Ni kosa gani alilolifanya Aboud Jumbe kustahili 'kifungo cha maisha'?

Hapana,

Mara baada ya Mzee Karume kuuwawa, nafasi yake ingechukulkiw na Mzee Thabiti Kombo kama ilikuwa ni swala la seniority, ila Mzee Kombo alikuwa na imani sana na utaifa ya Jamhuri ya Muungani na alijua kuwa nafasi ile ilitakiwa mtu aliyesoma kukaribiana na Nyerere kuliko yeye. Kwa hiyo akashauri nafasi hiyo apewe Jumbe, na kweli Jumbe aliifanya vizuri sana akiwa analenga kwenye utaifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya Zanzibar. Kama ulisikia ile hotuba ya Jumbe ya mwaka 1975 wakati wa uteuzi wa mgombea wa uraisi wa Tanzania wakati huo utakubaliana nami kuwa alikuwa na utaifa zaidi ya uzanzibari wakati huo. Jumbe aliipenda na aliifanya kazi yake ua umakamu wa Rais kwa ufanisi sana huenda kuliko makamu mweingine yeyote wa Rais katika historia ya Taifa hili. Wakati wa vita Uganda, Jumbe aliidhinisha hela kutoka akiba ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar, kwa ajili ya kununulia BM40 ambazo hatukuwa nazo wakati ule na Nyerere hakuwa na hela za kupata silaha hizo mara moja katika muda mfupi ule. Maamuzi yote yaliyokuwa yakifanyika na kuigusa Zanzibar wakati huo, yalikuwa hayatimii bila ridhaa ya Mzee Jumbe na Mzee Kombo. Mzee Jumbe alighafilika kidogo tu kutokana na kuchukia popularity ya Sokoine kufuatia vita ya uhujumu uchumi ya mwaka 1983, na ikawa ndiyo mporomoko wake wa moja kwa moja kisiasa.

Kichuguu,

Uliyazungumza mengi ni ukweli ila kuna tatizo moja umelisahau kulizungumza au kulisema. Nyerere alikuwa na influence na power mpaka visiwani na aliyekuwa na uwezo wa kupambana nae alikuwa ni Marehemu Karume peke yake. Alipofariki ndipo Nyerere alikuja akabadilisha baadhi ya vipengele wakati wa kuandika constitution ya Tanzania kuimeza Zanzibar. Haya yamezungumzwa na wanahistoria wengi nchini na nje ya nchi. Sasa unafikiri Thabit Kombo au Mzee Aboud Jumbe walikuwa na uwezo wa kumpinga maamuzi yake. Pesa za vita zilitoka lakini kwa shingo upande kwani zilikuwa ziende kufinance shughuli za maendeleo visiwani badala yake zikaenda kununua vifaa vya kijeshi. Hili liliwakera wengi ndio sababu ya rebellion by mzee Jumbe kutaka Zanzibar iwe inatambulika kama nchi ili iwe na uhuru wa kufanya maamuzi yake yenyewe pasina kuingiliwa au kulazimishwa na serikali ya muungano.
 
Mzee Jumbe hayupo kizuizini, anapata huduma zote kama kiongozi mstaafu wa nchi kwa nafasi aliyokuwa nayo. Ana ulinzi wa serikali, huduma za usafiri na mabo mengine. Kwa sasa huyu mzee umri umekwenda na hawezi kuhudhuria shughuli yenye usumbufu wa aina yeyote anahitaji muda mwingi wa kupunzika na kuangaliwa. Mimi nadhani wakati mwingine kabla ya kuanza kulalamikia jambo ni heri ungeuliza ili wenye taarifa waweze kukujulisha.

Hata mimi mleta uzi sikumuelewa vizuri, ni kifungo gani alichokua anakisema, Abdu Jumbe mimi ni jirani yangu kabisa hapa mjimwema, enzi hizo hiyo nyumba wakati inajengwa, Mjimwema kulikua kijijini kweli, nakumbuka enzi hizo, hadi mwaka 1990 alipokua anavuka na Patton pale Kigamboni wengine tulikua tunazuiliwa tusiingie, alikua anasafiri peke yake, miaka hiyo alikua akitumia Rand rover 110 then baadae akapewa Discovery then akawa na Nissan Patrol, nakumbuka hata Gazeti la Motomoto enzi hizo liliwahi kuhoji, kwanini huyu mtu alipwe na kutunzwa na Tanzania Bara? wakati hajawahi kuwa na wadhfa wowote huku. Gazeti lilidai (Wakati huo) kuwa huyu mzee alikua analikamua Taifa la Tanganyika jumla ya Tsh 42,000,000 kwa mwaka. Ikumbukwe pia, kwa historia yetu Bongo (Sina hakika na nchi zingine) mtu aliyewahi kuwa Rais, mara baada ya kutoka/kuachia madaraka, hua hajishighulishi tena na Siasa zaidi ya ushauri tu, nani anamkumbuka Marehem Abdul Wakili, mara baada ya kuondoka marakani, wapi aliwahi kusikika tena, tuache uzushi.

Kuhusu Ubabe aliotumia Mwl thidhi ya Jumbe, nachoweza kusema, kwa wakati ule, ilikua ni vizuri Zanzibar kuwa chini ya himaya yetu, msimamo wa Mwl. Nyerere juu ya mataifa mengine yaliokua bado hajapata uhuru, kila mtu humu anafahamu, tulikua na maadui wengi sana, nchi kama Afrika Kusini ilikua adui yetu mkubwa sana, wa umri wangu wanakumbuka jinsi mpaka wa Malawi ulivyokua ukitumika kuwapitisha wapelelezi wa Kikaburu enzi hizo, usalama wa taifa enzi hizo wakua wakifanya kazi hasa, sio leo, nadhani kwasasa hata jina la Usalama wa Taifa haliwafai, tungewaita usalama wa ccm, hivi kwa mfano Zanzibar ingejitegemea wakati ule, si kangekua ndio kangome ka maadui zetu? Kama leo tu kanataka kufanana na Al Shaabab, what about those times, kwahili na kwa wakati ule, Nyerere he was very right.
 
Tafuta filamu ya Jumong. Angalia jinsi Haemosu,baba mzazi wa Jumong, alivyofungwa gereza la siri lenye giza totoro na ulinzi mkali. Utaelewa tu
 
Amekuja kuonekana in Public siku aliyofariki mwanae ndio mara mwisho zifa zote za kitaifa haalikwi muulize mbona kuna makada wa CCM kama akina Kingunge juu ya utu uzima wao wanaalikwa.
Mdondoaji,

..inawezekana Mzee Aboud Jumbe hataki kushiriki shughuli zozote zile za kisiasa/kiserikali.

..niliwahi kusoma kwenye magazeti kwamba Mzee Jumbe ameacha wosia kwamba akifariki asizikwe kwa heshima za kiserikali na kijeshi kama inavyofanyika kwa viongozi wengine wakuu.
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama Mzee A.Jumbe yuko kifungoni! yuko huru kabisa na hata juzi juzi alipelekwa India kwa matibabu na mtoto wake mmoja kufariki huko akiwa anamtibu Baba yake!

Mzee Jumbe kwa sasa ni Mzee sana na afya yake imedhoofika sana tokana na umri! kwa umri ni mkubwa hata kuliko Mzee Nelson Mandela! na kwa sasa hata akialikwa ktk hafla za kitaifa itakuwa vigumu sana kuhudhuria!

Bi Zubeda hapo kwenye bold na italics naomba kusahihisha. Mzee Jumbe alizaliwa 1920 (soma kitabu the Partnership), Mzee Mandela alizaliwa 1918!

That makes him two years younger than Mandela. Lakini ni kweli hali yake kiafya imedhoofika kwa umri.
 
wewe uliona wapi mtu na akili zake ana sema moja jumlisha moja unapata ndatu? hilo kosa tena ukiwa ni mtu mzima na sio mtoto wa miaka 2
 
Kweli wakuu tumekumbushana historia hii ambayo huwa haisemwi kinagaubaga. Ila bado nina shida na kutambuliwa kwa Mzee Abdul Jumbe, hasemwi wala kuandikwa katika historia ya siasa ya nchi hii!
 
Ebu fafanua hapo kwenye Nyekundu, mwaka gani hiyo Historia, Maana tokea hii mipaka ya Africa iwekwe haijawai kubadilishwa au una-undugu na Museveni wa Uganda anaye dai kisiwa cha Kenya kuwa chake.

Arafat ni aibu kwako wewe kama mwananchi kutojua historia ya nchi hii. Hivi hujui kwamba 10 miles coast (kuanzia Kismayuu Somalia mpaka Msumbiji) ilikuwa chini ya utawala wa Zanzibar?

Mkataba huu ulibadilishwa wakati wa negotiations za uhuru wa Kenya na Tanganyika, na ndiyo Muingereza akaweka hilo kama sharti la kutoa uhuru.
 
Hivi sasa ni karibu miaka 25 tangu Abdu Jumbe awekwe kwenye kifungo cha nyumbani kutokana na kile kilichohitwa kuchafua hewa ya siasa huko visiwani. Katika kipindi hicho baadhi ya wale walikuwa katika mstali wa mbele katia kumchongea Jumbe kwa Nyerere, ikiwemo Shariff ahmad na Ahmad Rashid walikuja kutemwa katika CCM na kuwekwa lupango kwa miaka kadhaa. Hivi sasa baada yakushikishwa adabu wajisalimisha kwa CCM. Hata hivyo ukiwasikiliza kwa mbali, wanataka katiba ya sasa ya serikali ya muungano ifanyiwe marekebisho ili tuwe na mfumo wa shirikisho. Hoja hiyo ndiyo iliyomuweka Jumbe korokoroni. Sasa, iwapo hoja hiyo hivi sasa inazungumzika kwanini mzee wetu huyo hasiachiwe huru na kurejeshewa haki zake zote kama rais wa Zanzibar na makamu wa rais wa Tanzania?

kosa lile lile kudai zanzibar huru.....huuu ndio ukweli....
 
What is excatly the title of that book? and where can I possibly find?

Yes, aliandika kitabu titled "The Partnership: Tanganyika-Zanzibar Partnership: 30 Years Turbulent Years" (The partner-ship: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar : miaka 30 ya dhoruba - Swahili Edition) kilichochapishwa mwaka 1994, miaka 10 baada ya kujiuzulu wadhifa wake.

Katika kitabu hicho anadai kuwa Zanzibar haijawahi kunufaika na Muungano. Anasema kuwa haelewi ni kwa nini Tanzania bado inaendelea kusisitiza muungano wa sasa na kukataa kuwa na muungano wa serikali tatu pamoja na kuwa watu wengi wanataka Muungano wa sasa ufanyiwe marekebisho

Kwenye hotuba yake ya Januari 1998 ya kuadhimisha sherehe za 34 za Mapinduzi ya Zanzibar Jumbe alisema: "Sielewi ni kwa nini serikali inang'ang'ania kuwa na Muungano wa sasa, lakini ninahisi ni kwa sababu zile zile ambazo zimefanya kitabu changu, The Partnership, kikataliwe wakati wote wa kipindi cha mfumo wa chama kimoja."

Akasema kama Muungano una faida yoyote, na kama unao Tanganyika na wala siyo Zanzibar, ndiyo itakuwa imenufaika, "mwulize Nyerere kwa sababu yeye ndiye aliyekwenda Zanzibar. Yeye ndiye aliyetaka Muungano. Lazima alikuwa na malengo. Amefanikisha hayo malengo? Siwezi kuongea kwa niaba ya Watanganyika juu ya malengo ya Muungano."
 
Kichuguu,

Uliyazungumza mengi ni ukweli ila kuna tatizo moja umelisahau kulizungumza au kulisema. Nyerere alikuwa na influence na power mpaka visiwani na aliyekuwa na uwezo wa kupambana nae alikuwa ni Marehemu Karume peke yake. Alipofariki ndipo Nyerere alikuja akabadilisha baadhi ya vipengele wakati wa kuandika constitution ya Tanzania kuimeza Zanzibar. Haya yamezungumzwa na wanahistoria wengi nchini na nje ya nchi. Sasa unafikiri Thabit Kombo au Mzee Aboud Jumbe walikuwa na uwezo wa kumpinga maamuzi yake. Pesa za vita zilitoka lakini kwa shingo upande kwani zilikuwa ziende kufinance shughuli za maendeleo visiwani badala yake zikaenda kununua vifaa vya kijeshi. Hili liliwakera wengi ndio sababu ya rebellion by mzee Jumbe kutaka Zanzibar iwe inatambulika kama nchi ili iwe na uhuru wa kufanya maamuzi yake yenyewe pasina kuingiliwa au kulazimishwa na serikali ya muungano.

nguvu za Mwl kama zilivyo elezwa na Hassan Nassoro MoyoKarume alimweleza Nyerere matatizo ya Muungano, lakini hayakujadiliwa

WAKATI mjadala kuhusu muundo gani unafaa katika Muungano ukiendelea, imefahamika kwamba matatizo ya Muungano yalionekana tangu 1970, lakini hayakupatiwa ufumbuzi.

RAI imeelezwa kuwa, ingawa Mzee Abeid Amani Karume (sasa marehemu), alijitahidi kumweleza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuhusu matatizo kadhaa ndani ya Muungano, la
kini alijibiwa kuwa huo haukuwa wakati muafaka wa kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo.

Waziri wa kwanza wa Sheria katika Serikali ya Muungano, Hassan Nassor Moyo, ameiambia RAI kuwa Mzee Karume alibaini kasoro kwenye mambo matano na kutaka yaondolewe kwenye Muungano.

Akizungumza na RAI katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni nyumbani kwake Fuoni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Mzee Moyo aliyataja mambo hayo kuwa ni suala la kutangaza hali ya hatari, jeshi, ulinzi, polisi na mambo ya nje.

Mzee Moyo, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, alisema, Mzee Karume alianza kuona Muungano hausimami kama yalivyokuwa makubaliano yao hasa kwenye suala la vita.

Kwa mujibu wa Mzee Moyo,
jambo moja lililomtia hofu Mzee Karume, ni pale alipogundua kuwa Mwalimu Nyerere amepeleka jeshi nchini Msumbiji kusaidia harakati za ukombozi, huku Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar akiwa hana taarifa.

Mzee Moyo alisema tukio hilo lilisababisha wananchi wa Zanzibar kumlalamikia Mzee Karume, wakihoji iweje watoto wao wapelekwe kwenye vita kimya kimya, na kumtaka atoe maelezo ya kina.

“Baada ya kuona mambo hayaendi sawa, Karume aliitisha kikao cha Baraza la Mapinduzi, wakati huo Mzee Jumbe akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, na tukaamua kupeleka waraka rasmi kwa Baraza la Mawaziri, tukitaka mabadiliko katika Muungano.

“Mwalimu alipoupata waraka ule, akaitisha mkutano wa pamoja kati ya Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawaziri,
na katika mkutano ule, wajumbe wote tukiwa tumenuniana, hakuna aliyetaka kunywa hata chai, ndipo Mzee Jumbe akasoma ule waraka.

“
Mwalimu akamgeukia Mzee Karume na kumuhoji, hivi ndivyo mnavyotaka? Mzee Karume akamjibu waulize wanaume hao.

“
Tukaulizwa sisi wajumbe wa Baraza la Mapinduzi mara tatu, na wote kwa pamoja tukajibu, ndivyo tunavyotaka. Baada ya hapo akarejea kwa Karume na kumweleza, Sheikh Karume kama ndivyo hivyo mnavyotaka, basi wakati wake bado.

“Baada ya kusikia hivyo,
Mzee Karume alijibu kwamba ikiwa wakati wake bado, basi karatasi zote hizi za mabadiliko zibaki huku Bara,” alisema Mzee Moyo akirejea kauli za majibizano katika kikao hicho cha 1970.

Wiki iliyopita, Rai ilimnukuu Katibu Mkuu wa pili wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Makame Mzee Suleiman (87), akipinga kauli ya baadhi ya viongozi kwamba Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, alilazimishwa na Mwalimu Julius Nyerere kukubali kuunda Muunganga.

Alisema anawashangaa baadhi ya wanasiasa ambao wanalaumu kwamba Wazanzibari hawakushirikishwa kuamua suala la Muungano. Amesema ukweli ni kwamba wananchi wa Zanzibar, walishiriki katika kila hatua ya mchakato wa Muungano.

Alisema kabla ya hatua yoyote ile kufanyika, M
zee Karume hakufanya maamuzi peke yake, bali aliwauliza kwanza wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, iwapo wanaridhia kuwapo kwa Muungano au la.

“Mimi nikiwa Katibu,
Mzee Karume alituita mmoja mmoja pale nyumbani kwake Maisara, na alituhoji mara tatu. Je, mnautaka Muungano, wote tukakubaliana tunautaka.

“
Baada ya hapo akaitisha mkutano mkubwa wa hadhara pale kwenye Viwanja vya Maisara na kuwahoji wananchi, Je, mnautaka Muungano, wananchi wakajibu ndio tunautaka.

“
Karume hakuishia hapo, akafanya ziara katika matawi yote ya chama mjini na vijijini, na kuwahoji wanachama. Je, mnautaka Muungano, wakajibu ndio tunautaka,” alisisitiza, Mzee Makame.

Kwa mujibu wa
Mzee Makame, Hati ya Muungano ilisainiwa Aprili 22, 1964, na Aprili 26, 1964, viongozi hao walibadilishana hati hiyo iliyoridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BMZ), kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Na makubaliano yote yalikuwa kwenye maandishi, lakini sio kweli kama watu wanavyolaumu kwamba wananchi hawakushirikishwa kwenye mchakato mzima wa Muungano,” alisema.

Kasoro za kuasisi Muungano:

Mzee Moyo alisema kasoro kubwa iliyojitokeza kwenye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Jaji Wolfgang Dourado (sasa marehemu), kutoonyeshwa hati ya Muungano.

Alisema Muungano ulifanyika kwa moyo wa kuaminiana na Zanzibar ikaacha kuipeleka Hati ya Muungano ndani ya Baraza la Mapinduzi, kwa ajili kujadiliwa na kupitishwa kikatiba na hatimaye kuwa sheria.

“Wenzetu walipeleka hati katika Bunge la Tanganyika, ili kuipitishwa kikatiba na ifanywe sheria, sisi hatukufanya hivyo mpaka hii leo, tulikwenda kindugu zaidi na sio kisheria.

“Cha kuchekesha sheria ile iliyokuwa ipitishwe na Baraza la Mapinduzi kama wenzetu, imesainiwa na Mzungu wa Serikali ya Tanganyika akiitwa Solicitor General. Hili ni kosa kubwa,” alisema Mzee Moyo.

Baraza la Mapinduzi lilihoji:

Mzee Moyo alisema baadhi ya wajumbe wa Baraza la Mapinduzi walihoji hatima ya Zanzibar katika Muungano huo na kushauri kwamba waulizwe kwanza wanasheria, kabla ya kuungana.

“Mwenzetu mmoja, Khamis Abdallah Ameir, alimuuliza Mzee Karume, mbona jambo hili limekuja ghafla, ni bora tuulize wanasheria, akajibu kama hamtaki nitamleta mwenyewe Nyerere.

“Sisi tulihoji ardhi yetu itakuweaje, Mzee Karume akasema hayo yatakuwa mambo yetu wenyewe. Tulikuwa tunamheshimu sana Mzee Karume na akisema kitu huwezi kupinga,” anasema Mzee Moyo.

Vurugu zinazojitokeza:

Akizungumzia vurugu zilizojitokeza hivi karibuni Zanzibar zinazohusishwa na kero za Muungano, Mzee Moyo alisema tatizo kubwa ni viongozi wa kisiasa kuwa na misimamo yao ya kisiasa na kusahau kwamba Muungano huo haukuletwa na vyama vyao.

“Muungano huo haukuletwa na vyama, uliletwa na Serikali ya Tanganyika na Zanzibar. ASP haikuulizwa, walielezwa kwanza Serikali, Mzee Karume alikuja kuzungumza na wanachama wakati tayari ametia saini.

“Na yote haya yalifanyika kwa sababu tulikuwa tunaaminiana, lakini leo tumesahau lengo la Muungano, tunakwenda zaidi katika siasa za vyama, tuzungumze katika sura ya Wazanzibar na Watanganyika namna Muungano ulivyoasisiwa.”

Mzee Moyo alibainisha kuwa, kasoro zilizojitokeza 1970 chini ya Mzee Karume, ndizo hizo hizo zinapigiwa kelele na wananchi hivi sasa, na kusisitiza kuwa wakati umefika wa kasoro hizo kuwekwa mezani hivi ili zijadiliwe
 
... mwenye kutafuta hachoki na akichoka' elewa kaishapata "wengi hatujui historia ya nchi yetu" mimi mwenyewe nilikuwa natafuta historia ya huyu Mzee Jumbe, nipo nikakutana na hii thread.
Imenisaidia kiasi fulani' ninaomba wanaJF wanaofahamu mambo yalivyokuwa wakati huo na sasa watujuze zaidi.
 
Mzee Jumbe hayupo kizuizini, anapata huduma zote kama kiongozi mstaafu wa nchi kwa nafasi aliyokuwa nayo. Ana ulinzi wa serikali, huduma za usafiri na mabo mengine. Kwa sasa huyu mzee umri umekwenda na hawezi kuhudhuria shughuli yenye usumbufu wa aina yeyote anahitaji muda mwingi wa kupunzika na kuangaliwa. Mimi nadhani wakati mwingine kabla ya kuanza kulalamikia jambo ni heri ungeuliza ili wenye taarifa waweze kukujulisha.

Tunazungumzia sasahivi na kabla
 
Abdu Jumbe yupo hai kwa wale serengeti boys anaishi dar ila ni mzee sana
 
Ni suali gumu unalotaka kulipa majibu mepesi, Ukweli ukitaka kuujua nenda kwa mzee mwenyewe anaongea vizuri. Itoshe kusema alikuwa na mtazamo tofauti na Mwl. Nyerere juu ya mahusiano ya nchi hizi mbili zilizoungana. Sio Seif na Rashid tu bali wazanzibar wote inapofika kwenye hili suala la Mzee Jumbe hawasomeki kirahisi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom