Ni kosa kumuuliza Mwenzi kuhusu uhalali wa watoto wako?

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,365
7,606
Hivi karibuni na labda tokea zamani kumekuwapo na wimbi la wazazi wa kike kubainika kuwa waliwabambikizia wazazi wakiume watoto wasio wao.

Jambo hilo limekuwa likileta mtafaruku katika ndoa na familia nyingi pale inapobainika kuwa mtoto si wa baba mwenyenyumba.

Hii ni kwa sababu hakika ni jambo baya sana kwa Mwanamke kutoka nje ya ndoa kuliko mwanaume.

Mara baada ya visa kadhaa vya mauaji na kuumizana kimwili kunakopelekewa na bainiko la mtoto wa nje ya Ndoa ndani ya ndoa, nimeonelea ni vyema kwa wale wanaume wenye roho nyepesi na ambao watoto wamefanana zaidi UJOMBANI, Kuhoji wake/wanawake zao kuhusu uhalali wa watoto.

Je, ni Kosa Kumuuliza Mke/Mwanamke wako uhalali wa mtoto na yeye awe huru tuu kukueleza kama ni wako au sio wako ili ufanye maamuzi sahihi kabla hujachelewa?

Maana kunamsemo wa kiswahili usemao "Chelewa Chelewa Utamkuta Mwana Si wako".

Nawasilisha
 
ME wameshtuka na ile kauli ya "kitanda hakizai haramu" kama vile wanakandamizwa na dunia maana hawana watetezi wa haki sawa na KE ilihali kiuhalisia KE wenyewe hawawezi kulea damu zisizotokana na Waume zao...

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Ni Kweli na Kama Mwanaume ni mchepukaji na Mke amejua, kuwa Makini Sana maana adhabu kubwa anayoweza Kukupa ni kuzaa nje ya Ndoa.
 
Unaweza kuwauliza lakini kwamba watajibu nini utakuwa utajua.
Hiyo ni sawa na kumuuliza mtu kama ni mwizi, hata angekuwa mwizi sidhani kama angekwambia kuwa yeye ni mwizi. Au kumuuliza mdada kama huwa anagawa sana mbunye, hata kama ni malaya naamini hatokubali. Kifupi tu ni kuwa kati ya binadamu 100 labda ni mawili au wa3 tu wanaoweza kukubali makosa yanayoweza kuwaharibia sifa zao mbele ya jamii, kuwaharbia mahusiano ambayo bado wanayahitaji au kuua utu wao.
 
Majibu yalishatolewa. Kitanda hakizai haramu. Familia masikini ndo wanasema mtoto si wa kwangu au binti yangu kuzalia nyumbani ni mwiko. Familia zinazohitaji kujiimarisha kiukoo zinafurahi kuletewa hata mtoto wa kusingiziwa na binti akipata mimba kabla ya kuolewa anajengewa geto lake. Kama unahitaji ushahidi nenda mkoa wa mara ambapo hadi mwanamke anatoa mahari, anamiliki msichana, anaalika vijana wampe mimba binti anayemmiliki halafu watoto ni wa boma wala si wa mtia mimba.
 
Ni Kweli na Kama Mwanaume ni mchepukaji na Mke amejua, kuwa Makini Sana maana adhabu kubwa anayoweza Kukupa ni kuzaa nje ya Ndoa.
ZABURI 34:7

"Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa."

KE hawana kanuni kabisa kustaarabika, muhimu ni kumwomba sana Mungu asimamie upendo na ulinzi thabiti wa ndoa, la sivyo hata usipochepuka bado ni kazi bure tu kwa KE.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom