Ni kwa namna ipi polisi wanaweza kupata maelezo ya mtuhumiwa bila kumtisha au kumtesa?

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946
Msingi wa kesi za jinai ni maelezo yanayochukuliwa na polisi kutoka kwa watuhumiwa.

Katika uchukuaji wa maelezo kutoka kwa watuhumiwa polisi wanatakiwa wasionekane wametumia vitisho wala nguvu.

Ikithibitika kuwa polisi wametumia vitisho au nguvu kupata maelezo kutoka kwa mtuhumiwa, maelezo hayo yanakataliwa kupokelewa kama ushahidi mahakamani.

Hii inaonyesha polisi wanafanya kazi yao huku wamefungwa mikono.

Je, ipi ni namna bora ya wao kutenda kazi yao ya kuhakikisha wakosaji wote anafikishwa mbele ya sheria na kupata hukumu ya haki?
 
..sina uhakika, lakini nadhani kuna mtu anaitwa " MLINZI WA AMANI " ambaye kama mtuhumiwa amekiri anatakiwa asainishwe maelezo baada ya akishuhudiwa na mlinzi wa amani.

..kama kumbukumbu zangu ziko vizuri watuhumiwa wa kesi ya uhaini ya miaka ya 80 wale waliokiri walisainishwa maelezo wakishuhudiwa na mlinzi wa amani.

..Naomba kusahihishwa na Wanasheria kama nimekosea.

Cc Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa
 
Sheria zinawataka wachukue maelezo ya watuhumiwa ndani ya masaa manne tokea wamewakamata.

Na pia wanatakiwa wawapeleke mahakamani ktk muda usiozidi masaa 24. Wakizingatia haya watapunguza sintofahamu ya mtuhumiwa kusema aliteswa.

Na kama wanataka waaminiwe zaidi wawe wanawachukua video wakati wote wa kuwahoji.

Video hizi zianze kwa mtuhumiwa kueleza mwenyewe kwa hiari yake mazingira ya kukamatwa hadi muda huo anaohojiwa ili asije akasema nilihojiwa pembeni ya Camera.
 
Kwani polisi wa Ulaya wanapataje ushaidi?

Mkuu hii ni marekani​

The question of torture​

The issue of torture, and the US authorities' secrecy about its use, also continues to cast a long shadow over proceedings, with arguments about what evidence is admissible given what the defendants were subjected to at Guantanamo Bay and so-called 'Black sites' elsewhere.
 
..sina uhakika, lakini nadhani kuna mtu anaitwa " MLINZI WA AMANI " ambaye kama mtuhumiwa amekiri anatakiwa asainishwe maelezo baada ya akishuhudiwa na mlinzi wa amani.

..kama kumbukumbu zangu ziko vizuri watuhumiwa wa kesi ya uhaini ya miaka ya 80 wale waliokiri walisainishwa maelezo wakishuhudiwa na mlinzi wa amani.

..Naomba kusahihishwa na Wanasheria kama nimekosea.

Cc Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa
Uko sawa mkuu. Kuwa na amani
 
Very easy mkuu, polisi wetu wanahitaji kupata mafunzo ya kuwawezesha kumudu majukumu yao hasa detectives, wajue jinsi ya to secure and to approach crime scenes, wajue kuwa ni vema na sheria kumhoji suspect kwa facts sio vitisho, ni muhimu watumie science na technology mpya ili kujenga watertight case dhidi ya suspect, DNA ipo na waitumie kwenye kazi zao
 
Pamoja na muda sahihi wa kuchukuliwa maelezo umetajwa, maelezo yanatakiwa yachukuliwe mbele ya mtu mwingine asiyehusika na tuhuma hizo , kwa mfano mlizi wa amani, ndugu wa mtuhumiwa, wakili au mwanasheria wa mtuhumiwa. Kumnyima mtuhumiwa haki hiyo ni kukaribisha mashaka.
 
Very easy mkuu,polisi wetu wanahitaji kupata mafunzo ya kuwawezesha kumudu majukumu yao hasa detectives,wajue jinsi ya to secure and to approach crime scenes,wajue kuwa ni vema na sheria kumhoji suspect kwa facts sio vitisho,ni muhimu watumie science na technology mpya ili kujenga watertight case dhidi ya suspect,DNA ipo na waitumie kwenye kazi zao
Nakuelewa ila maelezo zaidi yanatakiwa. Mfano mtu katuhumiwa kuiba pesa akiwa mtumishi - DNA inasaaidia vipi hapo?
 
..kaka naomba ufafanuzi kuhusu huyo anayeitwa " mlinzi wa amani. "

..mara ya mwisho kumsikia ni wakati nafuatilia ile kesi ya uhaini zama zile.

..nimekuja kukumbuka wakati huu wa kesi ya Mbowe na wenzake watatu.

..asante.
Mkuu, mlinzi wa amani ni kiongozi wa kiserikali kwa ngazi ya kijiji, kitongoji, mtaa au kata. Huyu ni Mtendaji wa eneo husika, yaani, Mtendaji wa Kijiji, Mtendaji wa Mtaa, Mtendaji wa Kata na kadhalika. Kuwa mlinzi wa amani ni moja ya majukumu ya kisheria ya Mtendaji tajwa.
 
Hii ni common sense tu, ushahidi mwingi maelezo kidogo. mmeshindwa kupata ushahidi wa maana mnajifichia kwenye maelezo ambayo mmeyapata kwa vitisho.vipi kesho nikiandika Sirro gaidi mtachukua hayo maelezo? au mtataka ushahidi?
 
Msingi wa kesi za jinai ni maelezo yanayochukuliwa na polisi kutoka kwa watuhumiwa.

Katika uchukuaji wa maelezo kutoka kwa watuhumiwa polisi wanatakiwa wasionekane wametumia vitisho wala nguvu...
Siku ndugu yako akikamatwa kawaambie Polisi hamfungwi mikono pigeni mpaka aseme. Ushabiki mwingine wa kihuni mnaleta. Nani kakwambia Polisi chuoni wanafundishwa kutesa watu?

Huo utesaji wanafundishwa na kina Msangi na Kingai vituoni ndo maana Aina Yao ya mateso utaaikia ni kuning'iniza watu kama popo na kubinya pumbu.
 
Hii ni common sense tu,ushahidi mwingi maelezo kidogo. mmeshindwa kupata ushahidi wa maana mnajifichia kwenye maelezo ambayo mmeyapata kwa vitisho.vipi kesho nikiandika Sirro gaidi mtachukua hayo maelezo? au mtataka ushahidi?
Huu ni mchango wa kwanza wa mipasho. Uwe unaona aibu kidogo basi hata kama unatumia jina bandia. Hapa uache mipasho.
 
Wakajifunze Ulaya
Msingi wa kesi za jinai ni maelezo yanayochukuliwa na polisi kutoka kwa watuhumiwa.

Katika uchukuaji wa maelezo kutoka kwa watuhumiwa polisi wanatakiwa wasionekane wametumia vitisho wala nguvu...
 
Back
Top Bottom