Ni kwa namna gani bidhaa au huduma zako ziwe na ubora ?

Jul 3, 2016
19
13
Habari zenu wapendwa,
Ni matumaini yetu kuwa nyote mu wazima, leo tungelipenda ku-share nanyi juu ya dhana ya ubora wa bidhaa/huduma na jinsi gani kuhakikisha huo ubora

Biashara nyingi zinafilisika na kusitisha huduma kutokana na kushindwa kumhakikishia mteja (customer) ubora anaoutarajia.
Katika mpango wa biashara (business plan), benki na wadhamini huweka mazingatio makubwa katika kipengele hiki, hii ni kwa sababu uhai wa biashara yoyote kwa kiasi kikubwa unategemea ubora wa huduma au bidhaa.

Ubora katika bidhaa au huduma imekuwa ni miongoni mwa mbinu na mikakati katika kukabiliana na ushindani wa kibiashara.

Mteja mara nyingi huangalia ubora wa bidhaa au huduma katika mitazamo ya aina mbili, ambayo ni:

  1. Hali ya ushikiki (tangibility), hapa mteja huzingatia vitu vifuatavyo :
-Uhakika wa bidhaa kwa muda wa kipindi fulani (reliability)
-Uzuri wa bidhaa katika hali ya hisia (aesthetics)
-Kiasi gani bidhaa inaruhusu ku-repair na servicing kiujumla.
-Usalama kwa mtumiaji (safety and security)
-Urefu wa muda wa matumizi (durability)

2. Hali isiyo ya ushikiki (intangibilty), hapa mteja huzingatia vitu vifuatavyo:

-Ufanisi wa watoa huduma (competence)
-Upole, unyenyekevu na muonekano wa watoa huduma (courtsey and neat appearance)
-Kuaminika kwa watoa huduma (trustworthiness)
-Namna ya kuwasiliana na wateja (communicaations)
-Usalama wa eneo la kutolea huduma (security)

Kuna njia nyingi tu ambazo mfanyabiashara huweza kuzitumia ili kuhakikisha bidhaa au huduma zake zinakidhi viwango vya ubora (Kutokana na mtazamo wa mteja). Miongoni mwa njia hizo ni:

  1. Kuhakikisha anafanya vifungashio (packaging) kwa bidhaa zake.
  2. Mfanyabiashara kuchagua eneo moja au zaidi ya moja(focusing) katika mitazamo tuliyoiona hapo juu, mfano kuhakikisha upole na unyeyekevu wakati wa kutoa huduma n.k. Mfano The Ritz-Carlton Hotel ni miongoni mwa hoteli ambazo zimejijengea jina kubwa kutokana na kujikita katika kuhakikisha ufanisi wa watoa huduma wake, upole na unyenyekevu wa watoa huduma n.k
  3. Kuhakikisha matumizi ya teknolojia mfano teknoloja ya mawasiliano n.k. Hii itamsaidia mfanyabiashara kuepuka makosa ya kibinadamu ambayo hupelekea kuathiri ubora wa bidhaa hata huduma pia. Mfano matumizi ya programu maalum za komputa katika uthibiti na usimamizi wa masuala ya fedha, rasilimali watu n.k
  4. Matumizi ya malighafi (raw materials) yenye ubora wa hali ya juu katika utengenezaji wa bidhaa au utoaji wa huduma.
Pamoja na hayo tuliyoyaona hapo juu katika kuhakikisha ubora wa bidhaa au huduma, pia mfanyabiashara ana wajibu wa kuhakikisha sera zinazoongoza biashara yake zinazingatia njia nzuri na sahihi katika kuajiri na kutoa mafunzo kwa watendaji/wasaidizi wake pia kuwepo na utaratibu wa kuwapa motisha (motivation) wafanyakazi, hii itawapelekea kutimiza majukumu yao kwa bidiii na hatimaye kuja na huduma bora.

Ni matumaini yetu tulichokusudia kukifikisha kimeeleweka.

Kwa huduma zifuatazo:
-Utoaji wa ushauri wa kitaalamu katika Business Development &Management, Project Planning
and Management , Operations Management and Tax Management.
-Utoaji wa semina katika maeneo tutoleayo ushauri wa kitaalamu.
-Uandaaji wa mipango ya biashara (Business plans)
-Uandaaji wa michanganuo ya miradi (Project proposals)


Usisite kututafuta kwa namba 0719 518367, 0657 935110, 0783 695639
E-mail: platinumconsultancy74@gmail.com

Ahsanteni na karibuni sana.
 
Habari
nimependezwa na content yenu hongera sana, mm ni mjasiliamali nahitaji mniandalie project proposal inakuwa na vitu gani hasa? na dar maeneo gani?
akhasnteni
 
Habari
nimependezwa na content yenu hongera sana, mm ni mjasiliamali nahitaji mniandalie project proposal inakuwa na vitu gani hasa? na dar maeneo gani?
akhasnteni

Habari njema mdau, pia tunashukuru kwa pongezi zako kwetu.

Unamaanisha "Project Proposal" ya mradi usio wa kibiashara/kifaida au "Business Proposal" kwa ajili ya mradi wa kibiashara?

Kama ni kwa ajili ya mradi usio wa kibiashara, contents hutegemea na matakwa ya mfadhili wako (Kwa maana atahitaji vitu gani viwepo ndani ya proposal, mfano kuna mwingine kabla ya kumpelekea proposal atahitaji kwanza "Concept Paper")

Na ikiwa ni proposal kwa ajili ya mradi wa kibiashara, hapa itategemea, ikiwa ni kwa ajili ya kuanzia biashara kabisa na kuomba fedha kwa mfadhili, vitu vya msingi kabisa hujumuisha: uchambuzi wa mazingira ya biashara (Business environment analysis), uchambuzi katika ushindani (competitive analysis), uchambuzi wa soko (Market analysis), mpango fedha (Financial plan) na mengineyo.

Ikiwa ni kwa ajili ya kuombea fedha benki kwa biashara iliyokwisha anza tayari, contents zake huwa ni fupi sana, na mara nyingi hutegemea na miongozo ya maswali au vitu vinavyoulizwa na taasisi husika (Bank) katika fomu wanayokupatia.

Pia kuhusu upatikanaji wetu, tunapatikana katika Manispaa ya Kinondoni, mtaa wa Ada Estate, jirani na makao makuu ya Bakwata.

Karibu sana
 
Back
Top Bottom