Ni kiwango gani cha kilevi mwilini unachoruhusiwa kuendesha gari?

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
16,378
18,307
Hapa karibuni kumekuwa na ukamatwaji wa madereva ambao wanatumia kilevi na kuendesha magari ya abiria na hata binafsi.

Natumaini katika taratibu/ sheria zetu zinaeleza kuwa usipovuka kiwango fulani haitakuwa na athari na hata kama ukikamatwa unaweza kuruhusiwa.

Ningependa kufahamu kiwango hicho.
 
"Don't drink and drive" afu wewe unauliza kiwango!!! hairuhusiwi hata pafu moja.
 
bia moja tu ukizidisha nyingine kile kipimo chao kinakukamata!
Kuna hata vinywaji laini zaidi ya beer, nadhani tukipata kiwango kitasaidia wakati ukibanwa maana nasikia wengine wanadiriki hata kukaa karibu na mabaa wakisubiri utoke uingie barabarani
 
Hapa karibuni kumekuwa na ukamatwaji wa madereva ambao wanatumia kilevi na kuendesha magari ya abiria na hata binafsi.

Natumaini katika taratibu/ sheria zetu zinaeleza kuwa usipovuka kiwango fulani haitakuwa na athari na hata kama ukikamatwa unaweza kuruhusiwa.

Ningependa kufahamu kiwango hicho.
stock-photo-drunk-man-fallen-asleep-on-the-ground-leaning-his-head-on-a-bench-holding-a-bottle-of-white-wine-153849668.jpg
 
Nikiwa kitwanga kwa kweli kwenye dashboard huwa naona mshale kama hausomi unajikuta mpaka unagusa 170 ila sheria hairuhusu kuendesha ukiwa lusekelo
 
Kulaa apple au ndizi afu ukutane nae wakupatie ukipulizee utajutaa kuzaliwaa wakat hujalewaa
 
Hapa karibuni kumekuwa na ukamatwaji wa madereva ambao wanatumia kilevi na kuendesha magari ya abiria na hata binafsi.

Natumaini katika taratibu/ sheria zetu zinaeleza kuwa usipovuka kiwango fulani haitakuwa na athari na hata kama ukikamatwa unaweza kuruhusiwa.

Ningependa kufahamu kiwango hicho.
Ni 0.00%
 
Back
Top Bottom