SoC03 Ni kizazi cha vijana au kukomaa kwa akili za vijana

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Vijana wetu siku hizi wametekwa nyara na tamaduni za kila upande wa dunia na kuiga kila kinachotokea huko kwingine kuanzia mavazi ,matendo mpaka fikra na mwelekeo wa kimaisha kiasi kwamba hakuna mwenye Habari na kuenzi tamaduni zake wala kuzijua kabisa,vijana wamekuwa wapinzani wa kila lisiloafikiana na mawazo yao ya kimagharibi.

Hebu tutazame changamoto zinazoletwa na zama hizi.

Imamu Hasan Ibn Ali Ibn Abu Talib alisema “HAKIKA LEO NYINYI NI VIJANA WA TAIFA, NA KESHO MTAKUWA VIONGOZI WA UMMA, HIVYO, INAKUWAJIBIKIENI JUU YENU KUTAFUTA ELIMU.ILI KWAMBA KAMA HUWEZI KUYAHIFADHI YALE YOTE UNAYOJIFUNZA, BASI LAZIMA UYAANDIKE NA KUYATUNZA ILI BAADAE UWEZE KUYAREJEA (WAKATI UKIYAHITAJI)”.Biharul Anwar .J.2 ukurasa wa 132.Hadithi 37

Hivyo muhimu kwa vijana kusoma na kupata ujuzi wa kupambanua baina ya jema na ovu , na ili waje wawe viongozi wazuri na sio wasanii na waigizaji wa mambo ya hovyo ya nchi za magharibi.

Kila kizazi kina wajibu juu ya mwongozo wa kizazi kinachofuatia
-hususani wale watu wanaotambulika rasmi kama ndio viongozi wa jamii-wao wana wajibu mkubwa zaidi ,pia wanapaswa kuzingatia kutatua changamoto za leo kwa ufanisi bila kuiga yaliyofanyika jana .

Jambo la uongozi na mwongozo wa kizazi hiki unatofautiana katika njia na mbinu zake mwote katika vipindi mbalimbali vya nyakati na unatofautiana kulingana na vikundi au watu ambao tunashughulika nao. Hivyo ni lazima tuiondoe kabisa akilini mwetu, lile wazo kwamba hiki kizazi kipya lazima tuliondoe kabisa akilini mwetu, lile wazo kwamba hiki kizazi kipya lazima kiongozwe kwa kufuata njia zilizotumiwa na vizazi villivyopita .’’

Ni lazima nieleze hapa kwamba ,wakati tunapotumia msemo huu “kizazi cha vijana,”nia yetu sio kuainisha kiwango au umri wa vijana ,bali nia hasa ni kuwasilisha na kile kiwango au kundi la watu ambao,kutokana na athari za masomo yao wenyewe na uzoefu wa ustaarabu huu mpya ,wamekuza njia mahususi ya fikra na akili – iwe watu hawa watokee kuwa watu wazima au vijana.

Hata hivyo wengi wa watu hawa wanatokana na kizazi cha machipukizi, na ni kwasababu hii ndio maana tunakiita kizazii cha machipukizi, na ni kwasababu hii kwamba nakitaja kama “kizazi cha vijana” , ambapo tunaona kwamba kunakuwepo pia na idadi kubwa ya “watu wazima” ambayo wanayo namna hii mpya ya jinsi ya kufikiri, na wapo pia “vijana “ wengi ambao muundo waoo wa fikra na Imani zao zinafanana na zile za vizazi vilivyopita

Kwa hali yoyote ile kusudi ni kuzungumza kulingana na lile kundi la watu ambao wana mtindo huu mahsusi wa fikra -jambo ambalo linaongezeka siku hadi siku. Huu ni mtindo wa fikra ambao watu wazima na vijana ,wote wanaanza kuwa nao na huko baadae ,na Mwenyezimungu aepushie mbali ,kama itakosekana njia sahihi na taratibu za kuongoza na kuelekeza kizazi hiki zitakuwa hazitumiki ,basi tutakosa udhibiti kamili wa vizazi vya baadae.

Jambo hili ni jambo la muhimu sana katika nchi yetu ya Tanzania -na hata katika nchi nyingine yeyote ambako nalo bado ni jambo muhimu. Hata hivyo baadhi ya nchi walitambua jambo hili mapema kuliko tunavyopasa kufanya sisi na hivyo waliliweka mbele jambo hili kwa umakini sana ,ambako sisi kwa sasa limeanza kututatiza na kia uchao tunatafuta muarobaini.

Hiki kizazi chipukizi ni kizazi tu cha watu ambao wamejipumbaza wenyewe na ambao wanaabudu tu tamaa zao duni.

Tunadhani kwamba wakati wakizungumza nasi ,tunaweza kuwafinyia nyuso,mizaha,au kukimbilia kuwalaani na kuongea mambo mabaya kwao.Tunadhani kwamba tunaweza kuwaambia na halafu kila kitu kitakuwa sawasawa .Tunadhani kwamba tunaweza kuwashangaa na kuwapigia mayowe .Yote hay ani maneno ya kujiliwaza tu ambayo tunayasema nay apo pale tu kwaajili ya kutubakisha kwenye usingizi wetu na kutuzuia kufikiri hasa kuhusu namna nan jia bora ya kuchukua .Ndani ya kitambo kidogo,tutaamka na kutambua kwamba sasa tumechelewa sana kurudi nyuma.


NI NINI AMBACHO LAZIMA KIFANYIKE?

1. Ni lazima tuziimarishe Imani katika vichwa vyetu wenyewe kwamba uongozi na mwongozo wa kizazi hiki ni tofauti katika utaratibu na mbinu zake ,wote katika vipindi mbalimbali vya nyakati. Hivyo,ni lazima tuondoe kabisa yale mawazo kutoka vichwani mwetu ,kwamba kizazi hiki kipya lazima kiongozwe kwa kufuata zile taratibu zilizotumiwa na vizazi vlivyotangulia.

2. Lengo la umakinikaji ni kwamba ni lazima kwanza tutambue pale jitihada za kizazi hiki zilipotua .Ni lazima tuzitambue ,jitihada za kiakili,jitihada za kielimu -zile jitihada ambazo zitatuelekeza kwao tukiwa tunatambua(juu ya wajibu wao)-kwa maana ya yale mambo ambayo yanawasumbua vijana wa kisasa,ambayo hayajawasumbua vijana wa siku zilizopita.

Hapo zamani za kale ,milango ya kwenye matukio (yanayotokea duniani kote)yalikuwa yamefungwa machoni mwa watu -wakati watu wanapokuwa wamefungiwa milango , na madirisha pia yanakuwa yamefungwa ,basi Maisha yanakuwa si rahisi .Hivyo hakuna mtu aliyejua ni nini kilichokuwa kinatokea baadhi ya sehemu za ndani hata huko nje ya nchi.Leo hii milango hii na madirisha (ya kwenye miji nan chi nyingine)iko wazi kabisa.

Leo hii ,watu wanaweza kuiona dunia yote nah atua ya maendeleo ambayo dunia imefikia.Wanaiona elimu ya dunia ;wanauona uwezo wa kiuchumi duniani kote ;wanaziona nguvu za kisiasa na kijeshi za ulimwengu ;wanaweza kuziona demokrasiaa za dunia ;wanauona usawa unaochukua sura duniani kote ;wanayaona mavuguvugu na machafuko yote yanayotokea katika dunia .Vijana wanayaona mambo haya ,hivyo hisia zao zinapanda juu,na wanayo haki ya kuyaona mambo hay ana kujifikiria wenyewe na halafu waseme :kwanini tumeachwa nyuma (licha ya maendeleo yote haya )?

Mshairi mmoja alisema
“Ni lazima niseme kweli kwamba siwezi kuvumilia kuona ,wapinzani wangu wakiishi vizuri wakati mimi nikiangalia tu.”

Kwa namna hii dunia inasonga mbele kuelekea kwenye uhuru wa kisiasa ,kiuchumi na kijamii,na inaelekea kwenye umaarufu ,ubora ,heshima na uhuru hata hivyo sisi bado tumelala au tunashuhudia haya mabadiliko ya mbali tunapiga miayo.

Vizazi vilivyotangulia havikuelewa mambo yote hay ana havikuweza kuyatambua ,hata hivyo hiki kizazi kipya kinayo haki ya kusema kwamba .Kwanini Japan wameendelea kiviwanda kuliko sisi ndani ya mwaka huohuo na zama hizo hizo

HIVI HIKI KIZAZI KIPYA HAKINA HAKI YA KUULIZA MASWALI KAMA HAYA?

VIZAZI VILIVYOPITA HAVIKUWA NA UZITO MKUBWA WA UTANDAWAZI UKIWAELEMEA MABEGANI ,KAMA AMBAMO HIKI KIZAZI CHA SASA KINAPITIA
 
Back
Top Bottom