ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,252
- 8,341
Habari zenu wana JF, Kwanza namshukuru Mungu kwa siku hii ya leo, ni siku njema inayopendeza machoni pa Mungu. Namshukuru mama yangu mpendwa kwa sababu katika siku hii ya leo tarehe 28 September miaka kadhaa iliyopita alimleta duniani huyu anaeandika ujumbe huu, Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani huko aliko.
Wana JF leo ninafuraha sana kwani leo ni siku muhimu sana kwangu, kikubwa ninamshukuru Mungu hata kwa umri huu niliofikia leo,wengi walitamani wafikie umri huu lakini hawakuweza, mimi sijampa Mungu hata senti 5 lakini nipo hai hadi leo hii ninapokumbuka siku yangu ya kuzaliwa kweli achene Mungu aitwe Mungu, namshukuru Mungu kwa Baraka kubwa na ndogo ndoga anazoendelea kunijalia katika maisha yangu, naomba aendelee kunijalia kwa kila inapoitwa leo maana najua kila kitu anachonipa maishani ni kwa NEEMA tu.
Wanajamii leo ni siku yangu ya kuzaliwa naomba mfurahi pamoja nami.