Ni kuwa Hawa Letshego (Faidika) wako juu ya sheria ama?

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,723
5,899
Hii taasisi ya kukopesha watumishi wa Uma Faidika au Letshego inakiuka kanuni na taratibu za utoaji mikopo mathalani kupandisha riba bila taarifa mpaka kupitiliza na hii wameanza mwezi wa 9...

Lakini kama haitoshi pindi unapotaka kufuta mkopo inakulazimu mpaka kuanza kutishiana maisha maana sio kwa usumbufu huo utakaopata...

Nauliza je hii taasisi yenyewe inajitungia Sheria zake ama Kuna mkubwa anayeilinda ifanye hivi?
 
Mkuu kwani mkataba wako wa mkopo unasemaje? Kama kuna kitu wamefanya nje ya taratibu fauatilia utapata haki yako.
 
Watumishi wa umma huwa mnakimbilia kukopa bila hata kujua vigezo na masharti. Mikataba mingi ya mikopo imeandikwa kuwa riba inaweza kuongezwa wakati wowote bila taarifa.

Pili mkopo ni mkataba say wa miaka mitatu, unapoenda kufuta mkopo ina maana unavunja mkataba. Hivyo basi ni lazima utaratibu sahihi ufuatwe.

Acheni kukopa kopa hovyo!
 
Hii taasisi ya kukopesha watumishi wa Uma Faidika au Letshego inakiuka kanuni na taratibu za utoaji mikopo mathalani kupandisha riba bila taarifa mpaka kupitiliza na hii wameanza mwezi wa 9...
Lakini kama haitoshi pindi unapotaka kufuta mkopo inakulazimu mpaka kuanza kutishiana maisha maana sio kwa usumbufu huo utakaopata...
Nauliza je hii taasisi yenyewe inajitungia Sheria zake ama Kuna mkubwa anayeilinda ifanye hivi?
Ni wakati sasa wakopaji mkalilia kupata elimu ya mikopo ili mkaepuka malalamiko yasiyo na tija. Naiman haya malalamiko huja baada ya kukopa na kuishiwa kwa hiyo hela. Hapo ndipo sasa malalamiko huanza. Nimeifatilia hii taasis kwa karibu na kugundua kuwa wakopaji ndio wanashida.

Kwakuwa wanafika kwenye hizo tasisi nakufanya taratibu za mikopo bila kujua kwa kina.

Baada ya kusoma hii post ilinilazm kufika kwenye hayo matawi na kujifunza. Nilipofika nilitaka kulinganisha uwiano wa riba na bank nyingine. Nikauliza riba ya mwaka mmoja kwa milion moja.

Nikapewa chati nikaangalia makato ni 106,600. Hiivyo mpaka namaliza mkopo ningeludisha 1,279,200. Hivyo riba ni 279, 200. Nikaringanisha na bank zngine ambazo wao wanazema 17% kwa mwaka maana yake mpaka unmaliza mkopo unatakiwa kulipa 1,170,0000.

Sasa ukiwa mvivu wa kufikilisha kichwa lazma useme faidika riba zao ziko juu lakini kiuharisia nilichogundua faida riba zao kwa hapa sio kubw kuwazid hawa wenye %17 kwakuwa faidika unapewa milion cash na huku kwingine huwa wanakuwa na makato kwenye hela waliyo kukopesha hivyo unatakiwa uchukue hiyo hela uliyokatwa ujumlishe na hiyo riba 17% utaona hela wanayobakiwa nayo hizo mnazoita banki ni zaid ya hiyo ya faidika.

Niwambie wakopaji hamna mkopo nafuu kama mfatiliaji ili mkopo nafuu umekopa unaenda kufanyia nn?
 
Ni wakati sasa wakopaji mkalilia kupata elimu ya mikopo ili mkaepuka malalamiko yasiyo na tija. Naiman haya malalamiko huja baada ya kukopa na kuishiwa kwa hiyo hela. Hapo ndipo sasa malalamiko huanza. Nimeifatilia hii taasis kwa karibu na kugundua kuwa wakopaji ndio wanashida. Kwakuwa wanafika kwenye hizo tasisi nakufanya taratibu za mikopo bila kujua kwa kina.
Baada ya kusoma hii post ilinilazm kufika kwenye hayo matawi na kujifunza. Nilipofika nilitaka kulinganisha uwiano wa riba na bank nyingine. Nikauliza riba ya mwaka mmoja kwa milion moja. Nikapewa chati nikaangalia makato ni 106,600. Hiivyo mpaka namaliza mkopo ningeludisha 1,279,200. Hivyo riba ni 279, 200. Nikaringanisha na bank zngine ambazo wao wanazema 17% kwa mwaka maana yake mpaka unmaliza mkopo unatakiwa kulipa 1,170,0000. Sasa ukiwa mvivu wa kufikilisha kichwa lazma useme faidika riba zao ziko juu lakini kiuharisia nilichogundua faida riba zao kwa hapa sio kubw kuwazid hawa wenye %17 kwakuwa faidika unapewa milion cash na huku kwingine huwa wanakuwa na makato kwenye hela waliyo kukopesha hivyo unatakiwa uchukue hiyo hela uliyokatwa ujumlishe na hiyo riba 17% utaona hela wanayobakiwa nayo hizo mnazoita banki ni zaid ya hiyo ya faidika. Niwambie wakopaji hamna mkopo nafuu kama mfatiliaji ili mkopo nafuu umekopa unaenda kufanyia nn?

Huna ulijualo asee naomba nikwambie ivyo sio kukuzihaki au kukukejeli hapana ila ukweli ndio huo

Nimefanya kazi kwenye izi taasisi za mikopo kama 3 na wao waulize kwanini huwa wanaficha jumla ya mkopo unaorudisha nimefanya kazi Tunakopesha limited, Maboto enterprises, Bayport, Fanikiwa microfinance so nazijua vizuri apo kuna taasisi wana riba za 36% , 48%,50% na kuna taasisi moja nlienda fanya interview kwao wana toza asilimia 10 per month means wana 120% kwa mwaka

Kuna taasisi apo mpk nlikua naona dhambi kuingiza makato yani mtu anakopa milion 5 anakuja lipa milion 18-19.

Hauwezi linganisha taasisi yenye riba ya 17% kwa mwaka na taasisi yenye 48% kwa mwaka ndio maana ukienda kopa Milion 4 uko faidika wanakupa muda mrefu kwa kato la ajabu sasa nenda bank kakope 4M uone utarudisha kwa muda gani na pesa watakayo kata kama sio ndogo.

Pata changamoto utake kufuta mkopo kwenye izo taasisi au waambie unataka kuuza mkopo kwenda taasisi nyingine utazungushwa balaa na hautakuja pewa kamwe maana wanajua kupata mteja ni kazi sana kwao
 
Karibia taasisi nyingi zinazokopesha zinasumbua sana wateja ukitaka kuclear mkopo, Kuna mtu namfaham wanamzungusha toka mwaka Jana mwezi wa kumi.

Nahisi hizi taasisi nyingi zinakuwa na vigogo ndio maana pamoja na malalamiko mengi ya waajiriwa lakini mkono mrefu wa serekali yetu pendwa inashindwa kuzichukulia hatua
 
Watumishi wa umma huwa mnakimbilia kukopa bila hata kujua vigezo na masharti. Mikataba mingi ya mikopo imeandikwa kuwa riba inaweza kuongezwa wakati wowote bila taarifa.

Pili mkopo ni mkataba say wa miaka mitatu, unapoenda kufuta mkopo ina maana unavunja mkataba. Hivyo basi ni lazima utaratibu sahihi ufuatwe.

Acheni kukopa kopa hovyo!
Watumishi wa Umma Tanzania ( Hususani Walimu ) wana akili ndogo sana.

Ni Wapumbavu.
 
Karibia taasisi nyingi zinazokopesha zinasumbua sana wateja ukitaka kuclear mkopo, Kuna mtu namfaham wanamzungusha toka mwaka Jana mwezi wa kumi. Nahisi hizi taasisi nyingi zinakuwa na vigogo ndio maana pamoja na malalamiko mengi ya waajiriwa lakini mkono mrefu wa serekali yetu pendwa inashindwa kuzichukulia hatua

Bank ni simple microfinance sahau wanajua wanapoteza mteja hawafuti watakuzungusha kweli wakikubali wanakupiga fine ya kusettle mkopo wako
 
Kwenye finance ukisikia vitu kama "mkopo ndani ya saa 1" ogopa sana.

Sheria ya pesa ni rahisi sana, risk kubwa riba kubwa.

Mabenki wanakuwa makini sana, maana wanapunguza risk na hivyo hivyo wanapunguza na interest; hawa wa mkopo chapchap risk ni kubwa, vigezo vichache lakini wanajua watakupiga sawa awa kwenye riba.
 
Hii bank mara ya kwanza kuiona kwenye mitandao, nilihisi aina fulani ya tatizo, jina. Jina linabeba nafasi kubwa kwa tabia ya mtu au kitu. Letshego (let she go)!?
 
Kucheleweshewa pesa kwa muda unaoweza kufikia mwezi mmoja na nusu

Kupandishiwa riba muda wowote

Kukatwa pesa baada ya kumaliza deni

Kusumbuliwa kwa mtu anayetaka kufuta deni
Pole kwa hayo
Lakini usiwalaumu sana sababu huo ni mkata na anayeuvunja anatakiwa kuwajibika. Wawajibishe
 
Pole kwa hayo
Lakini usiwalaumu sana sababu huo ni mkata na anayeuvunja anatakiwa kuwajibika. Wawajibishe
Bado sijakopa, nilikuwa nataka nikope ila Sasa nimeghairi kabisa kukopa kwasababu kila Uzi unaowahusu hao jamaa umejaa malalmiko ya kutosha.
Imagine Kuna watu wanasema walikopa million 4 wakarejesha million 15?
 
Kabla ya kukopa lazima uangalia mkataba unasemaje.
Ukishakopa ukaona vitu vinafanyika nje ya makubaliano tafuta haki yako
Kama kila kitu kiko kwenye mkataba huwezi lalamika maana ulikubaliana
 
Hii taasisi ya kukopesha watumishi wa Uma Faidika au Letshego inakiuka kanuni na taratibu za utoaji mikopo mathalani kupandisha riba bila taarifa mpaka kupitiliza na hii wameanza mwezi wa 9...

Lakini kama haitoshi pindi unapotaka kufuta mkopo inakulazimu mpaka kuanza kutishiana maisha maana sio kwa usumbufu huo utakaopata...

Nauliza je hii taasisi yenyewe inajitungia Sheria zake ama Kuna mkubwa anayeilinda ifanye hivi?
Ukiona taasisi iko hivo ujue haina future
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom