wa ukae
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 2,649
- 2,008
Hongera sana kwa ufafanuzi mzuri wasioelewa nadhani watakuwa wameelewa sasaKama ulianza kutumia intaneti kabla ya mwaka 2009 utagundua kuwa gharama za intaneti sio Sawa na za sasa hasa kuanzia mwaka 2013 mpaka 2017.
Mwaka 2007 mtandao WA Zantel ulikuwa unauza MB 500 Kwa shilingi 6000.
Mwaka 2010, mtandao ulikuwa na bando za bei za mtandao WA Zain(Airtel) ziliuzwa Kwa sh 2000/MB 400, huu ndio ulikuwa mtandao nafuu.
Mwaka 2009 Vodacom walianzisha kifurushi cha 500 ambacho ulikuwa unapata MB 21 kutoka MB 15 Tu.
Kabla ya hapo mitandao haikuwa na vifurushi salio la kawaida kilikuwa linatumika kudownload.
Baada ya awamu ya pili ya mkongo wa Taifa pili ya mkongo wa Taifa kukamilika 2012, bei za data zilishuka.
Vodacom ilikuwa ni nafuu, night bundle iliuzwa Kwa sh 200 na ilikuwa ni unlimited.
Tigo walikuwa na bando la 500 ambapo unasurf internet bila ukomo na wa data mwaka 2014 kama sikosei. Mtandao WA smart uliuza data bila ukomo Kwa 1000.
Pia mkongo wa Taifa ukaleta 3g na 4g hapo kabla tulikuwa na edge.
Changamoto serikali haiboreshi miundombinu na inaongeza Kodi(tozo) Kwa kampuni za simu halafu tunaamishiwa Sisi.
.
Kwa sababu mkongo ulitakiwa utandazwe Kwa awamu tano, awamu ya mwisho ililengwa kutandaza Kwa taasisi kama shule na Pia home intaneti.
Mpaka sasa umeishiwa kwenye awamu mbili Tu.
Na matumizi ya data yanaongezeka hivyo wanatumia njia hiyo kutoza zaidi.
Kitu kinachosababisha data kupanda bei lakini licha ya hivyo huwezi linganisha be ya intaneti kabla ya mkongo kutandazwa na baada ya kutandazwa.