Ni kitu gani ulifanyiwa na mtu, kikundi cha watu au taasisi mpaka ukajiuliza hawa watu wananichukuliaje?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
569
1,214
Salaam wana JF,

Dunia uwanja wa fujo na kila mtu anafujo zake, lakini kuna baadhi ya watu wanazidisha fujo na kuanza kuona wao ndiyo wanapaswa kuishi peke yao duniani. Hawa huwa wanajiribu kufikiri kuwa binadamu wengine walikuja duniani kwa bahati mbaya.

Mtu au kundi kama hili hudiliki kuwafanyia binadamu wenzao lolote watakaloliona linafaa machoni pao. Sasa je, wewe uliwahi kukumbana mkasa kama huu na ilikuwaje?
 
Kuna nyumba nlikuwa naishi, nliamka nikawa nafagia nje, mtoto wa mwenye nyumba aliye darasa la sita akanifata nje, akaniambia ninataka kuoga, nikamuuliza kwa Nini unaniambia mm kwamba unataka kuoga? Akaniambia "bafu chafu na ninyi ndo huwa mnalisafisha" nikamwambia dogo , Kama unataka kuoga utaenda kuoga , Kama hutaki endelea kukaa hapohapo, dogo akaingia ndani nikamsikia anasafisha bafu, akamaliza akaoga, nakuja kurudi ndani nakuta dogo kachafua bafu kachanachana toilet paper katupatupa chooni, kaweka na matakataka bafuni, nikamuuliza mbona umechafua choo akasema mm siwezi waoshea ninyi choo , nikasema duh. Jamani tuwalee watoto wetu vizuri , wasiwe wanadharau watu. Wapendwa I was wondering huyu dogo ananichukuliaje.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom