Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Pole sana ,hakuna lisilo sameheka
Nilifanya kosa la kutohudhuria msiba wa mama ambae alikuwa wa muhimu sana kwangu,najisikia vibaya sana..nashindwa kukusahau mama yangu mpenzi .. natamani unitokee uniambie umenisamehe. Mungu akulaze mahali pema KUNEGUNDA.
 
Nilimkosea baba angu kwa makusudi kabisa nikiamini akija atanipiga ili Na mimi TUZIPANGE,ila aliporudi alilia na kutoa machozi mbele yangu huku akiniuliza kwa upole na uchungu "kwanini sam" SITOSAHAU ILE SIKU najuta najuta hadi kesho nikikumbuka ile kitu.
Hahaaa nimejikuta nacheka,
Dah! Pole sana .katika maisha tunakumbana na matukio mengi .
 
Najutia kutokwenda academy ya soka jijini Mwanza iliyokuwa chini ya Sylvester Mash nikiwa form two 2009 mipango niliandaa vyema kabisa sijui hata ilikopotelea jamani. Kuna huyu mtu anaitwa RICARDO IZECSON DOS ANTOS LEITE maarufu kama "KAKA" ndo nilikuwa namuangalia kama role model wakati anakiwasha pale AC MILAN na akina Pirlo, nilishuhudia akiwachakaza Man U pale Old Trafford na kutinga hatua ya Fainali walipocheza na Liverpool mwaka 2007. Hadi leo "KAKA" anabaki kuwa ndo binadamu pekee kuchukua tuzo mbele ya LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo. Nilitaka kuja kufanya unyama kama wa "KAKA" lakini Mungu hakupi unachotaka bali anakupa unachostahili.
 
Najutia kutokwenda academy ya soka jijini Mwanza iliyokuwa chini ya Sylvester Mash nikiwa form two 2009 mipango niliandaa vyema kabisa sijui hata ilikopotelea jamani. Kuna huyu mtu anaitwa RICARDO IZECSON DOS ANTOS LEITE maarufu kama "KAKA" ndo nilikuwa namuangalia kama role model wakati anakiwasha pale AC MILAN na akina Pirlo, nilishuhudia akiwachakaza Man U pale Old Trafford na kutinga hatua ya Fainali walipocheza na Liverpool mwaka 2007. Hadi leo "KAKA" anabaki kuwa ndo binadamu pekee kuchukua tuzo mbele ya LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo. Nilitaka kuja kufanya unyama kama wa "KAKA" lakini Mungu hakupi unachotaka bali anakupa unachostahili.
Luka Modric' alichukua nini mwaka jana?
 
Najutia san kipindi nasoma chuo kuacha kuendelea kufanya biashara na kujikita katika masomo vizuri. Sasa nimemaliza chuo nina gpa nzuri nipo tu sina hata pesa ya vocha kazi hakuna daah wale niliokuwa nafanya nao biashara zama izo tupo chuo biashara zao zimekuwa kubwa mitaji imepanuka na maisha yameanza kuwanyookea though wengine waliacha chuo na wengine wamemaliza ila kwa tabu sana na ufaulu mdogo. Mimi nimebakia tu na gamba langu zuri pasi na pesa mfukoni.

Nimekubali kosa nilibeti vibaya aisee na nakumbuka mshua wangi alikuwa ananikomalia niache kabisa habar za biashara nisome kwa bidii daaah sema nn i will bounce back stronger.
 
Kwa hesabu ya haraka hata Mimi naungana na wewe kwan unarudi unakuta baadhi ya darasa la saba uliowaacha wanamaendeleo,usafiri na maisha mazuri.
Hayo mafanikio ni kwa wachache tu waliowengi wanamaisha tu ya kawaida na ya chini.
Kwa elimu ulionayo unafanya mambo kwa mtazamo mpana Zaidi hata kama ni biashara pia utaiendesha kitaalamu
Pia kwa kutumia elimu unaweza kutengeneza fursa na kuifanyia kazi
shida ni mda tu, nimepoteza mda sana shuleni, nakuja kujishtukia tu nimezeeka
 
Mimi sitasahau kipindi nataka kuanza kidato cha kwanza, sasa kwenye maandalizi siunajua wengine familia zetu bilabila mzee hana kitu (hili labda sio tatizo maana hana)

Sasa mimi nilikua nina hela kdogo maana nlivomaliza darasa la saba kuna mwalimu nilikua namuuzia duka lake. Huyo mwalimu alikua anafundisha hisabati sasa mimi ndo nilikua nawanyoosha hilo somo, huyo mwalimu alikua ananikubali sana nlivo maliza tu akanipa kazi.

Sasa upuuzi nlofanya baada muda wa kuanza kidato cha kwanza kufika. Yule mwalimu alinilipa si nikachukua 10,000/= nikampa mshua akaninunulie kiatu(nilimpa maana alinambia town kuna viatu vizuri) zingine nkashona uniform na daftari nikabakiza elfu kumi tu ya ada.


Mshua hakununua kiatu ile hela sijui alifanyia nini? mi nikawa nmekaa tu siendi kuanza shule mara wiki ya kwanza ikaisha, ya pili hapo siwezi kumletea kibesi mshua arudishe hela au anipe kiatu.
Wiki ya tatu nikaona udwanzi huu sasa nikavaa uniform zangu nikavaa kiatu chake kilikua kikubwa kishenzi, hakinitoshi afu kibaya. Miaka 15 saivi imepita siwezi kusahau.

Hakuninunulia kiatu nilivaa lile lakuchumpa lake mpaka likaisha kidato cha pili.
 
Wakati najiandaa kwenda Chuo nilikutana na mbunge wa enzi za baba Liz akaniambia kama unataka kusoma ,basi kasome koz Fulan hutojuta, nikasoma hiyo koz isitoshe nilikuwa napenda wanavyovaaga smart na professional.
Kumaliza Chuo ajira wapi nikaanza ujasiliamali, na par time jobs.mama alinisema kwa nini nilisoma kozi hiyo, kuna kipindi ilifika na mm ni kasema najutraaa.why, nilikuwa Naomba kufanya kazi ambayo sikusomea hasa private sectors ilinibidi nisome zaidi.nikiwa na presentation, utafikiri Nina mtihani wa necta.

Ila moyoni nikabaki najisemea nilifanya right decision kusoma hii koz itanifanya niwe ninachotaka , najiamini naongea na kila mmoja, nikajisemea Siku ipo Iile vazi ntalitendea haki

Mungu sio mchoyo hata Siku moja, sasa hivi nikiangalia phone book yangu, inabadirika every day,😂😂hadi international no, inapobidi nasafiri😁😁😁😁

Mtu asikulazimishe ufanye kitu ambacho moyo haupendi.
 
kutumia miaka 25 ya maisha yangu kusoma tu ( mpaka chuo kikuu )....hua nahisi kama nimepoteza nusu ya maisha yangu, inaniumaga sana
Hii ishu ya kusoma imeniudhi sana mimi. Kati ya mistake nilifanya, ni kungangania kwenda chuo. Nothing new. Kupoteza muda tuu. Nina wasiwasi na jinsi nitakavyopanga elimu ya wanangu hlf ntajua jinsi ya kuwatengenezea njia yao mana kweny mfumo wetu wa elimu ni hewa tuu na kuna ukungu wa kutosha sana, cha muhimu nizisake noti kwanza
 
Back
Top Bottom