Ni kumbukumbu ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika, si sawa kutaja miaka kwani Tanganyika iliishi miaka 2 na miezi 4 tu baada ya uhuru!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,872
Binafsi naamini tunasherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambayo leo haipo bali tuna Tanzania.

Ukisema kwa mfano miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika unamaanisha nini? Tanzania ina miaka 57 na Tanganyika haipo.

Karibu kwa mjadala chanja.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote Majilio haya!
 
Tamaa ya kuvimeza Visiwa sisi ndio tumemezwa😆😆🤣😂

Ujanja mwingi mbele giza.
chrisfreshhah.png
Mgeni rasmi ni Samia Suluhu na Hussein Mwinyi wengine wote ni watazamaji kama sisi 😆😆😆
 
Zanzibar tuna wahudumia kwa kila kitu lakini wao hawana mchango wowote
1964 Zanzibar ilikuwa tajiri kuliko Tanganyika.

Nyerere alikuwa anatazama tv kutokea Zanzibar.

Wakati huo hakukuwa na Wachaga bali Wamachame, Wakibosho, Wauru, Wamarangu na nyie Warombo!
 
Zanzibar tuna wahudumia kwa kila kitu lakini wao hawana mchango wowote

Ni kweli mnatuhudimia kwa kutuwekea kambi Za majeshi kila mtaa Na kutuletea majeshi ya Burundi wakati wa uchaguzi. Mnatuuwa ili kuweka vibaraka wenu. Hongera kwa Huduma hizi Za uvamizi
 
Nimezaliwa 1980 nikaitwa John, lakini 1991 nikabadili dini na jina nikaitwa Ramadhan. Vipi mtasema nimezaliwa upya 1991 au ndio yule yule John wa 1980?
 
Kwanza wengi wanajua Disemba 09 ni siku ya Uhuru wa Tanzania. Hizo story za Uhuru wa Tanganyika mnaozishikia bango Sana ni wale wa upande wa Pili. Sisi Wa bara Tunaamini, Tanganyika ilibadilishwa jina na kuitwa Tanzania baada ya kujiongezea mipaka yake kisiasa kuhusisha na visiwa vya unguja na Pemba.
 
Binafsi naamini tunasherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika ambayo leo haipo bali tuna Tanzania.

Ukisema kwa mfano miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika unamaanisha nini? Tanzania ina miaka 57 na Tanganyika haipo.

Karibu kwa mjadala chanja.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote Majilio haya!
Kwani binti yako nikimuoa na kuanza kuitwa Mrs Izia kunampunguzia umri wake?
 
Back
Top Bottom