Ni kosa gani ulilowahi kusingiziwa au kuadhibiwa wakati hukulitenda ng’o?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,488
17,685
Katika maisha yetu ya kila siku kuna kusingiziwa na maonevu ya hapa na pale, hasa pale mtu unaposingiziwa kosa na hata kuadhibiwa bila sababu. Hii ni hali ya kawaida kabisa katika maisha kwa kuwa tunaishi katika dunia iliyojaa watu wa aina mbalimbali na wenye maamuzi anuwai.

Sio rahisi binadamu yeyoye yule asipitie hali kama hii akiwa shuleni, nyumbani au mtaani. Kwa mfano, binafsi nimewahi kusingiziwa na hata kuadhibiwa kwa makosa kadhaa mabayo sikuyatenda ng’o. Na hili sio kwangu tu, hata kwako pia huenda kwa namna moja au nyingine uliwahi kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukulitenda hata kidogo, lakini maisha yakaendelea kama kawaida. Ila kuna siku ukikaa chini na kutafakari unajisemea moyoni: “siku ile niliadhibiwa bila kosa masikini mie!!”. Inauma lakini unapiga moyo konde na kusonga mbele. Ndivyo maisha yalivyo.

Mimi nimewahi kusingiziwa mara kadhaa na kuadhibiwa bila shuruti kwa makosa mbalimbali ambayo sikuyatenda kabisa. Mosi, wakati nikiwa mtoto mdogo huko kijijini kwetu Mchambawima, niliwahi kusingiziwa kudokoa mboga nikaadhibiwa kulala bila kula na masimamgo juu kwamba, “umevuna ulichopanda nenda kalale na njaa ujifunze adabu njema”. Kwa kuwa niliadhibiwa na wazazi baada ya wao kujiaminisha kimakosa, sikuwa na namna bali kukubali adhabu bila shurti baada utetezi wangu kugonga mwamba.
1642594755386.png

Wakati fulani binadamu huvuta hisia nzuri na mbaya za wakati uliopita

Pili, wakati nikisoma shule siku moja kulikuwa na concert kule ukumbini. Siku hiyo sikuwa nafahamu kwamba kuna concert hivyo nikaenda zangu kule gallery kujisomea prep kama kawaida yangu. Ghafla akaja prefect mmoja na kuniuliza kwanini nimeingia kule gallery na kunituhumu kuwa nimeenda pale ili kutazama conert bila kulipia.

Nilijaribu kumfahamisha kuwa sikuwa nafahamu kuhusu uwepo wa concert yenyewe na hata conert yenyewe ilikuwa haijaanza. Ningesikia kelele za concert wala nisingeenda mle kujisomea. Pamoja na kwamba nilikuwa na madaftari ya kujisomea hakunielewa katu. Akanipeleka kwa mwalimu Mgimwa akanipa adhabu ya kuchimba kisiki nyuma ya bweni la Shaaban Robert East.

Niliamua kukubali yaishe kwa kuwa wakati huo maprefects wa Complex walikuwa wanajiona ni miungu watu. Nikaadhibiwa na maisha yakaendelea. Lakini kitendo kile kinaniuma mpaka leo. Yapo maonevu mengi ambayo nimewahi kuadhibiwa bila kosa, lakini kwa uchache nimeltaja haya mawili kama sample.

Ni dhahiri kuwa hata wewe kwa namna moja au nyingine uliwahi kusingiziwa au kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukuwa umelitenda lakini ukakubali kufunika kombe mwanaharamu apite. Hebu tuambie ilikuwaje na ulidahibiwaje.

Nawasilisha.​
 
Manjiani majuzi tu hapa..

Kuna Khenge iliniovateki ndani ya eneo la 50 wakati huo Niko below 50, cha kushangaza eti tukasimamishwa wote kuwa Tume Over speed.. Wale Mbwa nilibishana nao mpaka nikamua waniandikie tu 30 kuliko niwapooze na 10..

Jamaa angu akanitonya kuwa kuna namna huchukua speed ya Wa mbele yako Ila Picha wanakupiga wewe.
 
Wazee wa 50 achana nao kabisa; wana uonevu wa kijinga usiombe ukakutana nao hasa wakiwa na njaa!
 
Wakati nipo shule ya msingi kulikuwa na tabia ya walimu kuanzisha miradi yao na kuwapa wanafunzi wauze wakati wa mapumziko wanafunzi wa darasa husika mlikuwa mnagawanywa watatu watatu kila siku sasa siku hiyo sikwenda shule wale wenzangu walipopewa ile hela wakagawana wakaila wakamwambia mwalimu hela wamenipa mimi nikanunue mihogo na sikuja shule daah baada ya siku mbili nimefika shule mwalimu ananidai hela nikabaki nashangaa sitamsahau yule mwalimu alinichapa fimbo na huku anawaambia wanafunzi wanizomee darasani baada ya hapo ananiambia nirudishe pesa ambayo sikuchukua kabisa nilikaa nyumbani miezi mitatu sitaki kusikia shule kabisa hili tukio lilitokea nikiwa darasa la tatu
 
Nilipiga mtoto wa mtu roba nikaiba shilingi ishirini yake,wakaja nisingizia kuwa nimeiba hamsini badala ya ishirini!
 
Katika maisha yetu ya kila siku kuna kusingiziwa na maonevu ya hapa na pale, hasa pale mtu unaposingiziwa kosa na hata kuadhibiwa bila sababu. Hii ni hali ya kawaida kabisa katika maisha kwa kuwa tunaishi katika dunia iliyojaa watu wa aina mbalimbali na wenye maamuzi anuwai.

Sio rahisi binadamu yeyoye yule asipitie hali kama hii akiwa shuleni, nyumbani au mtaani. Kwa mfano, binafsi nimewahi kusingiziwa na hata kuadhibiwa kwa makosa kadhaa mabayo sikuyatenda ng’o. Na hili sio kwangu tu, hata kwako pia huenda kwa namna moja au nyingine uliwahi kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukulitenda hata kidogo, lakini maisha yakaendelea kama kawaida. Ila kuna siku ukikaa chini na kutafakari unajisemea moyoni: “siku ile niliadhibiwa bila kosa masikini mie!!”. Inauma lakini unapiga moyo konde na kusonga mbele. Ndivyo maisha yalivyo.

Mimi nimewahi kusingiziwa mara kadhaa na kuadhibiwa bila shuruti kwa makosa mbalimbali ambayo sikuyatenda kabisa. Mosi, wakati nikiwa mtoto mdogo huko kijijini kwetu Mchambawima, niliwahi kusingiziwa kudokoa mboga nikaadhibiwa kulala bila kula na masimamgo juu kwamba, “umevuna ulichopanda nenda kalale na njaa ujifunze adabu njema”. Kwa kuwa niliadhibiwa na wazazi baada ya wao kujiaminisha kimakosa, sikuwa na namna bali kukubali adhabu bila shurti baada utetezi wangu kugonga mwamba.
View attachment 2088082
Wakati fulani binadamu huvuta hisia nzuri na mbaya za wakati uliopita

Pili, wakati nikisoma shule siku moja kulikuwa na concert kule ukumbini. Siku hiyo sikuwa nafahamu kwamba kuna concert hivyo nikaenda zangu kule gallery kujisomea prep kama kawaida yangu. Ghafla akaja prefect mmoja na kuniuliza kwanini nimeingia kule gallery na kunituhumu kuwa nimeenda pale ili kutazama conert bila kulipia.

Nilijaribu kumfahamisha kuwa sikuwa nafahamu kuhusu uwepo wa concert yenyewe na hata conert yenyewe ilikuwa haijaanza. Ningesikia kelele za concert wala nisingeenda mle kujisomea. Pamoja na kwamba nilikuwa na madaftari ya kujisomea hakunielewa katu. Akanipeleka kwa mwalimu Mgimwa akanipa adhabu ya kuchimba kisiki nyuma ya bweni la Shaaban Robert East.

Niliamua kukubali yaishe kwa kuwa wakati huo maprefects wa Complex walikuwa wanajiona ni miungu watu. Nikaadhibiwa na maisha yakaendelea. Lakini kitendo kile kinaniuma mpaka leo. Yapo maonevu mengi ambayo nimewahi kuadhibiwa bila kosa, lakini kwa uchache nimeltaja haya mawili kama sample.

Ni dhahiri kuwa hata wewe kwa namna moja au nyingine uliwahi kusingiziwa au kuadhibiwa kwa kosa ambalo hukuwa umelitenda lakini ukakubali kufunika kombe mwanaharamu apite. Hebu tuambie ilikuwaje na ulidahibiwaje.

Nawasilisha.​
Daaa mchumba alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja katika kitengo cha kubambikia watu kesi, kuchepuka kulipo noga jamaa akampanga waniwekee madawa ya kulevya ili nitupwe sero wao wale maisha. Acha tu niishie hapa
 
Du pole sana mkuu; hapa duniani kuna kuoneana kwingi wewe acha tu!
 
Wakati nipo shule ya msingi kulikuwa na tabia ya walimu kuanzisha miradi yao na kuwapa wanafunzi wauze wakati wa mapumziko wanafunzi wa darasa husika mlikuwa mnagawanywa watatu watatu kila siku sasa siku hiyo sikwenda shule wale wenzangu walipopewa ile hela wakagawana wakaila wakamwambia mwalimu hela wamenipa mimi nikanunue mihogo na sikuja shule daah baada ya siku mbili nimefika shule mwalimu ananidai hela nikabaki nashangaa sitamsahau yule mwalimu alinichapa fimbo na huku anawaambia wanafunzi wanizomee darasani baada ya hapo ananiambia nirudishe pesa ambayo sikuchukua kabisa nilikaa nyumbani miezi mitatu sitaki kusikia shule kabisa hili tukio lilitokea nikiwa darasa la tatu
Hee! Hii ni hatari sana. Na ikitokea hivi hata mtu ujitetee namna gani hufui dafu, sijui hata watu wengine wanakuwa wanawaza nini wakati wanatoa maamuzi ya kukurupuka.
 
Daaa mchumba alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja katika kitengo cha kubambikia watu kesi, kuchepuka kulipo noga jamaa akampanga waniwekee madawa ya kulevya ili nitupwe sero wao wale maisha. Acha tu niishie hapa
Aisee pole sana, ungetupa kisa chenyewe japo kwa ufupi tupate la kujifunza.
 
Nikiwa sekondari o-level kuna binti tunafananishwa sana hususani na watu wa madarasa mengine.

One day, mwalimu wa Chemistry akiwa laboratory akaona mtoto wa mlinzi wa shule ameenda kwenye majani nyuma ya lab akaficha mzigo chini ya kanga iliyokuwa imetandikwa pale.

Mwalimu akajua tu ni ishu ya magendo. Akaenda kuangalia akakuta package za kutosha za chips mayai. Alipofika eneo lile kulikuwa na binti mmoja wa a-level amekaa kwenye majani akijisomea. Mwalimu akashawishika kuwa ule ni mzigo wake. Binti akaukataa kata kata.

Mwalimu akamwambia adhabu yake anamfungia ndani ya laboratory awe mlinzi aangalie nani atakuja kuchukua mzigo ule.

Kwa bahati mbaya, mzigo ule ulikuwa wa yule mtu ambaye tulikuwa tunafananishwa na alikuja kuuchukua. Mwalimu aliporudi yule mtuhumiwa namba moja akasema ni Zurie ndo amekuja kuuchukua ule mzigo.

Kesho yake mwalimu ananiita na kuniambia “siamini na wewe unafanya matendo ya kuvunja sheria za shule, umeanza lini?” I was so shocked. Maana nilikuwa a law-abiding student sina makuu zaidi ya kusoma.

Aisee mwalimu kuona nakataa nikapelekwa kwa matron, kufika kwa matron nikakataa, nikapelekwa kwa mkuu wa shule. Nikasema sio mimi na nikademand yule mtoto wa mlinzi aje aseme kama nimewahi hata kuzungumza naye.

Dogo alipokuja ndo ikawa pona pona yangu. Akamtaja mhusika. Ila cha kushangaza nilichukiwa na karibu darasa zima eti ni snitch, kwamba nilitakiwa kulikubali kosa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom