Ni kitu gani kinasababisha mitungi ya Oksijeni kulipuka?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nimeona Irag limetokea tukio la kutisha.

Hata hivyo sio mara ya kwanza kusikia mitungi ya gesi ikilipuka.Hasa mitungi ya gesi ya kupikia majumbani.

Swali langu ni hili,je sababu ya kulipuka huwa ni nini?

Je, upo uwezekano wa kuchukua tahadhari au ndio hivyo ni kudra za mwenyezi Mungu tu?

Mbona sijawahi kuona elimu ya kuchukua tahadhari ikitolewa?
===
Watu 64 wamefariki Dunia na wengine 50 wamejeruhiwa baada moto Mtungi wa Oksijeni kulipuka katika wodi inayotibu wagonjwa wa Corona katika Hospitali ya Al-Hussein katika mji wa Nasiriya, kusini mwa Iraq.

Waziri Mkuu Mustafa Al-Kadhimi ameagiza kusimamishwa kazi kwa Meneja wa Hospitali hiyo na Viongozi wengine wa Hospitali na kuagiza wakamatwe kwa mahojiano zaidi.

Aidha Spika wa Bunge la Iraq Mohamed al-Halbousi ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa tukio hilo la moto katika hospitali hiyo ni uthibitisho tosha wa kushindwa kuwajibika katika majukumu ya kulinda maisha ya waIraqi, na ni wakati wa kukomesha janga hili".
 
Sio mjuzi sana ila kuna siku nilisikia wakitoa mafunzo kidogo kuhusu mitungi ya gesi za kupikia majumbani..

Kua kamwe usipime mtungi kwa kuutikisa, kuna namna ya kupima kiasi cha gesi uliyobaki kwa kutumia maji( wajuzi watasaidia hapa nimesahau ila nakumbuka ni kua unamwagia maji upande wa mtungi wako kuna mahali patakauka na pengine hapatakauka kwa haraka)

Hakikisha ukimaliza kupika unazima gesi yako, hata kama sio wewe ulietumia jiko ni vizuri kuhakikisha mtungi umefungwa na gesi haitoki.
 
Back
Top Bottom