Ni kwa nini nguruwe anaitwa kiti moto?

Yaliwa ikiwa na moto, kwenye kiti huwezi tulia
kwa kuwa lake joto, ni utamuwe asilia
si mkubwa wala mtoto, ya moto hupendelea
kikipikwa kitimoto, kula hutachelea

HONGERA SANA.
Masahihisho (Una shida kwenye mizani. Shairi ni vina na mizani)

Yaliwa ikiwa moto, kitini hutotulia,
Iwapo na lake joto, utamuwe asilia,
Mkubwa hata mtoto, ya moto hupendelea,
Ikipikwa kitimoto, kula hautochelea,
 
Yaliwa ikiwa na moto, kwenye kiti huwezi tulia
kwa kuwa lake joto, ni utamuwe asilia
si mkubwa wala mtoto, ya moto hupendelea
kikipikwa kitimoto, kula hutachelea

Yaliwa ikiwa moto, kitini hutotulia,
Ikiwa na lake joto, utamuwe asilia,
Mkubwa hata mtoto, ya moto hupendelea,
Ikipikwa kitimoto, kula hautachelea.
 
Miss Judith umotomoto kama kitimoto. Mahesabu fanya hesabu kitimoto chaliwa kwa hesabu. Chaliwa kwa ndizi mbili na kachumbiri ya mia mbili. Kutulia kitini ni mtihani hadi iishe siniani. Kigogo hadi Igogo Mfenisini hadi Jamatini Yaitwa kitimoto juu ya uhotohoto wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom