Ni kwa namna ipi polisi wanaweza kupata maelezo ya mtuhumiwa bila kumtisha au kumtesa?

Sio lazima kupata maelezo ya mtuhumiwa.

Mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya kwani chochote atakacho sema kinaweza kutumika kama ushahidi dhidi yake mahakamani.

Kama Jamuhuri inaamini umefanya kosa basi ni kazi yao kutafuta ushahidi lakini sio wajibu wa mtuhumiwa kuwapa huo ushahidi.

Mtuhumiwa ana wajibu wa kuijibu mahakama tu! Mengine ni hiyari yake.
 
Msingi wa kesi za jinai ni maelezo yanayochukuliwa na polisi kutoka kwa watuhumiwa.

Katika uchukuaji wa maelezo kutoka kwa watuhumiwa polisi wanatakiwa wasionekane wametumia vitisho wala nguvu.

Ikithibitika kuwa polisi wametumia vitisho au nguvu kupata maelezo kutoka kwa mtuhumiwa, maelezo hayo yanakataliwa kupokelewa kama ushahidi mahakamani.

Hii inaonyesha polisi wanafanya kazi yao huku wamefungwa mikono.

Je ipi ni namna bora ya wao kutenda kazi yao ya kuhakikisha wakosaji wote anafikishwa mbele ya sheria na kupata hukumu ya haki?

Unamtesa mtuhumiwa ili akupe maelezo unayotaka kwa ajili ya kumbambikia kesi. Huko ni kutafuta ushahidi au ni uhuni?
 
Najaribu KUTAFAKARI mfano jambazi anaye miliki SILAHA ya kivita akikamatwa na kufikishwa Kituo chapolisi saa nne asubuhi watoa taarifa wakapiga Simu saa Tano asubuhi wakiwaeleza Polisi kwamba jambazi huyo ana SILAHA na anapohojiwa anakataa kwamba Hana SILAHA yoyote baada ya kuvunja SHERIA na kumtesa anaamua kuwapeleka Askari alikoificha SILAHA hiyo saa nane mchana anaitoa alipo ificha baada ya kupigwa anakiri kwamba aliua na alimzika marehemu sehemu nyingine hatimaye saa kumi anaonesha shimo alimomficha marehemu.

Kesho yake anakubali kuwataja anaoshirikiana nao msako unatumia siku tatu.

Je,hayo masaa manne,24 na kuteswa kwake kunaweza kumponya na kesi yake kwakuwa aliteswa na kufikishwa mahakamani zaidi ya masaa 24?
 
Kutesa ni njia ya unyama haifai, lakini kwa mtu Sugu nunda bila njia hio atoi ushahidi.
 
Na ndugu Mungu amrehemu alikuwa bubu kuna siku alipotea akakamatwa usiku,nasi tukihangaika kumtafuta vituo vyote vya police tukampata asubui kituo kimoja akiwa ameteswa Sana ikiwemo kuchomwa Sana sigara wao wakiamini anajifanya bubu lazima ataongea, tulipofika kituoni tukampata tukawaelezea matatizo yake wakaishia tu kutupa pole.
Angalia unamtesa mtu bila kuwa na uhakika wa afya yake.
 
Jaribu kutafakari mfano MTUHUMIWA anayedhaniwa jambazi anakamatwa anateswa na mwisho wa siku inagundulika hana hatia. Anafadiwaje huyo mtu?

Wewe ni mtu mmoja?!
 
Jaribu kutafakari mfano MTUHUMIWA anayedhaniwa jambazi anakamatwa anateswa na mwisho wa siku inagundulika hana hatia. Anafadiwaje huyo mtu?
Hapo sasa ndiyo nitaungana na wadau wanaosema kunahitajika ubobevu Katika tasnia ya upelelezi ili mtuhumiwa anapoingizwa kikangaoni wawe na fact asilimia 99.

Vinginevyo watu wanao amua kuwa wahalifu siyo wapole kama unavyofikiri.Mtu anaye amua kuua ili apate Mali na ukatili mwingine umuhoji kwa kumuomba sidhani kama anaweza kukupa ushirikiano ingawa ni mbaya sana kumtesa mtuhumiwa kwa hila au ili atoe rushwa au kwasababu yoyote Ile ili kumfurahisha mtu mwingine.
 
Kwani nchi wanazokataza kabisa utesaji wanafanyaje?

Kikubwa ni kuwa na uchunguzi wa kisasa; forensic science ndio njia pekee ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
 
Nakuelewa ila maelezo zaidi yanatakiwa. Mfano mtu katuhumiwa kuiba pesa akiwa mtumishi - DNA inasaaidia vipi hapo?
Sawa mkuu DNA imeweza kusaidia ila its not limited kwa kosa ulilolitolea mfano,kitu muhimu its to link suspect na crime scene,mtu kaiba pesa akiwa mtumishi wa umma ,kesi hii ni kufuatilia hio pesa iliibiwa vipi?nani walihusika,imepelekwa wapi,ikiwa ni pamoja na kuomba kibali cha mahakama ili kupata recording zote za mawasiliano. Maelezo mengine yatafuata ila unaweza angalia pia dstv kuhusu program zao ndani ya ID.
 
Kwani nchi wanazokataza kabisa utesaji wanafanyaje?

Kikubwa ni kuwa na uchunguzi wa kisasa; forensic science ndio njia pekee ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
Yes forensic investigations ni key!nchi yetu bado sana kwenye hili
 
Kwani nchi wanazokataza kabisa utesaji wanafanyaje?

Kikubwa ni kuwa na uchunguzi wa kisasa; forensic science ndio njia pekee ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo mbalimbali.
Nchi gani inakataza utesaji? Utesaji umewekwa kwenye SHERIA za nchi nyingi sana hata kwenye SHERIA yetu ya ushahidi sura ya 6 inaeleza kwamba ushahidi wa kuteswa hauwezi kupokelewa mahakamani isipokuwa kama kuteswa huko kutasababisha upatikanaji wa kitu kiswahili chake sina hakika.(lead to Discovery).

USA ndiyo mbaya zaidi nadhani unajua pamoja na kwamba wao ni machampion wa haki za binadamu.
 
Na ndugu Mungu amrehemu alikuwa bubu kuna siku alipotea akakamatwa usiku,nasi tukihangaika kumtafuta vituo vyote vya police tukampata asubui kituo kimoja akiwa ameteswa Sana ikiwemo kuchomwa Sana sigara wao wakiamini anajifanya bubu lazima ataongea, tulipofika kituoni tukampata tukawaelezea matatizo yake wakaishia tu kutupa pole.
Angalia unamtesa mtu bila kuwa na uhakika wa afya yake.
Mkuu ububu ni ulemavu SIYO tatizo la kiafya
 
Tusaidie hayo wanayofundishwa na kama yanaufanisi kwa nini wanatumia njia hii isiyopendeza?
Kwa sababu polisi wengi ni form four waliofeli.
Jeshi la polisi la Tanzania ni la kikoloni
Wanafanya ili kuiridhisha ccm so kama cyo mwana ccm unakuwa mhalifu hata kabla hujapelekwa mahakamani.
Badala ya kupendekeza kuajir watu wa kada tofauti kama psychologist nk. Yule waziri wa form four anasema polisi hawataki watu wenye degree
 
Wakiajiri wataalamu wataweza kuwalipa?
Pili Kazi ya police ni kupokea amri na maagizo bila kuhoji,kwa wasomi ni vigumu kupokea amri bila kuhoji,hivyo Kazi haitofanyika.
 
Issue ya kunalipa haipo Tanzania. Kwani mtu uliyesoma ualimu hadi ngazi ya degree analipwaje?
Issue ya kupokea order ipo popote pale kazini. Chain of command ili mradi ziwe halali na zenye weledi
 
Msingi wa kesi za jinai ni maelezo yanayochukuliwa na polisi kutoka kwa watuhumiwa.

Katika uchukuaji wa maelezo kutoka kwa watuhumiwa polisi wanatakiwa wasionekane wametumia vitisho wala nguvu.

Ikithibitika kuwa polisi wametumia vitisho au nguvu kupata maelezo kutoka kwa mtuhumiwa, maelezo hayo yanakataliwa kupokelewa kama ushahidi mahakamani.

Hii inaonyesha polisi wanafanya kazi yao huku wamefungwa mikono.

Je, ipi ni namna bora ya wao kutenda kazi yao ya kuhakikisha wakosaji wote anafikishwa mbele ya sheria na kupata hukumu ya haki?

Wanafundishwa huko chuon, ndo maana wanaitwa Police; Kama kupiga ni uchunguzi basi Hakuna haja ya Kwenda chooni
 
Back
Top Bottom