Ni kosa gani alilolifanya Aboud Jumbe kustahili 'kifungo cha maisha'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kosa gani alilolifanya Aboud Jumbe kustahili 'kifungo cha maisha'?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Kadudu, Sep 5, 2009.

 1. K

  Kadudu Member

  #1
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani huyu mheshimiwa yuko wapi? Mbona kimya.

  Hata hashirikishwi kwenye issue za CCM kulikoni?

  KAWAWA sometimes huwa anashirikishwa why not JUMBE? Or is there any wrong doings alizofanya au he is SICK?
   
 2. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukiona hivyo hana umuhimu kwenye mambo yao!! Maana chama cha kijani chaangalia interest kama huna lako halipo.

  Kwa Mzee Kawawa huwa wanaenda wakitaka sifa lakini hawamtumii kwa ushauri wala chochote.
   
 3. Ndanda to Lomwe

  Ndanda to Lomwe Member

  #3
  Sep 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee yuko nyumbani kwake Kigamboni,anahudumiwa kama kawaida ya wastahaafu,walinzi na matibabu na Serikali ya Jamhuri,anaugua muda mrefu sana prostate cancer na Zaidi anasumbuliwa sana na macho,nadhani hata haoni kabisa.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Chama cha mafisadi hawana utamaduni wa kuenzi historia yao iliyo sahihi; hasa watu waliokitumikia chama hicho wakati ambao kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi.!!

  Ndio maana huwezi kuwasiklia watu kama Mwakawago, Gama na hata Mang'ulla ambao walikiongoza chama kwa muda mrefu, wakishirikishwa kwenye mambo ya CCM -Mtandao- Mafisadi!!
   
 5. S

  Simoni Member

  #5
  Sep 5, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  UBINAFSI, UBINAFSI, UBINAFSI. It is a frankestein syndrome. It is a monster that nowa its creator cannot control it. Ndiyo maana kinawatafuna hata wenye chama chao.

  Akina Mangula na Mwakawago wasilie kwani na wao waliwafanya hivyo hivyo watangulizi wao. Hiyo ni laana. Laana Laana
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Kwa kweli sijamuona huyu Mkuu muda mrefu sana...hata kwenye makutano ya Kitaifa.....Namtakia kila kheri
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Yuko Kigamboni.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Nyerere hajamwita akaenda?
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu, katika viongozi tulionao sasa, ikiwa ni pamoja na wale walioko hivi ofisini na wale ambao tayari wamestahafu hakuna yeyote kati yao aliyetoa mchango mkubwa katika ustawi wa nchi yetu kama Aboud Jumbe.

  Yeye ndiye aliyeipa Zanzibar katiba ya mwaka 1984. Kabla ya hapo, wananchi wa kawaida hawakuwa na sauti yeyote katika uendeshaji wa sauti yao. Madaraka yote ya kutunga sheria yalikuwa mikononi mwa Baraza la Mapinduzi ambalo wajumbe wake walikuwa wanateuliwa moja kwa moja na rais mwenyewe. Katiba hiyo ya mwaka 1984 ndiyo iliyoanzisha Baraza lawawakilishi.

  Aidha bila ya Aboud Jumbe kuridhia kuunganisha ASP na TANU, CCM ambayo hivi sasa vigogo wengi wanajivunia hisingelizaliwa.

  Katika hali hiyo, inakuwa vigumu kuelewa ni kwa namna gani mtu kama huyo, aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi ya yetu anavyoweza akaachwa kando na huku tukamtanguliza mtu ambaye japo amekuwa madarakani, lakini mchango wake ni ni wakutilia shaka.
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa ni karibu miaka 25 tangu Abdu Jumbe awekwe kwenye kifungo cha nyumbani kutokana na kile kilichohitwa kuchafua hewa ya siasa huko visiwani.

  Katika kipindi hicho baadhi ya wale walikuwa katika mstali wa mbele katia kumchongea Jumbe kwa Nyerere, ikiwemo Shariff ahmad na Ahmad Rashid walikuja kutemwa katika CCM na kuwekwa lupango kwa miaka kadhaa.

  Hivi sasa baada ya kushikishwa adabu wajisalimisha kwa CCM. Hata hivyo ukiwasikiliza kwa mbali, wanataka katiba ya sasa ya serikali ya muungano ifanyiwe marekebisho ili tuwe na mfumo wa shirikisho. Hoja hiyo ndiyo iliyomuweka Jumbe korokoroni.

  Sasa, iwapo hoja hiyo hivi sasa inazungumzika kwanini mzee wetu huyo asiachiwe huru na kurejeshewa haki zake zote kama rais wa Zanzibar na makamu wa rais wa Tanzania?
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mapema mwaka 1984 aliyekuwa rais wa Zanzibar, makamu wa kwanza wa rais wa Tanzania, na makamu mwenyekiti wa CCM Al Haji Abdu Jumbe alihenguliwa kwenye nyadhifa zote hizo na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani, kwa kile kilichohitwa kuchafua hali ya kisiasa nchini.

  Ikumbukwe katika viongozi tulio nao sasa hakuna kama Jumbe; yeye ndiye aliyeanzisha tena mfumo wa uwakilishi baada yakufutwa kufuatia mapinduzi ya 1964, na vile vile yeye ndiye aliyeridhia muungano wa ASP na TANU uliozaa CCM. Inavyosemekana kosa, alilofanya Jumbe ni kuwa na dhamira ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kwa lengo la kuanzishwa hapa nchini mfumo wa shirisho badala ya serikali mbili.

  Kwakuwa hivi sasa suala hilo linazungumzika, ingelikuwa vyema mzee wetu huyo akaachiwa na kupewa marupurupu na heshima zote anazostahili ili aweze kutoa mchango wake katika mjadala wa katiba mpya unao tarajiwa hivi karibuni.
   
 12. K

  Kivia JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kila jambo na wakati. Mfano, siku za nyuma ilikuwa kosa kubwa kuhoji katiba lakini leo hii tunaongea mabadiliko ya katiba hapa tz. Mzee wetu sheikh Aboud jumbe yupo huru na anapata stahiki zake zote[tumuombee afya mzee wetu huyu kwani umri nao umeenda]
   
 13. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kweli katika hili Watanzania tusimame, tusitekeleze kila alichofanya Nyerere, kiukweli Ndugu Jumbe, hatendewi haki kwa kuhifadhiwa hapo Kigamboni.

  hapewi heshima ya kama mmoja wa maraisi wa Zanzibar, hashirikishwi kwenye hafla zozote, kwanini hawa wazanzibar hawaoni umuhimu wa mtu wao.

  Imetosha sasa, Jumbe atolewe kizuizini.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Byendangwero

  Mkuu unasahau watu waliomchomea utambi mpaka sasa wapo madarakani ijapokuwa wamestaafu na wakimuachia na kumlipa marupurupu yake yote ana siri nyingi ndio maana wamemtupa kule kigamboni hoping atafia na siri zake moyoni.
   
 15. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama Mzee A.Jumbe yuko kifungoni! yuko huru kabisa na hata juzi juzi alipelekwa India kwa matibabu na mtoto wake mmoja kufariki huko akiwa anamtibu Baba yake!

  Mzee Jumbe kwa sasa ni Mzee sana na afya yake imedhoofika sana tokana na umri! kwa umri ni mkubwa hata kuliko Mzee Nelson Mandela! na kwa sasa hata akialikwa ktk hafla za kitaifa itakuwa vigumu sana kuhudhuria!

  Mzee wetu k huyu baada ya kudhalilishwa na JK Nyerere, aliamua kuachana na siasa kabisa na alichokuwa akifanya ni ibada na kuomba toba kwa Mola wake na kuwa msoma dua muhimu ktk kongamano za kiislamu kama vile Kikundi muhimu cha Kiislamu cha TABLIGH FII SABILILLAH chenye makao yake makuu Kiwalani Dar-es-salaam!

  Tabligh ni kitengo muhimu sana cha Kiislamu chenye jukumu la kuitangaza na kueneza ujumbe maalum alioteremshiwa Mtume Mtukufu Muhammad(SAW) kwa binaadamu wote hapa duniani!

  Mzee Jumbe umri wake umekwenda sana na ni Mola peke yake anaejua ni lini atapokea roho yake lakini kwa hakika Mzee Jumbe kwa sasa anaishi maisha mazuri ya furaha na amani zaidi kuliko wakati alipokuwa Rais! kwa sababu yuko karibu zaidi na Wananchi wa Kawaida kuliko huko nyuma !
   
 16. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli amekwisha rejeshwa kundini mbona jina lake halitajwi tajwi, wakati kwa maoni yangu amechangia sana kuliko yeyote yule kuirejesha Zanzibar kwenye utawala wa kisheria.
   
 17. V

  Vumbi Senior Member

  #17
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mzee Jumbe hayupo kizuizini, anapata huduma zote kama kiongozi mstaafu wa nchi kwa nafasi aliyokuwa nayo.

  Ana ulinzi wa serikali, huduma za usafiri na mabo mengine. Kwa sasa huyu mzee umri umekwenda na hawezi kuhudhuria shughuli yenye usumbufu wa aina yeyote anahitaji muda mwingi wa kupunzika na kuangaliwa.

  Mimi nadhani wakati mwingine kabla ya kuanza kulalamikia jambo ni heri ungeuliza ili wenye taarifa waweze kukujulisha.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Feb 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,789
  Likes Received: 5,049
  Trophy Points: 280
  ..kwanini haendi kupumzikia Zanzibar?

  ..Nyerere kaondoka madarakani muda mrefu sana, lakini Mzee Jumbe kajichimbia hapohapo Mjimwema hataki kurudi kwao.
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Swali zuri sana labda wale watetezi wa kusema huyu mzee yupo huru watujuze!
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Feb 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,789
  Likes Received: 5,049
  Trophy Points: 280
  Mdondoaji,

  ..hata Mzee Mwinyi naye kajibanza huku Tanganyika "analima" maembe.

  ..Sheikh Idiris Abdul Wakil Nombe naye alikuwa kajinafasi Ilala-Bungoni.

  ..Maalim Seif naye inasemekana alikuwa akiishi hotelini hapa DSM. sijui kama ni kweli.

  ..Hamad Rashid Mohamed naye anaishi Tanganyika akifanya biashara ya vyuma chakavu.

  ..Zanzibar itajengwa na nani kama watu kama hawa hawataki kwenda kuishi huko?
   
Loading...