Ni kosa kubwa sana kwa askari kunyang'anywa silaha yake

LMG na hizo zingine ulizozitaja, huwa zinapiga target iliyo karibu na mwenye silaha? Mtu yuko karibu na wewe mnaongea wawili, LMG inakusaidiaje katika mazingira ya aina hiyo, just in case akiamua kukugeuka ghafla? Ulipita JKT wapi wewe?
Mbona umekimbilia LMG na kuziacha SMG na AK47 kwenye swali lako? Nilitaka kukuonyesha kuwa unaweza kutumia hata LGM kama adui angeonekana kutoka mbali. Lakini inaonekana kuwa adui alilisogelea lindo bila kuonekana hadi akaifikia target yake kwa kisilaha cha kipuuzi kama pistol. Malindo yetu yote lazima yawe na kitu kwenye afya wanaita "care of the carer". Yaani askari lazima awe hai kabla ya kulinda uhai wa wengine. Askari mwenye silaha lazima alindwe na askari mwingine mwenye silaha, shida ya baadhi ya askari polisi wetu wote wanamkimbiza mwizi na kusahau adui zake na adui zake na wale wa silaha yake
 
Hamza alifanya ambush... Kwenye ambush hata awe komando ananyanganywa silaha vizuri tu maana kwenye silaha wa kwanza kubonyeza trigger ya silaha yake ndio mshindi.

Bunduki sio Kama jiwe kile ni chuma kikipita kwenye nyama ushaisha mapema tu.

Kwa hiyo kwenye ambush kijeshi mkitegwa hata platoon nzima inaweza kumalizwa na maadui wawili tu.

Tulishapigwa ambush kalemie Congo kwenye oparesheni ya kijeshi. Usiombee.
Acha kutetea wewe,yule askari wa pili anakimbia nini baada ya mwenzie kufa,ni kweli alikua kajeruhiwa ila hakutakiwa ampe mgongo,mbinu nzuri ya kujilinda ni kushambulia kama features zinazokufanya ujifiche kirahisi hamna...wamefuata mishahara tu hao madogo huko,wengine nikiwaona nawaonea huruma tu walivo.
 
Hamza naye hakuwa boya. Na pistol na SMG japo zina nguvu tofauti ila ukweli ji kuwa zote zinaua! Kwa namna alivyofanya tukio Hamza, hata commandor anakufa tu. Silaha sio issue ya positioning and power pekee ila TIMING ndio kimsingi main issue.

Mazingira ya ghafla ni rahisi kutumia pistol kuliko silaha kubwa hasa kama adui yuko karibu na pia mazingira ya pembeni kuna raia au mali za watu. Huanzi kufyatua tu risasi kwa SMG kumlenga Hamza bila kujali risasi ikimkosa Hamza inaweza kuleta madhara gani kwa waliopo around.

Ni rahisi kukosoa na kulaumu lakini uhalisia wa tukio kwenye ground ni tofauti na hizi keyboards tunazotumia hapa.
 
Mbona umekimbilia LMG na kuziacha SMG na AK47 kwenye swali lako? Nilitaka kukuonyesha kuwa unaweza kutumia hata LGM kama adui angeonekana kutoka mbali. Lakini inaonekana kuwa adui alilisogelea lindo bila kuonekana hadi akaifikia target yake kwa kisilaha cha kipuuzi kama pistol. Malindo yetu yote lazima yawe na kitu kwenye afya wanaita "care of the carer". Yaani askari lazima awe hai kabla ya kulinda uhai wa wengine. Askari mwenye silaha lazima alindwe na askari mwingine mwenye silaha, shida ya baadhi ya askari polisi wetu wote wanamkimbiza mwizi na kusahau adui zake na adui zake na wale wa silaha yake
Soma tena nilichoandika hapo juu. Soma kwa makini maneno matano ya mwanzoni kwenye sentensi yangu ya kwanza kabisa
 
Hamza naye hakuwa boya. Na pistol na SMG japo zina nguvu tofauti ila ukweli ji kuwa zote zinaua! Kwa namna alivyofanya tukio Hamza, hata commandor anakufa tu. Silaha sio issue ya positioning and power pekee ila TIMING ndio kimsingi main issue.

Mazingira ya ghafla ni rahisi kutumia pistol kuliko silaha kubwa hasa kama adui yuko karibu na pia mazingira ya pembeni kuna raia au mali za watu. Huanzi kufyatua tu risasi kwa SMG kumlenga Hamza bila kujali risasi ikimkosa Hamza inaweza kuleta madhara gani kwa waliopo around.

Ni rahisi kukosoa na kulaumu lakini uhalisia wa tukio kwenye ground ni tofauti na hizi keyboards tunazotumia hapa.
Polisi wa wenzetu anakuwa na silaha kubwa mkononi, pistol kiunoni, kisu na kabomu hata kamachozi sehemu fulani kama silaha zake za kutumia kulingana na tukio, mazingira na ukubwa wa tatizo
 
Ni kweli lakini kwa askari wetu nadhani kama mnavyowaona kuna wengine hata basic tools tu hawana. Lakini pamoja na kuwa na silaha zote hizo, timing ikifanyika basi tena!
Na ndio maana nadhani Hamza alimshoot yule mlinzi binafsi sababu alikuwa na silaha na angeweza kumletea madhara mapema au Vinginevyo aliunganishwa kwenye kundi la askari tu aisee
 
Nilipitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja miaka hiyo. Baada ya kumaliza ukuruta (pass out) tulipatiwa uwezo wa kulinda vituo mbalimbali kwa kutumia silaha za moto. Onyo kali tulilopewa ni kuhusu ubaya wa askari kunyang'anywa au kupoteza silaha yake, kofia, buti au chochote kinachomfanya aweze kutimiza majukumu yake ya uaskari.

Tufanye nini ili wananchi tuambiwe ni kwanini askari wetu walipokonywa silaha zao na Hamza?

Kwanini Hamza asingeachwa ili ahojiwe zaidi yeye mwenyewe?

Hakuna aliyestahili kujiuzulu kwa tukio lote lile?
We ukifa kwanza bunduki ikachukuliwa, nani anakuwa amepokonywa bunduki, wewe au maiti yako?
 
Ni kweli lakini kwa askari wetu nadhani kama mnavyowaona kuna wengine hata basic tools tu hawana. Lakini pamoja na kuwa na silaha zote hizo, timing ikifanyika basi tena!
Na ndio maana nadhani Hamza alimshoot yule mlinzi binafsi sababu alikuwa na silaha na angeweza kumletea madhara mapema au Vinginevyo aliunganishwa kwenye kundi la askari tu aisee
Kwani wakiwa depo hawafundishwi mambo ya timing? kama unajua kuna mambo ya timing kwanini askari anawageuzia mgongo watazamaji kwenye mpira?

Nilipokuwa JKT niliambiwa kuwa kwenye lindo usikae sehemu ya wazi pande zote nne ili uwe makini na upande wa mbele tu, yaani nyuma yako lazima kuwe na kizuizi kama ukuta, mwamba, nk ili adui asitokee nyuma yako. Kama hakuna ukuta basi angalia zaidi sehemu yenye hatari zaidi. Usivute sigara usiku kwenye lindo ili adui asifahamu ulipo, usiwashe taa yoyote ulipo, walinzi msikae wote sehemu moja, msiangalie wote upande mmoja. Haya yote yalikuwa mafunzo ya kujaribu kupunguza hiyo timing yako unayohubiri.
 
Pamoja na mafunzo yote hayo, huamini kuwa hata wewe ingeweza kutokea adai, hasa mwenye mafunzo kama yako au kuzidi yako na anayajua yote hayo akakukabili kwa mbinu zake na akakuondoa? Maana ya timing ni kuwa haiwezekani muda wote kwa sababu wewe ni mlinzi basi utakuwa wa kwanza kufanya timing kumdhibiti adui. Kumbuka timing inayoongelewa hapa sio dakika au saa, ni sekunde!

Kubali na uupe nafasi udhaifu wa kibinadamu kuwa pamoja na kuwa sawa tukio linaleta mafunzo/lesson learned lakini hata wewe na mafunzo yako lingeweza kukupata vizuri tu.

Na kitu kingine, ujue kabisa, mazingira ya lindo kama pale salender ambapo kuna magari yanapita muda wote, sio kweli kuwa askari hata angekuwa na nafasi hiyo, angerusha risasi ovyo kumlenga Hamza bila kujali risasi zitakazomkosa zitampata nani (raia).

Limeshatokea na limetoa funzo kwa namna mbali mbali ila lawama zisiwaendee askari waliouwawa kuwa walikuwa wazembe!
 
Back
Top Bottom