Mdondoaji,
..hata Mzee Mwinyi naye kajibanza huku Tanganyika "analima" maembe.
..Sheikh Idiris Abdul Wakil Nombe naye alikuwa kajinafasi Ilala-Bungoni.
..Maalim Seif naye inasemekana alikuwa akiishi hotelini hapa DSM. sijui kama ni kweli.
..Hamad Rashid Mohamed naye anaishi Tanganyika akifanya biashara ya vyuma chakavu.
..Zanzibar itajengwa na nani kama watu kama hawa hawataki kwenda kuishi huko?
Mkuu,
Mzee Mwinyi anaishi pale Mikocheni ila kila baada ya wiki mbili anaenda zake zanzibar na ana nyumba zake kule anafikia .
Seif Sharif Hamad sijui,
Hamad Rashid ana biashara zake huku inaeleweka kwanini anapendelea kuishi huku.
Ila mkuu Mzee we Aboud Jumbe ni mzaliwa haswa wa zanzibar na hana biashara huku wala nini. Anakaa mahali nyumba ilikuwa katika hali mbaya sana kabla Mh. Mkapa kwa huruma akaenda kuokoa jahazi. Wanawe wengi wako hali mbaya sijui yule aliyekuwa akisome ukapteni wa ndege yuko wapi. Kuna siri inaendelea na pia kwanini yuko Dar wakati yeye alikuwa Rais wa Zanzibar.
Idriss Abdul Wakil sijui mkuu ila nadhani alikuwa anaishi Zanzibar na tumemzika Zanzibar ila hilo la Dar silijui.