Ni kwa nini viongozi wengi wa Africa wanapenda kung'ang'ania madarakani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwa nini viongozi wengi wa Africa wanapenda kung'ang'ania madarakani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Obi, Jan 28, 2010.

 1. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mara nyingi sana tumeshuhudia vurugu na machafuko yaliyopoteza maisha ya watu wakiwepo watoto wagodo wasio na hatia katika nchi zetu hizi za Africa. Machafuko na vurugu hizo yanaambatana na mambo mengi mabaya yakiiwemo ya ubakaji na mauaji ya kutisha sana. Sio hayo tu ni mengi sana yakiwepo ya wananchi wa nchi husika kuwa wakimbizi na wengine kuwa ombaomba na kukosa mwelekeo katika maisha yao.
  Vurugu na machafuko hayo yanasababishwa na baadhi ya viongoozi wa nchi husika kung'ang'ania madaraka hata kama chaguzi huru na za haki zikiwa zimefanyika na wananchi kuwachagua viongozi wao wanaowapenda. Mifano ni dhahiri sana. Kwa mfano tumeshuhudia vurugu na machafuko yaliyotokea katika nchi ya jirani Kenya. Uchaguzi umefanyika lakini watu hawataki kukubaliana na matokeo ya uchaguzi huo. Zimbabwe nako mambo ni yaleyale viongozi hawataki kukubaliana na matokeo.
  Najiuliza kukataa huko matokeo ni kwa maslahi ya nani hasa? Je ni kwa ajili ya nchi na wananchi wake au ni kwa nini hasa?
  Katika utawala wa Dk. Salmin Amour Juma, aliyekuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya tano, walitokea watu na wapambe waliomshawishi kutaka kubadilisha Katiba ya Zanzibar , ili imwezeshe kuendelea kuongoza visiwa hivyo, kwa muhula wa tatu. Hilo lilishindikana. Nakumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema “ Muogopeni kama ukoma mtu anayetaka kuingia Ikulu, kwa gharama yoyote hata kwa kutoa rushwa, kwani Ikulu ni mzigo mkubwa kwa jamii". Alisema kuwa Ikulu ni tatizo kubwa kwa sababu ukiwaona watu wana njaa, wana shida, wana maradhi na hata matatizo mengine yote, hayo yanakuhusu wewe, kwani hao ni watu wako waliomo katika nchi yako, hivyo kila kinachowasumbua kinakuhusu.
  Katiba ni kitu cha kuheshimiwa sana kwa sababu ndio muongozo wa Nchi yeyote katka Dunia hii.
  Huku kungangania madaraka kwa baadhi ya viongozi wetu wa kiafrika ni kwa maslahi ya nani? Kuna nini ikulu? Kuna biashara gani zaidi ya kuwasaidia watu?
  Mungu Ibariki Taifa letu la Tanzania.

  Naomba kuwasilisha

  Obi

   
 2. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ufisadi tu ndio unawasumbua...
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uroho na tamaa ya kundelea kupata fedha kwa urahisi kwa kutumia madaraka na kuishi maisha ya kifahari ambayo hawakuwa nayo kabla ya kupata madaraka
   
 4. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kicheruka

  Ni uyasemayo ni ya kweli. Inabidi tutafute mbinu ya kuwakabili watu wa namna hiyo ili tuweze kuwa na maendeleo na sio vita tena. Ninaamini siku moja Bara la Africa litaungana na kuwa na safaru moja kama wenzetu wa European Union. Halitakuwa tena Bara la machafuko wala Bara la mateso tena. Litakuwa Bara lenye amani na upendo kwa watu wote. Yote haya yatawezekana wananchi wakiungana kwa pamoja kusema NO kwa mafisadi na wapenda madaraka (Fond od Power People)
   
 5. P

  Pepe Rainer Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna msemo wa kiingereza unaosema, charity begins at home,amani unayoiongelea inabidi ianze ndani ya nchi yetu.tukiangalia uchaguzi wa tarime ambapo chama tawala kilishiliki kwa sehemu kubwa kusababisha vurugu na kuvuruga amani katika uchaguzi mdogo kwa kutumia police je hiyo amani katika Africa itawezekana kama hata katika uchaguzi mdogo ndani ya nchi yetu ilitoweka.
  serikali inapaswa kuheshimu uwepo wa vyama vingine na kutotumia migambo au police kuvuruga na kuwatisha watanzania ili uchaguzi uwe huru

  watu wa kenya waliigia katika machafuko na sisi twaweza ingia katika machafuko kama uchaguzi utaendelea kuwa sio huru na wa kulazimisha chama fulani kuendelea kushika madaraka hata kama wananchi hawamtaki kiongozi wake.

  uchaguzi wa 2005 ni uchaguzi uliokuwa umejaa rushwa,na viongozi wetu wa juu wa nchi kushinda kwa kishindo kwa rushwa

  Viongozi wetu yawapasa kuelewa nini maana ya demokrasia na kuitekeleza katika vitendo kwa kulekebisha sheria za uchaguzi na uchaguzi kufanyika kwa uhuru na haki na kuto ingilia uchaguzi kama kwa kutumia police na mgambo

  yote uliyajadili kwa Afrika yako nchi ketu na yatupasa wote kufanya mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya taifa letu na Afrika kwa ujumla
   
Loading...