Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?


tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,346
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,346 2,000
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miaka 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kimaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
frem zero

frem zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Messages
574
Points
1,000
frem zero

frem zero

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2016
574 1,000
Mkuu hii ilikuwa iringa miaka hiyoo.
Hahahaaaa duh kumbe hisia zangu za kweli. Nilijua ni iringa maana huko kwa mabumunda ni balaa. Mie pia niliishi iringa kanisa langu lilikuwa rc mshindo. Ni kuna mabumunda hatari bila kusahau gubiti za kutosha
 
C

Credere Potest

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2016
Messages
218
Points
500
C

Credere Potest

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2016
218 500
Dah! Mimi najutia sana kwenda kusoma coz ya ajabu ajabu kweli UDOM...niliacha coz ya maana ya SUA Na Mzumbe nikakimbilia DOM..... Hilo jambo najutia hadi huu mda ninavyoandika hapa ....labda badae Mungu akinisaidia nitaacha kujutia.....
 
chopeko

chopeko

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
1,490
Points
1,500
chopeko

chopeko

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
1,490 1,500
Katika maisha yako huenda kuna kosa moja ulilotenda ambalo unajutia kulifanya na kama ungepewa nafasi usingerudia tena.

Mimi katika maisha yangu kosa kubwa nililotenda na ambalo nitalijutia katika maisha yangu yote ni kuchelewa kuanza shule. Nimeanza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 12 na kuhitmu darasa la saba nikiwa na umri wa miaka 19. Baada ya kuhitimu s/msingi nikakaa kwa muda wa miaka 6 kabla sijarudi shule tena na kurudia darasa la saba. Hapa nilikuwa na umri wa miak 25. Kwa bahati nzuri nikafaulu kwenda sekondari na kuanza kidato cha kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Bahati nzuri ni kwamba zamani hakukuwa na age sealing. Ingekuwa zama hizi nisingeruhusiwa kusoma shule. Namshukuru Mwalimu Nyerere kwa kuondoa ubaguzi wa kiumri kwenye elimu.

Nimesoma hivyo hivyo nikiwa babu hadi nimehitimu kidato cha sita. Kosa la pili ambalo nalijutia ni kusoma kozi ya ajabu ajabu ambayo haina tija wala mantiki ya kinaisha. Kama umri ungekuwa unaweza kurudishwa nyuma nikarudi kuwa mvulana kamwe nisingesoma kozi hii niliyosoma. Ningejitahidi nisomee udaktari au sheria.

Je, kuna kosa gani ulilotenda katika maisha yako ambalo litaendelea kukutesa maisha yako yote na ambalo usingependa kulirudia kama ungepewa nafasi ya kujisahihisha?
Nafikiri kosa la kuanza shule na umri mkubwa halikuwa kosa lako.Hilo ni la wazazi maana kuanza shule kwa ninavyoelewa mtoto hana maamuzi yoyote kwa familia zetu nyingi za kiafrika.!!
Kwa hiyo wala usilijutie mkuu!!
 
supermarket

supermarket

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Messages
7,205
Points
2,000
Age
32
supermarket

supermarket

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2016
7,205 2,000
Kujuta kwangu ni kama mzigo mzito ninao ubeba kichwani unanielemea, kila kitu kwangu ni changamoto nikiteleza narekebisha, nainuka na kuendendelea na safari
 

Forum statistics

Threads 1,295,973
Members 498,495
Posts 31,229,499
Top