Ni kwa nini rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar hapewi nafasi ya kukagua gwaride la muungano?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Huwa nashuhudia gwaride la sherehe za kumbukumbu ya muungano likikaguliwa na rais wa jamhuri ya muungano pekee wakati muungano una serikali mbili? Kwa nini rais wa Zanzibar naye asiwe anapewa kanafasi japo ka kukagua gwaride la mgambo tu?
 
Jibu liko kwenye RED hapo juu! Baadaye nafikiri utauliza kwa nini Dr Shein, Rais wa Zanzibar asihamie Ikulu ya Magogoni eti kwa kuwa na yeye ni Rais!! Kaaazi kweli kweli!
 
rais wa zanzibar anashinda kwa kura laki nne ni sawa na kura alizopata mmbunge wa Ilemela
 
Kwani ulishawahi kumuona rais wa Tanganyika akikagua gwaride la muungano? Kama siyo, iweje sasa udai rais wa zanzibar akague gwaride?
 
Huwa nashuhudia gwaride la sherehe za kumbukumbu ya muungano likikaguliwa na rais wa jamhuri ya muungano pekee wakati muungano una serikali mbili? Kwa nini rais wa Zanzibar naye asiwe anapewa kanafasi japo ka kukagua gwaride la mgambo tu?

Huwa anakagua gwaride siku ya kuazimisha Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Jibu liko kwenye RED hapo juu! Baadaye nafikiri utauliza kwa nini Dr Shein, Rais wa Zanzibar asihamie Ikulu ya Magogoni eti kwa kuwa na yeye ni Rais!! Kaaazi kweli kweli!

Ahaa! Kwa hiyo ukishakuwa rais wa muungano basi unameza na ule uungano pia? Japokuwa huyu ni rais wa jamhuri ya muungano lakini Zanzibar nayo ina serikali, rais, bendera na wimbo wa taifa ndani ya muungano. Yote kwa yote nimeuliza tu. Rais wa Zanzibar hawezi kukaa magogoni wakati naye ana ikulu yake ya kujidai. Inawezekana sherehe hizi za muungano haziwahusu sana wenzetu.
 
rais wa zanzibar anashinda kwa kura laki nne ni sawa na kura alizopata mmbunge wa Ilemela

Lakini si rais? Kama tatizo ni wingi au uchache wa kura si apewe hata mgambo wa majiji? Pamoja na kura chache kumbuka kuwa naye ni rais.
 
We we we we lazima gwaride likaguliwe na rais wa jamhuri ya muungano ndo boss kwani ulishawahi kujiuliza kwa nini sherehe hizi hufanyika tanzania bara tu!
 
Rais wa Zanzibar yupo na tunamuona, Jee Rais wa Tanganyika yuko wapi nae japo ahudhurie tu sherehe?
 
Huwa nashuhudia gwaride la sherehe za kumbukumbu ya muungano likikaguliwa na rais wa jamhuri ya muungano pekee wakati muungano una serikali mbili? Kwa nini rais wa Zanzibar naye asiwe anapewa kanafasi japo ka kukagua gwaride la mgambo tu?

na kwanini rais wa muungano mala kwa mala haonekani zanzibar? ama kwanini mawaziri kama kina magufuri,mwandosya hawaonekani zanzibar,lazima tujiulize pia hilo,na hayo ndiyo maswali ya kuyauliza ktk mchakato wa katiba mpya ili kuweza kuondoa kasoro za muungano
 
Hivi waziri mkuu na rais wa zanziba nani bosi wa mwenzake?
 
na kwanini rais wa muungano mala kwa mala haonekani zanzibar? ama kwanini mawaziri kama kina magufuri,mwandosya hawaonekani zanzibar,lazima tujiulize pia hilo,na hayo ndiyo maswali ya kuyauliza ktk mchakato wa katiba mpya ili kuweza kuondoa kasoro za muungano

Je, rais wa muungano anaweza kutoa amri kwa rais wa Zanzibar, au kumuwajibisha?
 
Jibu liko kwenye RED hapo juu! Baadaye nafikiri utauliza kwa nini Dr Shein, Rais wa Zanzibar asihamie Ikulu ya Magogoni eti kwa kuwa na yeye ni Rais!! Kaaazi kweli kweli!
Buchanan hilo ndiyo jibu lenyewe kwa wale wanao jifanya wana uelewa mdogo, ili hali ktu kiko wazi kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom