Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Wakati najiandaa kwenda Chuo nilikutana na mbunge wa enzi za baba Liz akaniambia kama unataka kusoma ,basi kasome koz Fulan hutojuta, nikasoma hiyo koz isitoshe nilikuwa napenda wanavyovaaga smart na professional.
Kumaliza Chuo ajira wapi nikaanza ujasiliamali, na par time jobs.mama alinisema kwa nini nilisoma kozi hiyo, kuna kipindi ilifika na mm ni kasema najutraaa.why, nilikuwa Naomba kufanya kazi ambayo sikusomea hasa private sectors ilinibidi nisome zaidi.nikiwa na presentation, utafikiri Nina mtihani wa necta.

Ila moyoni nikabaki najisemea nilifanya right decision kusoma hii koz itanifanya niwe ninachotaka , najiamini naongea na kila mmoja, nikajisemea Siku ipo Iile vazi ntalitendea haki

Mungu sio mchoyo hata Siku moja, sasa hivi nikiangalia phone book yangu, inabadirika every day,😂😂hadi international no, inapobidi nasafiri😁😁😁😁

Mtu asikulazimishe ufanye kitu ambacho moyo haupendi.
Kwa hiyo mkuu sasa hivi umejikita kufanya kazi ambayo hujasomea lakini ambayo unaipenda? Sio wewe tu, tupo wengi.
 
inatakiwa walau mtu wa degree ya miaka mitatu kama ameenda straight amalize akiwa na 21 yrs awahi kupambana na maisha
Hii ishu ya kusoma imeniudhi sana mimi. Kati ya mistake nilifanya, ni kungangania kwenda chuo. Nothing new. Kupoteza muda tuu. Nina wasiwasi na jinsi nitakavyopanga elimu ya wanangu hlf ntajua jinsi ya kuwatengenezea njia yao mana kweny mfumo wetu wa elimu ni hewa tuu na kuna ukungu wa kutosha sana, cha muhimu nizisake noti kwanza
 
Najutia kutokwenda academy ya soka jijini Mwanza iliyokuwa chini ya Sylvester Mash nikiwa form two 2009 mipango niliandaa vyema kabisa sijui hata ilikopotelea jamani. Kuna huyu mtu anaitwa RICARDO IZECSON DOS ANTOS LEITE maarufu kama "KAKA" ndo nilikuwa namuangalia kama role model wakati anakiwasha pale AC MILAN na akina Pirlo, nilishuhudia akiwachakaza Man U pale Old Trafford na kutinga hatua ya Fainali walipocheza na Liverpool mwaka 2007. Hadi leo "KAKA" anabaki kuwa ndo binadamu pekee kuchukua tuzo mbele ya LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo. Nilitaka kuja kufanya unyama kama wa "KAKA" lakini Mungu hakupi unachotaka bali anakupa unachostahili.
USIJALI KUNA MTU ALITAK AWE RUBANI MAMBO HAYAKWENDA KAMA AKIVUOPANGA AKAISHIA KUFUGA KUKU ...... sasa sijui ndege akimaanisha nn
 
Kwa hiyo mkuu sasa hivi umejikita kufanya kazi ambayo hujasomea lakini ambayo unaipenda? Sio wewe tu, tupo wengi.
haaaaaa asante nikidhani nimepotea njia mm vyeti nimeweka ndani nainjoy maisha kwa mambo mengine kabisa nadhani sisi ndonwale walioenda shule wakaelimika wakatawala mazingira nakuyamanipulate watakavyo, japo nje siendi ila wa nje wanakuja kwangu...
 
Mimi sitasahau kipindi nataka kuanza kidato cha kwanza, sasa kwenye maandalizi siunajua wengine familia zetu bilabila mzee hana kitu (hili labda sio tatizo maana hana)

Sasa mimi nilikua nina hela kdogo maana nlivomaliza darasa la saba kuna mwalimu nilikua namuuzia duka lake. Huyo mwalimu alikua anafundisha hisabati sasa mimi ndo nilikua nawanyoosha hilo somo, huyo mwalimu alikua ananikubali sana nlivo maliza tu akanipa kazi.

Sasa upuuzi nlofanya baada muda wa kuanza kidato cha kwanza kufika. Yule mwalimu alinilipa si nikachukua 10,000/= nikampa mshua akaninunulie kiatu(nilimpa maana alinambia town kuna viatu vizuri) zingine nkashona uniform na daftari nikabakiza elfu kumi tu ya ada.

Mshua hakununua kiatu ile hela sijui alifanyia nini? mi nikawa nmekaa tu siendi kuanza shule mara wiki ya kwanza ikaisha, ya pili hapo siwezi kumletea kibesi mshua arudishe hela au anipe kiatu.
Wiki ya tatu nikaona udwanzi huu sasa nikavaa uniform zangu nikavaa kiatu chake kilikua kikubwa kishenzi, hakinitoshi afu kibaya. Miaka 15 saivi imepita siwezi kusahau.

Hakuninunulia kiatu nilivaa lile lakuchumpa lake mpaka likaisha kidato cha pili.

Lakuchumpa ukatinga nalo hahaaaahaaaaaaaa
 
inatakiwa walau mtu wa degree ya miaka mitatu kama ameenda straight amalize akiwa na 21 yrs awahi kupambana na maisha
Kwa saiv hiii naona inawezekana, ni tofauti na umri wa watu waliopita. Kipind cha nyuma, watu kumaliza form 4 au kuanza form one, umri ulikua mkubwa. Saiv vijana ni wadogo lakin yuko form 4 au kamaliza form six anasubr tokeo. Utofaut upo sana.
 
niliwahi disco chuo fulan kwa uzembe sana kisa ilikuwa pesa kwa sababu niliamini nipo kwenye haki sikutoa mwisho wa siku nikajikuta nimedisco nilijuta sana maisha yangu yalibadilika nilianza umwa hovyo kila nikienda hospital pima naambiwa sina tatizo lakin naumwa sana ilifika mahali nilinusulika ajali ya gari nikawa nalaumu kwanin nimepona hii ajali masikini ya mungu kumbe nilikuwa napita mahali ili kujijenga zaidi badae nilifanya maamuzi magumu nikarudi chuo,maisha yakabadilika nikaanza pata marafiki wapya nikajifunza vitu vipya vingi sana namshukuru mungu ule muda haukupotea bure niliyojifunza ni zaid ya ile miaka mitatu niliyopoteza kule mwanzo now nimegraduate maisha yangu si ya majuto tena nimekuwa mtu mwenye furaha sana na kule kudisco kumekuwa fundisho kubwa sana kwangu sitokuja kuwa mtu wa majuto tena na kulaumu si sehemu ya maisha yangu tena.
Nawasilisha
BAADA YA KUGRADUATE KAPIME TENA TUPE MREJESHOO
OV2.5
 
Mie nimejifunza mengi
Mimi nakumbuka na kujuta kwa kujifunza kwa nn sikuchagua mchumba kipindi niko chuo kikuu, sasa nimeajiriwa sehemu toka 2014, hamna wadada, siwaelewi kbs, fujo , nilitaka nioe mwaka huu lkn sina Mdada!!! Du sijui nifanyaje? Au nisubiri walimu wapy nimuombe DIO nikae na dawati pembeni nijifanye nakagua vyeti nijichagulie m1.
I am totally frustrated, nataka kuoa
Mkuu nimecheka Sana eti ukae na dawati ujifanye unakagua vyeti ili ujipatie 1 mda ushapita Sasa miaka 3 kutoka 2016 vipi ulishaoa au Bado Mambo magumu
 
Nilifanya kosa la kutohudhuria msiba wa mama ambae alikuwa wa muhimu sana kwangu,najisikia vibaya sana..nashindwa kukusahau mama yangu mpenzi .. natamani unitokee uniambie umenisamehe. Mungu akulaze mahali pema KUNEGUNDA.
Pole sana
 
Nilimkosea baba angu kwa makusudi kabisa nikiamini akija atanipiga ili Na mimi TUZIPANGE,ila aliporudi alilia na kutoa machozi mbele yangu huku akiniuliza kwa upole na uchungu "kwanini sam" SITOSAHAU ILE SIKU najuta najuta hadi kesho nikikumbuka ile kitu.

Samahan Sam...niwe mkweli nimecheka balaa..nakuhisgi ww mtata.mtukutu kumbe kwel bwana..yaan naandika hapa nacheka balaa..hahahaa...nna 2nd born anataka kuwa km ww😂😂😂..dah
 
Mimi sitasahau kipindi nataka kuanza kidato cha kwanza, sasa kwenye maandalizi siunajua wengine familia zetu bilabila mzee hana kitu (hili labda sio tatizo maana hana)

Sasa mimi nilikua nina hela kdogo maana nlivomaliza darasa la saba kuna mwalimu nilikua namuuzia duka lake. Huyo mwalimu alikua anafundisha hisabati sasa mimi ndo nilikua nawanyoosha hilo somo, huyo mwalimu alikua ananikubali sana nlivo maliza tu akanipa kazi.

Sasa upuuzi nlofanya baada muda wa kuanza kidato cha kwanza kufika. Yule mwalimu alinilipa si nikachukua 10,000/= nikampa mshua akaninunulie kiatu(nilimpa maana alinambia town kuna viatu vizuri) zingine nkashona uniform na daftari nikabakiza elfu kumi tu ya ada.

Mshua hakununua kiatu ile hela sijui alifanyia nini? mi nikawa nmekaa tu siendi kuanza shule mara wiki ya kwanza ikaisha, ya pili hapo siwezi kumletea kibesi mshua arudishe hela au anipe kiatu.
Wiki ya tatu nikaona udwanzi huu sasa nikavaa uniform zangu nikavaa kiatu chake kilikua kikubwa kishenzi, hakinitoshi afu kibaya. Miaka 15 saivi imepita siwezi kusahau.

Hakuninunulia kiatu nilivaa lile lakuchumpa lake mpaka likaisha kidato cha pili.
, umenifurahisha sana na nadhani ulifurahi sana lilivoisha hilo buti la urithi
 
kosa nalojutia ni kukutana na mpenza wangu wa kwanza toka nipo sec, kilichotutenganisha niliama shule, sasa tumekutana tena sasa ninampenda kupitiliza ila sitakubali anivue chupi, sababu nimeshaolewa na nina watoto wawili nae kashaoa, ila wote tunapenda na nimemkisi mala kibao sababu lips zake nitamu kwa kukisi....
Labda si mwanaume ni mvulana ila nahis utapigwa miti soon
 
kosa nalojutia ni kukutana na mpenza wangu wa kwanza toka nipo sec, kilichotutenganisha niliama shule, sasa tumekutana tena sasa ninampenda kupitiliza ila sitakubali anivue chupi, sababu nimeshaolewa na nina watoto wawili nae kashaoa, ila wote tunapenda na nimemkisi mala kibao sababu lips zake nitamu kwa kukisi....
Akikaza anakuvua tena bila kipingamizi chochote!!
 
Back
Top Bottom