Ni kitu gani ulijifunza nje ya Shule /Chuo kimekusaidia wewe au Jamii yetu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Blogging...
Kilimo...
Kuchora

Kuna mamillioni ya maarifa nje ya darasa....
Karibu kushiriki na wanaJF wenzako ujuzi au chochote ulichojifunza nje ya mfumo wa kawaida wa shule...
 
Kujua kwamba Mungu anayehubiriwa na dini hayupo kumenifanya niishi bila hofu ya Mungu huyo na kuniweka huru.
Du!!! Tofauti kabla ya elimu mpya na hii ni nini. Maana Nahisi maisha Bila Imani ya Uwepo wa Mungu ni balaa
 
Swali lako la awali linaweza kuwa na majibu mengi sana. Lakini mimi napenda kuangalia jibu la epistemology. Kwa sababu, huo ni mziziwa mengine yote.

Ninaweza kuyaangalia maisha kwa kutumia mantiki zaidi.

Kwakweli,kutoamini kuwepoMungu kumenifanya niwe na huruma na upendo zaidi. Nafikiri hii wanaita "Secular Humanism".

Nimesoma sehemu kuna mchungaji anawaombea watu kwa kulipwa shilingi laki moja, yaani ukitaka akuombee kwa Mungu unamlipa shilingi laki moja.

Sasa mtu kama mimi nimesoma historia najua Kanisa Katoliki lilifanya habari hizi miaka mingi sana,sasa limeacha.Ni kuwaibia wajinga waliwao tu.

Ukisema maisha bila ya imani ya uwepo wa Mungu ni balaa unakuwa unaonyesha kwamba hujapanua mawazo vizuri na kujua mambo mengi.

Kwa mfano, nchi za Asia kuna mamilioni ya watu wa dini ya wa Buddha, hawaaminikuwapo kwa Mungu, halafu imani zao zakidini haziwaruhusu kuua hata nzi, wanajitahidi katikamaisha yao wasiue hata sisimizi. Sasa hapo hapo kuna watu wa ISIS wanaamini Mungu kweli na kila siku wanachinja watu wenzao, sasa hapo utaona kwamba kusema kutoamini Mungu ni balaa ni kufupisha mambo kunakoweza kukupa majibu tofauti na ukweli.

Ukweli ni kwamba, ukifikiria kirahisi unaweza kuona kutoamini Mungu kutamfanya mtu akose muongozo na kutenda mabaya yote bilahofu ya Mungu. Kwangumimi ni tofauti.

Kwa mfano, naona kama binadamu anayemuamini Mungu anaweza kufanya mabaya mengi akijua kwamba Mungu atarekebisha. Anaweza kuchafua mazingira huku akiamini kwamba anachotakiwa kufanya ni kuomba Mungu tu mambo yatabadilika. Atakata miti bila mpango akisema Mungu kasema zaeni mkaijaze dunia mkaitawale.

Mimi nisiyeamini Mungu nitaona kwa sababu Mungu hayupo, dhamana ya kutunza mazingira naichukua mwenyewe. Nikikata miti najua nitakosa mvua, kwa hiyo nakuwa muangalifu. Kwa sababu najua Mungu hayupo nikiomba Mungu hakuna kitakachobadilika.

Pia, kukosa imani ya Mungu kunanifanya nitoe sadaka zaidi kwa watu wanaohitaji msaada na kumuomba Mungu. Kwa sababu najua Mungu hayupo kuwasaidia, nachukua jukumu la kuwawezesha kwa sababu najua Mungu hayupo. Ningeamini Mungu yupo ningewapotezea kwa kusema Mungu atawasaidia.

Kwa hivyo kuna watu wamesoma vyuo mpaka kumaliza kwa sababu nimewasaidia kuwalipia full gharama za vyuo, kwa sababu nimewaona wanaomba Mungu ambaye hayupo. Nikasema ngoja tu nichukue hili jukumu, kwa sababu Mungu hayupo na hawa wakimtegemea Mungu watakosa kwenda shule.

Cha ajabu, baada ya kufanikisha walimshukuru sana Mungu kwa kunitumia mimi kama chombo cha kufanikisha maombi yao.

Mimi sikuwapinga.

Nimekuwa nikimsoma muandishimmoja myahudi anaitwa Yval Noah Harari, ametoa vitabu vyake viwili vizuri kweli "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History of Tomorrow"

Yuval Noah Harari - Wikipedia

Katika vitabu hivi, ameongelea uwezo wa watu kutengeneza kitu kinaitwa "imagined reality" (yaani,ukweli wa kufikirika tu") kama kitu kimojakikubwa sana kilichomfanya mtu awe tofauti na mnyama.

Ametaja namna fulani za huu "ukweli wa kufikirika tu" kamaideas za thamani ya hela, uwepo wa taifa na uwepo wa Mungu.

Amesema kwamba vyote vitatu hivi si vitu vilivyopo kweli .Noti ya sh 10,000 haina thamani ya vitu inavyoweza kununua, lakini tumekubaliana iwe na hiyo thamani, taifa la Tanzania halipokiuhalisi,l imetungwa tu na kukubalikakisheria, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo - kwa sababu ana a logical contradiction- lakini watu wamekubaliana awepo tu ilikurahisisha kanuni za morality na Mungu awe source of order and morality.

Ni vitabu vizuri sana kujielimisha mambomengi sana. Kama una muda vitafute.
 
Ni kitu gani ulijifunza nje ya Shule /Chuo kimekusaidia wewe au Jamii yetu ...
Aise nje ya darasa mkuu hapo umetukamata, labda jinsi ya kuishi na watu, kujuwa mila na utamaduni wa waTZ, wazungu na wahindi, mapishi tofauti, kilimo kidogo sana nyumbani, bustani za mboga mboga, mipapai, miembe, miwa, mifenesi, mitiki, nazi, passions, migomba tofauti, mifugo kidogo sana kakuku hapa na pale na mbwa, kwa walioniiga, wawili watatu, nina miti mingi ya kivuli kwangu, wengine walijenga bila kupanda miti wala majani, mazege na blocks tupu...Walinishangaa mwanzoni, ila kwa sasa wamepanda hata majani na hii mimea, hata wengine wametoa viblocks na zege nyumba iwe kijani kidogo..Kwa kweli umenikamata vibaya sana hapo...
 
Swali lako la awali linaweza kuwa na majibu mengi sana. Lakini mimi napenda kuangalia jibu la epistemology. Kwa sababu, huo ni mziziwa mengine yote.

Ninaweza kuyaangalia maisha kwa kutumia mantiki zaidi.

Kwakweli,kutoamini kuwepoMungu kumenifanya niwe na huruma na upendo zaidi. Nafikiri hii wanaita "Secular Humanism".

Nimesoma sehemu kuna mchungaji anawaombea watu kwa kulipwa shilingi laki moja, yaani ukitaka akuombee kwa Mungu unamlipa shilingi laki moja.

Sasa mtu kama mimi nimesoma historia najua Kanisa Katoliki lilifanya habari hizi miaka mingi sana,sasa limeacha.Ni kuwaibia wajinga waliwao tu.

Ukisema maisha bila ya imani ya uwepo wa Mungu ni balaa unakuwa unaonyesha kwamba hujapanua mawazo vizuri na kujua mambo mengi.

Kwa mfano, nchi za Asia kuna mamilioni ya watu wa dini ya wa Buddha, hawaaminikuwapo kwa Mungu, halafu imani zao zakidini haziwaruhusu kuua hata nzi, wanajitahidi katikamaisha yao wasiue hata sisimizi. Sasa hapo hapo kuna watu wa ISIS wanaamini Mungu kweli na kila siku wanachinja watu wenzao, sasa hapo utaona kwamba kusema kutoamini Mungu ni balaa ni kufupisha mambo kunakoweza kukupa majibu tofauti na ukweli.

Ukweli ni kwamba, ukifikiria kirahisi unaweza kuona kutoamini Mungu kutamfanya mtu akose muongozo na kutenda mabaya yote bilahofu ya Mungu. Kwangumimi ni tofauti.

Kwa mfano, naona kama binadamu anayemuamini Mungu anaweza kufanya mabaya mengi akijua kwamba Mungu atarekebisha. Anaweza kuchafua mazingira huku akiamini kwamba anachotakiwa kufanya ni kuomba Mungu tu mambo yatabadilika. Atakata miti bila mpango akisema Mungu kasema zaeni mkaijaze dunia mkaitawale.

Mimi nisiyeamini Mungu nitaona kwa sababu Mungu hayupo, dhamana ya kutunza mazingira naichukua mwenyewe. Nikikata miti najua nitakosa mvua, kwa hiyo nakuwa muangalifu. Kwa sababu najua Mungu hayupo nikiomba Mungu hakuna kitakachobadilika.

Pia, kukosa imani ya Mungu kunanifanya nitoe sadaka zaidi kwa watu wanaohitaji msaada na kumuomba Mungu. Kwa sababu najua Mungu hayupo kuwasaidia, nachukua jukumu la kuwawezesha kwa sababu najua Mungu hayupo. Ningeamini Mungu yupo ningewapotezea kwa kusema Mungu atawasaidia.

Kwa hivyo kuna watu wamesoma vyuo mpaka kumaliza kwa sababu nimewasaidia kuwalipia full gharama za vyuo, kwa sababu nimewaona wanaomba Mungu ambaye hayupo. Nikasema ngoja tu nichukue hili jukumu, kwa sababu Mungu hayupo na hawa wakimtegemea Mungu watakosa kwenda shule.

Cha ajabu, baada ya kufanikisha walimshukuru sana Mungu kwa kunitumia mimi kama chombo cha kufanikisha maombi yao.

Mimi sikuwapinga.

Nimekuwa nikimsoma muandishimmoja myahudi anaitwa Yval Noah Harari, ametoa vitabu vyake viwili vizuri kweli "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History of Tomorrow"

Yuval Noah Harari - Wikipedia

Katika vitabu hivi, ameongelea uwezo wa watu kutengeneza kitu kinaitwa "imagined reality" (yaani,ukweli wa kufikirika tu") kama kitu kimojakikubwa sana kilichomfanya mtu awe tofauti na mnyama.

Ametaja namna fulani za huu "ukweli wa kufikirika tu" kamaideas za thamani ya hela, uwepo wa taifa na uwepo wa Mungu.

Amesema kwamba vyote vitatu hivi si vitu vilivyopo kweli .Noti ya sh 10,000 haina thamani ya vitu inavyoweza kununua, lakini tumekubaliana iwe na hiyo thamani, taifa la Tanzania halipokiuhalisi,l imetungwa tu na kukubalikakisheria, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo - kwa sababu ana a logical contradiction- lakini watu wamekubaliana awepo tu ilikurahisisha kanuni za morality na Mungu awe source of order and morality.

Ni vitabu vizuri sana kujielimisha mambomengi sana. Kama una muda vitafute.
Nimemuangalia Huyo jamaa mwenye mvuto wa malaki ya watu waliochagua kutokumuamini Mungu.

1:Kwanza Huyu jamaa NI SHOGA, Ameolewa na Mwanaume anaitwa Itzik Yahav. Point yangu ni kwamba Mtu ambae anachukua maamuzi ambayo hata Mbwa,paka,ngombe asiyejitambua hawezi kuchukua inakubidi umsikilize kwa makini usijekuwa contaminated.
2:NI mtu aliyefanya tafiti kwenye Platform ya Evolution kitu ambacho kikobiased kwenye kumpinga Mungu hivyo matokeo lazima yaheshimu jukwaa alilosimamia.
3:pamoja na yote ni Msomi mwenye mazuri yake
Hapo juu, tu inaonyesha msomi huyu maisha yake tu, na majukwaa aliyopitia Hawezi Kumwamini Mungu.

Mfano wa mchungaji Anaeomba watu PESA sioni kama ni mfano sahihi, Maana Anachokifanya ni kinyume cha neno analoamini. Pili kanisa, au mchungaji sio Mfano sahihi wa Mungu, Kunauwezekano wakasambaza picha hasi juu ya Mungu kwa manufaa,Sababu na malengo yao ambayo sio lazima yaendane na Mungu,

Kuhusu mtu kufanya Mungu atarekebisha, Mfano Kuchafua Mzaingira sio sawa pia. Yesu alipofanya Muujiza wa kubadili Mikate michache kuwa mingi aliwaambia Waokote mabaki yote maana yake alijali mazingira. Unachokifanya unatumia mifano ya watu wasiofuata Mambo ya Mungu wakijificha chini ya mwamvuli wa Mungu ili Kuhalalisha maamuzi uliyochukua.

Kuhus mazingira Pia, Kazi ya Kwanza kupewa MWANADAMU ni kuijali na kuitunza dunia Wakipewa Modal ya Bustani ya endeni" And the Lord God took the man, and put him into the garden of Eden to dress it and to keep it."
Kama kuna mtu anaharibu mazingira kwa kigezo cha Mungu huyo aeleze anatoa wapi huo ujasiri.

Nimeandika haya kwa Sababu naamini Mungu, Ila lengo sio Kukufanya Umuamini pia Mungu, Ila uongeze uwezo wa kuhoji hicho unachokiamini na Role Model wa imani hiyo. Maana kutokuamini Mungu nayo ni Imani iliyojificha ndani ya Sayansi and Logical arguments.
 
Nimemuangalia Huyo jamaa mwenye mvuto wa malaki ya watu waliochagua kutokumuamini Mungu.

1:Kwanza Huyu jamaa NI SHOGA, Ameolewa na Mwanaume anaitwa Itzik Yahav. Point yangu ni kwamba Mtu ambae anachukua maamuzi ambayo hata Mbwa,paka,ngombe asiyejitambua hawezi kuchukua inakubidi umsikilize kwa makini usijekuwa contaminated.
2:NI mtu aliyefanya tafiti kwenye Platform ya Evolution kitu ambacho kikobiased kwenye kumpinga Mungu hivyo matokeo lazima yaheshimu jukwaa alilosimamia.
3:pamoja na yote ni Msomi mwenye mazuri yake
Hapo juu, tu inaonyesha msomi huyu maisha yake tu, na majukwaa aliyopitia Hawezi Kumwamini Mungu.

Mfano wa mchungaji Anaeomba watu PESA sioni kama ni mfano sahihi, Maana Anachokifanya ni kinyume cha neno analoamini. Pili kanisa, au mchungaji sio Mfano sahihi wa Mungu, Kunauwezekano wakasambaza picha hasi juu ya Mungu kwa manufaa,Sababu na malengo yao ambayo sio lazima yaendane na Mungu,

Kuhusu mtu kufanya Mungu atarekebisha, Mfano Kuchafua Mzaingira sio sawa pia. Yesu alipofanya Muujiza wa kubadili Mikate michache kuwa mingi aliwaambia Waokote mabaki yote maana yake alijali mazingira. Unachokifanya unatumia mifano ya watu wasiofuata Mambo ya Mungu wakijificha chini ya mwamvuli wa Mungu ili Kuhalalisha maamuzi uliyochukua.

Kuhus mazingira Pia, Kazi ya Kwanza kupewa MWANADAMU ni kuijali na kuitunza dunia Wakipewa Modal ya Bustani ya endeni" And the Lord God took the man, and put him into the garden of Eden to dress it and to keep it."
Kama kuna mtu anaharibu mazingira kwa kigezo cha Mungu huyo aeleze anatoa wapi huo ujasiri.

Nimeandika haya kwa Sababu naamini Mungu, Ila lengo sio Kukufanya Usiamini Mungu, Ila uongeze uwezo wa kuhoji hicho unachokuamini na Role Model wa imani hiyo.
Unafahamu asexual reproduction ni nini?
 
Back
Top Bottom