoni mwao! na kama una nafasi ya kazi uliwahi kumpa kijana mwenzako connection akakataa? kuwa wewe na kibaruwa isiwe kigenzo cha kuwaona wenzako hawana akili, nakuomba kama una notebook andika maneno haya, "THERE IS NO PERMANENT SITUATION IN LIFE".
   
 9. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Kaka ni ukweli mpira burudani but watanzania tumezidi, unakuta dume linaipenda manchester kuliko ferguson anavyoipenda, badala ya kufanya kazi au biashara mda wote manchester halafu mwisho wa siku linalalamika maisha magumu,

  Career world imenifundisha vitu vingi sana, kikubwa ni use your time and muda haurudi nyuma, wenzako wakina rooney, messi ronaldo na wengineo wapo kazini pale tunapowaangalia, ilo neno niliambiwa na mzungu mmoja hivi baada ya kutukuta tunabishana mpira muda wa kazi kipindi ndo nimeajiriwa direct from varsity,

  So tubadilike wadau marekani imejengwa na wamarekani na tanzania itajengwa na watanzania wenye moyo
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hiyo Avatar yako inakusuta na kuonesha wewe ni wale wale tu hapa unacholeta ni uchakumbi tu wala hakuna lingine!!....
   
 11. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna hatari ukaja kushambuliwa na mashabiki wa soka. Hata hivyo hoja zako ni za kweli kabisa. Pamoja na watu kutetea kuwa kila mtu ana hobi zake lakini ni lazima hobi ziendane na ufanyaji kazi. Vijana siku hizi ni Man U tu na Barcelona. Wanajimilikisha timu. Watu wanaoelekea kuwa wamesoma kiasi fulani wanashabikia Uingereza na wale wanaoonekana kuwa na elimu ya chini zaidi wanabishana mambo ya Simba na Yanga (bila hata kujali viwango vya timu). Ulaya ndiko kwenye soka lakini si kawaida kwa wenzetu kujadili mambo ya mpira kwa kiwango cha kusahau kufanya kazi. Kwa kweli ni tatizo kubwa mno. Vyombo vya habari kwa kutambua hili vina-take advantage kwa kuandika yale wapenzi wa soka wanayopenda kusikia kama "Sunzu full baruti" au "Yanga kuigaragaza Zamalek." As long as mentality hizi zinaendelea nchi zetu zitaendelea kuwa masikini. Maneno yamekuwa mengi mno kuliko kazi.

  Lakini pia usishangae sana, hii ndiyo Afrika. Afrika kwa sehemu kubwa haina inacho-export in terms of utamaduni, biashara na burudani inaishia ku-import tu ndiyo maana mabishano ya Yesu ni Mungu na Yesu si Mungu utayasikia sana huku. Afrika ina majukumu machache ya kufanya sasa isipofanya haya itafanya nini instead?
   
 12. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuwa na nafasi ya kazi ama kibarua si kigezo cha kufanya kazi. Matola hivi umeshaona namna wafanyakjazi wengi wa halmashauri zetu wanavyofanya kazi (Wanavyoishia kupiga porojo)? Ukifika katika ofisi za Serikali utaishia kuambiwa njoo kesho, watu wako bize na ratiba za burudani. Matola usiishie kuniomba nikupe connection za kazi, nitakupa connection lakini bidii yako ikoje? Huishii kuzungumzia Liverpool? Au ndiyo kazi na dawa?
   
 13. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,738
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba, vijana tunakwepa au ni wavivu wa kujadili mambo magumu na ambayo yanajenga mustakabali wetu. Soka ni burudani, je baada ya burudani??????
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Labda unajichanganya mwenyewe mimi hapa sizungumzii wazembe kazini na mimi ni mmoja wa watu wakorofi ninapofika sehemu kupata huduma halafu watu hawatimizi wajibu wao, hapa nilikuwa nina maana si wote ambaop wako benchi ni wazembe au hawana akili kuna watu wamekosa fursa tu lakini kama una connection ukiwapa utashangaa mwenyewe wanavyowajibika.

  Kwanza mimi mambo ya kijinga kushabikia mipira kama zuzu ndio siyapendi kabisa kwa sababu naufahamu mpira ukishakuwa teja wa upenzi wa mpira unakuwa kama zuzu, hata rafiki zangu wananishangaa mpaka leo hawajui mimi nashabikia timu gani Uingereza kumbe mimi sina timu huwa naangalia tu kama just a fun na huwa naamuwa siku hiyo niipende timu ipi!.......i have nothing to lose in football.
   
Loading...