Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,859
- 1,301
Nilimsikia itv jana usiku akitetea muswada mbovu. Kweli sikuamini kama yule ni jaji. Nitatoa machache aliyosema:
Alipoulizwa kuhusu kwanini mswada unazuia suala la muungano na mengine yasiongelewe alisema: si kweli kuwa imezuiliwa kuaongelea na akapiga bla bla nyingi za kisiasa lakini mwishoni akasema, muswada utakaporudi utakuwa na marekebisho kwa kuongeza kifungu kidogo cha tatu (sec 9(3) ambacho kitaruhusu mambo yote hayo kuongelewa. Kama muswada wa sasa unaruhusu yaongelewe kwa nini aje na marekebisho ya kuongeza hicho kifungu kidogo? Eti huyo ni jaji!
Kwenye sehemu ya sita inayohusu referendum (kura ya maoni) alisema vifungu vya adhabu vimewekwa ili kudhibiti watu wanaoweza kufanya uhuni katika mikutano kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai....
Hapa kuna maswala mawili - kwamba kuvuruga kwenye mkutano halali ni kosa la jinai ni sawa; na tayari kuna sheria inayoshughulikia watu wa aina hiyo; penal code inajitosheleza katika hili.
Pili ni kwamba Werema ametueleza uongo wa wazi. Kifungu cha 28(2) kinasema " For the purposes of paragraph (c) of subsection (1), the referendum campaign shall be conducted by the Commission and no political party or affiliate organization to a politcal party shall participate in the campaign" na
kifungu 28(3) kinasema "A person who contravenes the provisions of subsection (2) commits an offence and shall on conviction be liable to imprisonment, without fine, for a term not exceeding two years"
Jaji anatueleza kuwa kifungu hiki kimewekwa kudhibiti watakaofanya vurugu kwenye kampeni! wakati ukweli ni kuwa kifungu hiki kinawazuia vyama vya siasa kufanya kampeni, isipokwa tume peke yake ambayo ndiyo itakuwa imeandaa katiba.
Tatizo la Werema ni kuchanganya utaalamu na siasa na hivyo kujikuta siasa imemfunga macho na ubongo. Siamini kama jaji anaweza kusema aliyosema kwenye TV.
Hivi si kuna chama cha majaji? Hatuwezi kupetition huko wakamvua huo ujaji maana hakika amewadhalilisha majaji na taaluma yao.