Ni kwa manufaa yetu sote Wizara, Mashirika ya Umma, bodi na Idara za Serikali kuongozwa na watu wenye weledi husika

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
14,332
2,000
Kama tunataka nchi yetu iendeshwe kitaalamu, kwa weledi na muelekeo sahihi unaoleweka mawaziri wa wizara, wakurugenzi wa wizara, wakuu wa idara lazima wawe watu wa taaluma husika na uzoefu husika kulingana na wizara,shirika na idara husika.

Wizara ya habari, iendeshwe na mtu mwenye uzoefu wa tasnia ya habari, wizara ya uchumi na mchumi, wizara ya nishati na mtu mwenye uzoefu wa nishati, wizara ya ulinzi na mzoefu wa mambo ya usalama n.k.

Kumfanya mwanesheria waziri wa Afya, mtaalamu wa Kiswahili mkurgenzi wa kituo cha uwekezaji n.k ni kuleta mchanganyiko usio sahihi wa rasilimali watu, haina mantiki katika maendeleo, inashusha morali ya watumishi wa chini na inafifisha ufanisi.

Watu wenye weledi husika wanapasawa kuongoza sehemu husika.
 

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,441
2,000
Labda CCM iwe imekufa, vinginevyo tegemea kila siku kurudi nyuma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom