Ni kwa namna ipi kashfa ya BOT inaweza kuathri benki nyingine?

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
103
heshima yenu wana JF.
ni maoni yangu kuwa JF ina watu wenye vipaji na proffessions mbalimbali. mimi siko kwenye uchumi kielimu. ila baada ya kupata maoni namna ambavyo BOT imechafuka, tukianza na kashfa ya Balali, ikaja ya kuajiri vihiyo na watoto wa wakubwa wenye Hisa benki za biashara, na hii kashfa ya karibuni ya ela za BOT kutumika wakati wa uchaguzi kiolela, nimekuwa na dukuduku la kutaka kujua kutoka kwenu.

ninaelewa kuwa BOT ni chombo pekee cha kudhibiti na kurekebisha banki zote zikiwemo za biashara.

pia ninaelewa kuwa BOT ndiyo inayoshauri serikali lipi la kufanya ili yawepo mazingira safi kwa ajiri ya benki zote kwa usawa, na kuvuta benki mpya.

pia ni chombo kinachoweza kufuta kuadhibu na /kusimamisha benki yoyote itakayokiuka maadili ya benki, ikiwemo kuajiri vihiyo n.k

ndugu wanauchumi je kashfa hizi haziwezi kusababisha itilafi katika maswala ya benki za biashara hapa tanzania?

nitashukuru hata mtu akija na data au source, si unajua sisi sio uwanja zake
 
ndugu wanauchumi je kashfa hizi haziwezi kusababisha itilafi katika maswala ya benki za biashara hapa tanzania?

nitashukuru hata mtu akija na data au source, si unajua sisi sio uwanja zake

Mimi nitajaribu kukujibu, ila jibu langu litakuwa la nadharia kwa mantiki kwamba sitakupa data halisi za jinsi gani benki zetu zinaweza kuathirika. Lakini nazani kwamba jibu langu litakupa angalau mwanga wa kujuwa madhara ya rushwa BOT kwa benki za bihashara.

Athari za rushwa BoT ni sawa na athari atakazopata mteja wa benki yeyote ya bihashara; NBC kwa mfano, endapo NBC itakumbwa na rushwa. Hii ni kwasababu BoT ni benki ya mabenki yetu ya bihashara na taasisi nyingine za fedha Tz. Hivyo chukulia NBC kama mteja wa BoT.

Sasa serikali kwa kushirikiana na BoT ndivyo vinavyotoa mwongozo juu ya nyenendo za benki za bihashara. Kwa mfano kutoa kiwango cha fedha ambacho benki za bihashara zinatakiwa ziwenazo kwa masaa 24. Vile vile serikali kwa kushirikiana na BoT ndizo zinazotoa bima kwa mabenki ya bihashara ili kuhakikisha kwamba mteja (mtu wa kawaida) wa benki za bihashara hapati hasara pale benki yake inapofirisika.

Rushwa inapoikumba BoT inaangamiza uchumi kwa namna kuu tatu.(i)mwongozo wa nyenendo za benki za bihashara unalegalega na hivyo kufanya benki za bihashara kuwa huru (fungulia mbwa)na matokeo yake mfumuko wa bei unatokea au fedha zinatoweka katika mzunguko, mana kazi ya BoT ya kuchota fedha wakati wa maji-kujaa kwenye benki za bihashara na ile ya kujaza maji wakati wa maji-kupwa inakosa mwelekeo. Rushwa hii ikikomaa utakuta benki za bihashara zenye connections/mianya ya rushwa za BoT zinaruhusiwa kuwa na kiwango kikikubwa cha fedha katika masaa 24, wakati benki zisizo na mianya zinasakamwa na hivyo kujikuta zikifirisika kwa ushindani husio fair. Uchumi wa nchi hapo ndio victim.

(ii)Rushwa BoT inapunguza uaminifu wake kwa mabenki za bihashara na hivyo kusababisha benki za bihashara kutafuta mbinu zakujihami kama capital flights (kutorosha fedha). Mfano wewe ukigundua kwamba benki yako haina uaminifu, lazima utatafuta mbinu za kusweka ela zako mchagoni. Kadhalika, benki zinapokosa uhaminifu na BoT zitaanza kujilimbikizia kiasi kikubwa zaidi ya kile kilichotolewa na BoT, zikiangalia namna ya kupeleka fedha sehemu salama. Hapa benki za bihashara zitapunguza wigo wa kazi zake, na uchumi wa nchi ndo unadidimia.

(iii)Wizi/rushwa BoT manake ni kwamba assets za BoT zinaliwa, kwa hiyo kila serikali inapohitaji fedha za ku-finance shughuli zake za masaa 24, lazima ziuze bonds kwa mabenki ya bihashara au zichapishe fedha. Kadhalika BoT inapotaka ku-finance shughuli zake za kila siku, mfano ujenzi wa ofisi mpya unaogharimu mabilioni ya shilingi zitalazimika ku-issue bonds; mabenki yanapokosa imani na BoT kwa ajili ya rushwa zitapunguza manunuzi ya bonds na hivyo kujikuta zikipungukiwa na assets, huku njia pekee kwa BoT ikiwa ni kuchapisha ela. Shughuli za benki za bihashara zitasinyaa sambamba na zile za uchumi wa nchi na mfumuko wa bei utakuwa unatoboa mawingu.
 
Back
Top Bottom