Ni kwa nini TFF wanamuogopa Michael Richard Wambura?.......Mizengwe yote hii ya nini?... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwa nini TFF wanamuogopa Michael Richard Wambura?.......Mizengwe yote hii ya nini?...

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Oct 27, 2011.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Salama wakuu wangu wapenda michezo....

  Kwa muda mrefu nimegundua kwamba TFF ya Leodgar Chilla Tenga imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha kwamba Michael Richard Wambura kwa namna au njia yoyote ile hashiriki shughuli za TFF.......Je tatizo ni nini hasa?.......Wanamuogopa?.......Ni kwa nini mara zote wamekuwa wakimuwekea mizengwe kiasi cha kukataa hata Rufaa zake mara anapoenguliwa katika kugombea uongozi,mfano juzi jina lake lilienguliwa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Mara na jana alipojaribu kupeleka rufaa yake kupinga uamuzi huo watendaji wa TFF pale Ilala walikataa katakata kuipokea Rufaa hiyo.............Kunani?

   
 2. u

  utantambua JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wote wanabaniana tu ulaji. Siiependi TFF (zamani FAT) imekaa kifisadi sana hakuna mianya ya uwajibikaji. Watendaji karibu wooote wako after their own bellies
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hawamuogopi bali hawamtaki........namjua Michael vizuri sana toka tukiwa watoto.......a very hard man to please and work with....na system in mkono katika kumbania pia
   
 4. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  He is a criminal, FULL STOP!!! Mbona hujauliza kwa nini kafukuzwa uanachama Simba???
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Michael anatakiwa kupeleka malalamiko yake kwenye vyombo vya sheria bila kujali upuuzi wa FIFA wa kuzuia masuala ya michezo kupelekwa kwenye mahakama za kawaida.

  Vinginevyo hawatoheshimiana na TFF kamwe.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Ni yeye tu na kimbelembele chake alikuja kujikuta ametengeneza maadui wengi.Binafsi namshauri aishi maisha engine nje ya soka.Yeye si ni fundi cherehani bana.
   
 7. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,268
  Likes Received: 4,238
  Trophy Points: 280
  Acha kumpakazia ,mbona RAGE alifungwa jela lakini still amerudi kwenye uongozi wa soka.Hakuna sababu ya msingi kumkataa Wambura halafu matapeli kama Rage,Hasanoo wameruhusiwa kugombea uongozi wa soka.Kwa kifupi Leodgar Tenga ameshindwa kazi TFF alianza vizuri lakini sasa amekuwa hana tofauti na kina Ndolanga.Hata wachezaji wenzake aliocheza nao wanasema jamaa ni mbishi
   
 8. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Ni nani mhalifu kati ya mwizi ISMAIL ADEN RAGE aliyefungwa jela na baada ya kutoka akpewa uongozi wa Moro Utd na baadae Simba?......Ni kwa nini mwizi kama RAGE alipewa fursa ya kugombea uongozi na kupewa lakini WAMBURA ananyimwa?......
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kiukweli TFF ya Tenga ni bora hata ya FAT ya Ndolanga......Wanamuogopa WAMBURA kwa sababu wanajua atawabania kwenye masuala ya pesa

  TFF ya Tenga ni wezi wa kutupwa,wao wanachoangalia ni pesa tu na si maendeleo ya soka.....Mikataba ya udhamini ni mibovu, ratiba ya ligi inabadilishwa kila uchao......

  TFF wao ni PESA mbele maendeleo ya soka NYUMA......

  Wanakera kweli
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Hawa TFF wana nini na Wambura?......Je Leodgar Tenga na Angetile Osiah wanamuogopa Wambura?.....Zengwe lilianzia kwenye uchaguzi wa TFF mwaka 2004,likaja kwenye uchaguzi wa Simba 2010, baadae likahamia kwenye uchaguzi wa FA ya Mara mwaka 2011 na sasa limehamia DRFA........Lazima kuna kitu hapa.....Si bure

  TFF yaanza ‘fitna' tena kwa Wambura


  na Juma Kasesa

  SAA chache baada ya Chama Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kuanika tarehe ya uchaguzi wa chama hicho, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeibuka na kudai kuwa, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Soka Tanzania (FAT), sasa TFF, Michael Wambura, hana sifa za kugombea.
  Tayari Wambura, alishaonyesha nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa DRFA, baada ya kupewa baraka na Kamati ya Rufaa chini ya Profesa Mgongo Fimbo.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema uamuzi uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo, kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Mkoa wa Mara (FAM), alikokuwa akiwania nafasi ya uenyekiti, haumhalalishi kuwania uongozi, kwa kuwa mzimu wa tuhuma za kukosa uadilifu na kupeleka masuala ya soka mahakamani bado unamuandama.
  Wambura alikatiwa rufaa na mmoja ya wagombea wa uchaguzi wa FAM, Titus Osoro, kwa kile alichodai hakuwa na sifa za kuwania uongozi, ambapo Kamati ya Uchaguzi ya TFF, ilimuengua kabla ya mgombea huyo kukata rufaa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, ambayo iliitupilia mbali kwa kuwa haikuwa na mamlaka kusikiliza rufaa za masuala ya uchaguzi.
  Alisema uamuzi wa Kamati ya Rufaa, kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM baada ya mgombea huyo kupinga uamuzi wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, haujamuondolea tuhuma zilizokuwa zikimkabili awali, ambapo mara mbili ameishazuiliwa kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali za michezo ikiwamo ndani ya shirikisho hilo.
  Osiah alisema kilichoamuliwa na Kamati ya Rufaa ni kutupilia mbali rufaa ya Osoro dhidi ya Wambura, kwa kuwa haikufuata taratibu za kisheria ambapo mkata rufaa alipaswa kuanzia ngazi mkoa, lakini badala yake alianzia ya taifa, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
  Alifafanua kuwa kilichoamuliwa na kamati hiyo ni kumrejesha Wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa FAM, japo kuwa uchaguzi wake ulikuwa umeshafanyika ambapo ilieleza Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilifanya makosa kumuengua mgombea huyo kwa kutumia rufaa ya Osoro ambayo haikuwa halali, lakini siyo kumsafisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili mgombea huyo.
  Alibainisha kuwa kwa mujibu wa katiba ya TFF, maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ni ya mwisho, hasa kwa uchaguzi unaohusu ngazi ya mkoa na wilaya, isipokuwa kwa uchaguzi wa ngazi ya kitaifa, ambapo Kamati ya Rufaa ndiyo inaweza kuingilia maamuzi ya kamati hiyo.
  Katibu huyo alisema katiba inafafanua kuwa Kamati ya Rufaa inasikiliza shauri lisilo la uchaguzi, hivyo uamuzi wake wa kuingilia maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi umeleta mkanganyiko ambapo sekretarieti ya shirikisho hilo imelazimika kuiandikia barua Kamati ya Sheria, Haki na Hadhi za Wachezaji, kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu muingiliano wa maamuzi wa kamati za TFF.
  Kabla ya DRFA kuanika tarehe ya uchaguzi huo ambayo imepangwa kuwa Machi 18, tayari Wambura ameonyesha nia ya kuwania uongozi wa chama hicho, ambacho mwenyekiti wake ni Amin Bakhresa huku katibu akiwa ni makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, hivyo kuonyesha kuanza kupanda kwa homa ya uchaguzi huo.   
 11. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ndugu yangu;
  yote hiyo ni njama tu za tff za kutaka kumzibia wambura. Kwani hata barua ya kumsafisha iliandikwa katibu mkuu wa tff bwana osia. Lkn jana tena huyo isia anajichanganya tena ktk hili suala la wambura. Nafikiri ni mizengwe tu za tff, kwani nchi hii kila kitu kiko hovyo.
   
Loading...