Ni kosa kisheria kurusha nyimbo bila idhini ya mwenye nao. Mtu anaweza kulipa faini au kufungwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,463
2,000
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Dkt. Ezekiel Kiongo amesema kumrushia mtu wimbo bila idhini ya mwenye nao ni kosa hata kama huuzi. Amesema ni kosa kurusha kazi ya mtu mwingine bila kibali chake.

Amefafanua, "Kwenye Sheria ya Mtandao (Cyber Law) inakataza na inasema mtu anaweza kulipa faini ya Milioni 5 au kifungo cha miaka mitatu. Unaweza ukaenda jela miaka mitano au zaidi, lakini ukalipa faini ya Milioni 20 au vyote kwa pamoja vile Mahakama inavyoona inafaa kama unauza na Msanii hana habari"

Amesema wasanii wanapaswa kujitokeza haki zao zinapokiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa ili kukomesha wizi kwenye kazi za sanaa

Chanzo: Bongo 5
 
Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,602
2,000
Video library za mtaani mtaji wenyewe laki 3
Faini milioni 20 wakiamua kufanya hii operesheni vijana wote wataishia SEGADANCE

Je wale jamaa wanaoweka MOVIE za mbele nao vipi mana sasa hivi wametapakaa wanaji promote mpk Instagram.

Na je sisi wa torrent hio adhabu haituhusu eeeh WARNER'S BROTHERS and Co waache kazi zao huko waje kukimbizana na sisi.

Hili swala ngumu kumeza ikiamuliwa livaliwe njuga hatoki mtu aisee mana wakidaka hizo PC zetu watabamba maushaidi ya kufa mtu
Nusu ya wana JF tutaishia segadance.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
20,197
2,000
Vitu vyengine huwa vinaachwa ili msilete mikwaruzano lukuki
 
zous

JF-Expert Member
Sep 25, 2017
475
1,000
Hiv kweli Wale wenye vibanda vya cd na kurusha nyimbo wamuombe Mondi au Kiba ruksa ya kurusha nyimbo zao.
 
Johnny Impact

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
2,884
2,000
Umasikini wako siyo sababu ya wewe kuvunja sheria.
Video library za mtaani mtaji wenyewe laki 3
Faini milioni 20 wakiamua kufanya hii operesheni vijana wote wataishia SEGADANCE

Je wale jamaa wanaoweka MOVIE za mbele nao vipi mana sasa hivi wametapakaa wanaji promote mpk Instagram.

Na je sisi wa torrent hio adhabu haituhusu eeeh WARNER'S BROTHERS and Co waache kazi zao huko waje kukimbizana na sisi.

Hili swala ngumu kumeza ikiamuliwa livaliwe njuga hatoki mtu aisee mana wakidaka hizo PC zetu watabamba maushaidi ya kufa mtu
Nusu ya wana JF tutaishia segadance.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom