Ni kwa nini IFM inatunuku shahada (Degree) wakati siyo Chuo Kikuu?

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Jamani nijuavyo mimi ni kwamba Shahada (Digrii) zinatunukuwa na Vyuo Vikuu pamoja na Vyuo Vishiriki vilivyo chini ya Vyuo Vikuu husika lakini nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini 'Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (Institute of Financial Management - IFM) imepewa mamlaka ya kutunuku Shahada za Uhasibu, Taxation, IT etc kwa wahitimu wake wakati siyo Chuo Kikuu?
 
Afadhali na potelea mbali ni mtu na ndugu yake. Kama unahoji umahiri wa vyuo, nenda pale UCC halafu ujiulize tunataraji wahitimu wa namna gani ktk IT ikiwa wakufunzi ndio wale.

Tukaage tukijivuna tu kuwa graduates lkn kama hamtasoma vitabu...degree ni makaratasi ambayo hata wewe unaweza tu ukjiandikia la kwako. Elimu yetu ni almost 0 na ndio maana kila siku hapa mnanung'unika oooh tiGO wanatuibia, mara ooh ITV mnaboa. Graduates are not competent! (kazi kujadili mishahara)
 
Jamani nijuavyo mimi ni kwamba Shahada (Digrii) zinatunukuwa na Vyuo Vikuu pamoja na Vyuo Vishiriki vilivyo chini ya Vyuo Vikuu husika lakini nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini 'Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (Institute of Financial Management - IFM) imepewa mamlaka ya kutunuku Shahada za Uhasibu, Taxation, IT etc kwa wahitimu wake wakati siyo Chuo Kikuu?

IFM has all the rights to offer degrees under act number 9 of 1997. Read here NACTE Overview

The National Council for Technical Education (NACTE) is a body corporate established by the National Council for Technical Education Act, 1997. The Act provides a legal framework for the Council to establish an efficient National Qualifications System that will ensure that products from technical institutions are of high quality and respond to changing needs as well as technological innovations in the … [Read More...]
 
Sasa ni kwa nini iendelee kutambulika kama Taasisi (Institute) badala ya Chuo Kikuu?

Hata huko UK kuna chuo kama kile alichosoma Salif Al Islam mwana wa dikteta wa zamani wa Libya Muammar Gaddaffi, London School of Economics kinatoa degrees mpaka kiwango cha PhD. Au Massachussets Institute of Technology ya USA
 
Aisee! ufahamu wako unaishia kwenye maswali bila kutafauta ukweli, ulishajaribu kufuatilia sheria iliyoanzisha chuo hiki (IFM)! Hivi unajua chochote kuhusu vyuo vya elimu ya juu? Unajua lolote kuhusu NACTE na TCU?

IFM wanastahili kutoa shahada na zaidi ya shahada au chini yake, ni chuo kinachotambuliwa na NACTE baraza la taifa la vyuo vya ufundi (usichanganye na veta). Vipo vyuo vingi tu hapa nchini ambavyo si vyuo vikuu (kundi la taasisi za elimu ya juu) kutaja vichache ni Mwalimu Nyerere Memorial Academy, DIT, TIA na IAA
 
Kama suala hulijui ni vyema ukawa unauliza hili ni jukwaa la great thinkerz.Kwanza kama bado upo chuo nenda kwa mwl wako akupe darasa nini maana ya University,Institute,college and school pia akuelezee kiundani sifa za kila moja uweze kutofautisha. Moja ya taasisi bora duniani ni MIT -Massachusetts Istitute of Technogy ambapo ipo kwenye top 5 ya vyuo/taasisi bora duniani na Inatoa Degree,Masters ,PhD mpaka post doctoral...so suala la IFM kuwa taasisi halafu kutoa degree sio suala la kushangaa.Wewe utakuwa ndio wale wale wanaofikiri chuo kikuu ni UDSM pekee.
 
Kasome NACTE na TCU ujue vigezo vya chuo kuweza kutoa digrii. Utapata mengi sana huko.
 
Afadhali na potelea mbali ni mtu na ndugu yake. Kama unahoji umahiri wa vyuo, nenda pale UCC halafu ujiulize tunataraji wahitimu wa namna gani ktk IT ikiwa wakufunzi ndio wale.
...
Mkuu, UCC sio chuo, ni centre tu ya kutoa some professional programmes. Highest award wanayotoa ni Diploma (ordinary).
 
Alikuwa hajui, tafsiri finyu ya neno Taasisi ndo iliyomponza! mwelewesheni na si kumshambulia, Tulipokuwa shule tuliamini Chuo Kikuu ni UDSM peke yake, tukadanganywa na jamii na tukadanganyika kweli! kwahiyo tukaaminishwa Taasisi ni kama Ngo tu so haziwezi toa Degree
 
Chuo kikuu cha Dodoma kilipomtunuku PHD Jakaya Kikwete nilishtuka na kutoa mchango wangu kuwa chuo hicho hakijafikiwa kiwango cha kutunuku PHD kwa vile hakina fakati ya PHD, lakini wenye hamasa za kiitikadi walinijia juu. Mengi yanayofanyika hapa Tanzania kwa sasa ni kiinimacho, ni sawa na chombo kubaki kinaelea baharini bila mwongozaji huku kikipigwa na mawimbi na kukosa mwelekeo, ndio maana mapapa na nyangumi wanaendelea kupiga mbizi ili mawimbi yaizamishe ili wafaidi yaliyomo.
 
Sasa ni kwa nini iendelee kutambulika kama Taasisi (Institute) badala ya Chuo Kikuu?

Alah! sasa kumbe wewe unataka tu kiitwe university? kutakuwa na maana gani kama kitaitwa university kama kitatoa watu ambao si competent? wanachoangalia kwenye utoaji wa elimu ni mtu kutoka akiwa competent na si uzito wa jina la chuo. Chuo kinaweza kuwa na jina kubwa lakini watu wanaomaliza kwenye chuo husika wakawa hawalingani na jina la chuo husika
 
Mungu akijalia mwakani naweza jiunga na chuo kikuu kama sio taasisi, naomba nieleweshwe tofauti iliyopo kati ya institute, university, school na college.
Wasalaam!
 
Mungu akijalia mwakani naweza jiunga na chuo kikuu kama sio taasisi, naomba nieleweshwe tofauti iliyopo kati ya institute, university, school na college.
Wasalaam!
Hatuwezi kukubali kuzalisha wasomi fake kama wewe, kama unajiandaa kujiunga na elimu ya juu na hata hujui kusoma dictionary nadhani una zaidi ya tatizo.
 
Nadhani wewe ulisoma au unasoma ud. Pia tangu utoke kijijini hujarudi kwa kuona utashusha P yako. Vile vile kama umemaliza una gentlemaman grade na kizingizio ulichonacho ud elimu tight.

ushauri, achana na mambo ya majina badala yake tumia elimu uliyonayo kujiletea maendeleo ya kwako na ya taifa lako. Usijifeel unaonewa kwa sababu boss wako kasoma THE INSITITUTE OF FINANCE wakati wewe umesoma ud
Jamani nijuavyo mimi ni kwamba Shahada (Digrii) zinatunukuwa na Vyuo Vikuu pamoja na Vyuo Vishiriki vilivyo chini ya Vyuo Vikuu husika lakini nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini 'Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (Institute of Financial Management - IFM) imepewa mamlaka ya kutunuku Shahada za Uhasibu, Taxation, IT etc kwa wahitimu wake wakati siyo Chuo Kikuu?
 
ninachoelewa ni kwamba institute ni center ambayo imebobea to a specific field, to me institute is better than university c'se they have all kinds of expertise in a particular field.
hint: look at TIA relationship with ministry of finance compared to ud, mz, tumaini etc, DIT and bodi ya wahandisi [engineers] compared to ud,etc dar maritime institute ..
 
Back
Top Bottom