Ni kosa la kustahili kutekwa kudai Katiba mpya Tanzania?

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,118
2,000
Katiba ya inchi ni makubaliano au utaratibu unaowekwa na wananchi wote namna gani taifa lao litawaliwe. Content kubwa ya katiba iliopo tume rithi kutoka katiba ya ukoloni.

Wakati wa uongozi wa awamu ya nne ya Urais chini ya mweshimiwa Rais Kikwete kulianzishwa mchakato wa katiba mpya. Bahati mbaya mchakato uliishia njiani japo lingekua jambo jema ungefika mwisho na inchi kupata katiba mpya.

Bado kumekuwepo na uhitaji mkubwa wa katiba mpya. Sidhani kama nikosa raia kudai katiba mpya ambayo shahiri dhahiri ni hitaji mhimu kwa taifa letu kwa sasa.

Sasa inapojitokeza hali ya watu kutekwa kwa kudai katiba mpya huku hata watekaji wakijua kinachodaiwa ni kwa faida ya ustawi wa taifa, kizazi cha sasa na vizazi vingine vingi vijavyo, ni uwenda wazimu na kuangalia shibe yao tu yaleo.

IMG_20210528_191747.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom