Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?


tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,345
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,345 2,000
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miaka 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
GACHIPA

GACHIPA

Senior Member
Joined
Dec 23, 2018
Messages
154
Points
250
GACHIPA

GACHIPA

Senior Member
Joined Dec 23, 2018
154 250
Nilimpenda sana Mdada mmoja kuliko maelezo nikiwa darasa la 5 yeye akiwa la 4 . Nilijitahidi kumtimizia kila alilohitaji na kuamini kuwa ndo atakuwa wa maisha.
Kadri siku zilivokuwa zikizidi ndo nilizidi kujichimbia shimo ambalo kutoka ilikuwa ngumu.
Hakuwahi kunambia hanitaki ila vitendo vilionesha ni mapenzi ya upande mmoja.
Nikawa nikijipa moyo huenda ni utoto atabadilika kumbe nazidi kujizamisha katika TOPE la mapenzi.
Nilidumu katika mapenzi kuanzia 2004-up to 2017 jambo ambalo limenifanya kutokuja kumpenda mwanamke yeyote (though pretending). Huo muda ulizidi kutengeneza mazingira yote that she was special.
Mwanzoni niliamini MPENDE MPENDAE. Baada ya kuona nasubiria meli airport. Ilibidi nioe kwa kufuata MPENDE AKUPENDAE.
Ningalikuwa na maamuzi sahihi mapema nisingalikuwa naumia mpaka muda huu kisa MAPENZI.
Aisee pole sana,haukuwahi hata kumuonja?wanawake viumbe vya ajabu kwelikweli
 
Meeyah

Meeyah

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2016
Messages
15,113
Points
2,000
Meeyah

Meeyah

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2016
15,113 2,000
Nilifanya kosa la kutohudhuria msiba wa mama ambae alikuwa wa muhimu sana kwangu,najisikia vibaya sana..nashindwa kukusahau mama yangu mpenzi .. natamani unitokee uniambie umenisamehe. Mungu akulaze mahali pema KUNEGUNDA.
 
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
359
Points
250
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
359 250
Pole sana ,hakuna lisilo sameheka
Nilifanya kosa la kutohudhuria msiba wa mama ambae alikuwa wa muhimu sana kwangu,najisikia vibaya sana..nashindwa kukusahau mama yangu mpenzi .. natamani unitokee uniambie umenisamehe. Mungu akulaze mahali pema KUNEGUNDA.
 
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
359
Points
250
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
359 250
Nilimkosea baba angu kwa makusudi kabisa nikiamini akija atanipiga ili Na mimi TUZIPANGE,ila aliporudi alilia na kutoa machozi mbele yangu huku akiniuliza kwa upole na uchungu "kwanini sam" SITOSAHAU ILE SIKU najuta najuta hadi kesho nikikumbuka ile kitu.
Hahaaa nimejikuta nacheka,
Dah! Pole sana .katika maisha tunakumbana na matukio mengi .
 
Born 2 Be Wild

Born 2 Be Wild

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
1,058
Points
2,000
Age
27
Born 2 Be Wild

Born 2 Be Wild

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
1,058 2,000
Najutia kutokwenda academy ya soka jijini Mwanza iliyokuwa chini ya Sylvester Mash nikiwa form two 2009 mipango niliandaa vyema kabisa sijui hata ilikopotelea jamani. Kuna huyu mtu anaitwa RICARDO IZECSON DOS ANTOS LEITE maarufu kama "KAKA" ndo nilikuwa namuangalia kama role model wakati anakiwasha pale AC MILAN na akina Pirlo, nilishuhudia akiwachakaza Man U pale Old Trafford na kutinga hatua ya Fainali walipocheza na Liverpool mwaka 2007. Hadi leo "KAKA" anabaki kuwa ndo binadamu pekee kuchukua tuzo mbele ya LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo. Nilitaka kuja kufanya unyama kama wa "KAKA" lakini Mungu hakupi unachotaka bali anakupa unachostahili.
 
Wild Thoughts

Wild Thoughts

Senior Member
Joined
Mar 17, 2019
Messages
156
Points
250
Wild Thoughts

Wild Thoughts

Senior Member
Joined Mar 17, 2019
156 250
Najutia kutokwenda academy ya soka jijini Mwanza iliyokuwa chini ya Sylvester Mash nikiwa form two 2009 mipango niliandaa vyema kabisa sijui hata ilikopotelea jamani. Kuna huyu mtu anaitwa RICARDO IZECSON DOS ANTOS LEITE maarufu kama "KAKA" ndo nilikuwa namuangalia kama role model wakati anakiwasha pale AC MILAN na akina Pirlo, nilishuhudia akiwachakaza Man U pale Old Trafford na kutinga hatua ya Fainali walipocheza na Liverpool mwaka 2007. Hadi leo "KAKA" anabaki kuwa ndo binadamu pekee kuchukua tuzo mbele ya LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo. Nilitaka kuja kufanya unyama kama wa "KAKA" lakini Mungu hakupi unachotaka bali anakupa unachostahili.
Luka Modric' alichukua nini mwaka jana?
 
mc gregor

mc gregor

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2017
Messages
428
Points
1,000
mc gregor

mc gregor

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2017
428 1,000
Najutia san kipindi nasoma chuo kuacha kuendelea kufanya biashara na kujikita katika masomo vizuri. Sasa nimemaliza chuo nina gpa nzuri nipo tu sina hata pesa ya vocha kazi hakuna daah wale niliokuwa nafanya nao biashara zama izo tupo chuo biashara zao zimekuwa kubwa mitaji imepanuka na maisha yameanza kuwanyookea though wengine waliacha chuo na wengine wamemaliza ila kwa tabu sana na ufaulu mdogo. Mimi nimebakia tu na gamba langu zuri pasi na pesa mfukoni.

Nimekubali kosa nilibeti vibaya aisee na nakumbuka mshua wangi alikuwa ananikomalia niache kabisa habar za biashara nisome kwa bidii daaah sema nn i will bounce back stronger.
 
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
359
Points
250
hazard Don

hazard Don

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
359 250
Kwa hesabu ya haraka hata Mimi naungana na wewe kwan unarudi unakuta baadhi ya darasa la saba uliowaacha wanamaendeleo,usafiri na maisha mazuri.
Hayo mafanikio ni kwa wachache tu waliowengi wanamaisha tu ya kawaida na ya chini.
Kwa elimu ulionayo unafanya mambo kwa mtazamo mpana Zaidi hata kama ni biashara pia utaiendesha kitaalamu
Pia kwa kutumia elimu unaweza kutengeneza fursa na kuifanyia kazi
shida ni mda tu, nimepoteza mda sana shuleni, nakuja kujishtukia tu nimezeeka
 
Wild Thoughts

Wild Thoughts

Senior Member
Joined
Mar 17, 2019
Messages
156
Points
250
Wild Thoughts

Wild Thoughts

Senior Member
Joined Mar 17, 2019
156 250
Mimi sitasahau kipindi nataka kuanza kidato cha kwanza, sasa kwenye maandalizi siunajua wengine familia zetu bilabila mzee hana kitu (hili labda sio tatizo maana hana)

Sasa mimi nilikua nina hela kdogo maana nlivomaliza darasa la saba kuna mwalimu nilikua namuuzia duka lake. Huyo mwalimu alikua anafundisha hisabati sasa mimi ndo nilikua nawanyoosha hilo somo, huyo mwalimu alikua ananikubali sana nlivo maliza tu akanipa kazi.

Sasa upuuzi nlofanya baada muda wa kuanza kidato cha kwanza kufika. Yule mwalimu alinilipa si nikachukua 10,000/= nikampa mshua akaninunulie kiatu(nilimpa maana alinambia town kuna viatu vizuri) zingine nkashona uniform na daftari nikabakiza elfu kumi tu ya ada.


Mshua hakununua kiatu ile hela sijui alifanyia nini? mi nikawa nmekaa tu siendi kuanza shule mara wiki ya kwanza ikaisha, ya pili hapo siwezi kumletea kibesi mshua arudishe hela au anipe kiatu.
Wiki ya tatu nikaona udwanzi huu sasa nikavaa uniform zangu nikavaa kiatu chake kilikua kikubwa kishenzi, hakinitoshi afu kibaya. Miaka 15 saivi imepita siwezi kusahau.

Hakuninunulia kiatu nilivaa lile lakuchumpa lake mpaka likaisha kidato cha pili.
 

Forum statistics

Threads 1,295,951
Members 498,495
Posts 31,228,868
Top