Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,864
- 155,820
Hapa jamvini kuna wenye magari na wapo ambao wanaendelea kuyatafuta magari na siku hizi gari sio anasa tena ni hitaji la muhimu, hivyo basi ndoto ya wengi ni kuwa na gari.
Ukiwa na gari yako, je vitu gani ungependa kulifanyia gari yako? Na vipi usingependa kulifanyia gari yako?
Mwingine anapenda gari iwe tinted kuanzia kioo cha mbele hadi kwenye taa, mwingine hataki gari iendelee kuwa na muziki uliokuja na gari, hivyo atabadilisha mfumo mzima wa sauti (sound system).
Mwingine hataki tu kuendelea na urembo wa kiwandani wa ndani ya gari, atabadilisha viti, ataipamba dashboard, atabadilisha roof na kadhalika.
Mwingine yeye gari yake ndio kila kitu kwake. Gari ni bar, ina chupa ya Konyagi, k Vant, Bia nk. Gari ina mipira ya kiume, begi la nguo, raba za mazoezi, packet ya sigara na viporo vya chips.
Ili mradi kila mtu na mawazo yake. Je wewe kwako ni kipi halali na kipi ni haramu kwa gari yako?