Princess Zara
Senior Member
- Dec 17, 2016
- 124
- 314
Kila mtu duniani ana kitu fulani ambacho hakifanyii ubahili pindi anunuapo. Yani haoni shida kutumia pesa nyingi kukinunua kama amekipenda.
Kwangu mimi ni Mashuka na Vyombo vya kulia chakula. Mungu anajua napenda kulala sehemu inayovutia. Yani nikiona shuka hata kama bei yake ni nusu ya mshahara wangu lakini nimelipenda nalinunua hapo hapo. Yani nikichaguaga mashuka unaweza kusema my life depends on it.
Vyombo ndo ugonjwa wangu mwingine. Naweza kukaa masaa matatu mfululizo online naangalia vyombo. Napenda vyombo sana na nishawaza kufanya biashara hiyo(Inshaallah one day). Kuna siku niliona set ya vibakuli na vijiko vyake kwenye duka moja bei noma sana. Nilitoa macho kama mjusi kabanwa na mlango lakini vilikuwa vizuri sana. Nakumbuka kwa miezi 3 nilikuwa sili hata muhindi wa kuchoma njiani kwa kujibana ili nikainunue. Na nilifanikisha.
Je wewe mwenzangu 'uchizi' wa matumizi unakupata kwenye kitu gani?