Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,478
17,676
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miaka 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miak 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kinaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?
Nafikiri kosa la kuanza shule na umri mkubwa halikuwa kosa lako.Hilo ni la wazazi maana kuanza shule kwa ninavyoelewa mtoto hana maamuzi yoyote kwa familia zetu nyingi za kiafrika.!!
Kwa hiyo wala usilijutie mkuu!!
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom