Ni Kitu gani kimeufunika ghafla ule 'Mvumo' wa Hasira za Watanzania wa Mitandaoni kwa Ole Sabaya na Paul Makonda?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,795
Nimeshtuka kuona sasa ni Wiki ya Tatu hii Watanzania wengi wa Mitandaoni ni kama vile tumezimwa ghafla na ule 'Mvumo' wetu wa Kumsagia Kunguni Ole Sabaya na Pacha wake wa Matukio ya 'hovyo hovyo' nchini Paul Makonda.

Ni kwanini Watanzania wa Mitandaoni humu na hata wale wa nje ( katika Jamii ) tukiwa tuna Jambo letu huwa hatuendi nalo hadi likamilike na badala yake huwa 'tunachepushwa' Kiaina kisha tunalisahau na kuachana nalo na kuwapa Ushindi wale tuliokuwa tukiwasagia Kunguni?
 
Nimeshtuka kuona sasa ni Wiki ya Tatu hii Watanzania wengi wa Mitandaoni ni kama vile tumezimwa ghafla na ule 'Mvumo' wetu wa Kumsagia Kunguni Ole Sabaya na Pacha wake wa Matukio ya 'hovyo hovyo' nchini Paul Makonda...
Sabaya si ananyea debe mkuu? Tutadeal nae alimpelekea mahakamani. Bashite hana ishu naamini kunankona watambamba tu maana alifanya mengi machafu. Hayupo salama dawa ni kuacha wanaomfuatilia waendelee na kazi.

Otherwise tulikuwa na upepo wa Chalamila then ukaja upepo wa Madc ambao hadi wasanii na waandishi wamekula mashavu.

Wacha tusubiri DED na DAS then Sabaya atakuwa amerudishwa mahakamani tutaendelea kudemka nae. Uzuri wake ushahidi unazidi kupokelewa kwa TAKUKURU
 
Nchi ya matukio hii sasa hv watu wako na manara na barbra

Nchi haina direction kwa hiyo popote pale tulipo ni kama tumefika kwa sababu hatuwahi popote.

Wananchi wako frustrated wanajiliwaza na instagram na "memes"(wanailazimisha furaha) so ikitokea umepita kwenye anga zao kama sabaya wanakuchamba siku mbili tatu then wanasubiria tukio lingine
 
Nimeshtuka kuona sasa ni Wiki ya Tatu hii Watanzania wengi wa Mitandaoni ni kama vile tumezimwa ghafla na ule 'Mvumo' wetu wa Kumsagia Kunguni Ole Sabaya na Pacha wake wa Matukio ya 'hovyo hovyo' nchini Paul Makonda.

Ni kwanini Watanzania wa Mitandaoni humu na hata wale wa nje ( katika Jamii ) tukiwa tuna Jambo letu huwa hatuendi nalo hadi likamilike na badala yake huwa 'tunachepushwa' Kiaina kisha tunalisahau na kuachana nalo na kuwapa Ushindi wale tuliokuwa tukiwasagia Kunguni?
Kwa sababu kigogo nae amehamia upande wa sabaya.
 
Back
Top Bottom