Ni kitu gani alifanya JK na kikabaki kuwa cha Watanzania?, Je ile Gesi ni yetu?

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari Wana JF,

Kuna hoja nyingi sana zinasukuma kujengwa bandari kubwa ya Bagamoyo.

Mradi huu ukipata nguvu sana wkt wa JK. Haukukamilika wkt wake.

Sasa umerejea kwa kasi kiasi cha kudhorotesha hata miradi mingine.

Binafsi ukiniuliza, nitakwambia JK ndio kila kitu kwenye huu Mradi. Hadi muda huu.

SWALI: JK alishafanya mradi gani mkubwa, ukabaki kuwa ni Mali ya Watanzania.?

Hivi Wana JF wote mlikuwa "watoto wachanga" wkt anasema gesi mtwara lazima itoke. Na hadi watu wakachapwa, huko Mtwara kwamba itatoka tu kwa manufaa ya nchi yote!
Hamkumbuki hotuba ya JK akijenga hoja hilo jambo la gesi.?!

Au wote humu mlikuwa watoto?!

SASA UKWELI: Je, leo ile gesi ni kwetu Watanzania?!.

(Nyerere hakuwa mjinga kuepuka dhambi ya kuuza migodi yetu)

Je, leo JK ndio aaminike kwenye ishu ya bandari ya Bagamoyo?!

JK huyu huyu ambae wkt wa Mwinyi aliwahi kuwa Waziri wa Nishati, Madini na Maji.....hadi Leo maji ni mgao Dsm.

Ni kheri nimsikilize Mzee Mangula kuliko JK mara mia.

JK & Co tuachie Bagamoyo yetu.

Mama Samia, watch out! Hii ndio hesabu ya mwisho ya Wachina.

(Tz ndio yenye ARDHI zaidi kusini mwa jangwa la Sahara).

TUMEKWISHA...!!
 
Huyu mkwere wa Msoga ndio adui nambari moja kwa maendeleo ya nchini yetu!!! Bila yeye kufanya uharamia wake na rasimu ya katiba haya malumbano yote ya kujenga Bandari ya Bagamoyo yasingekuwepo kwani yangekuwa yameishashuhurikiwa vilivyo na taasisi husika!! Ujanjaujanja huu wa hawa mafisadi wa kuwania 10% usingepewa nafasi. Kuwa karibu kwake na huyu mama kutaipeleka nchi sehemu mbaya sana.
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Kuna mambo kadha wa kadha hayakuwa sawa wakati wa JK ila haimaanishi hakuna landmark yoyote ambayo imeachwa.
Kwa uchache, JK kafanya yafuatayo makubwa na yenye hadhi/kumbukumbu njema
Kajenga daraja la Kigamboni (daraja la Nyerere)
1638410257151.jpeg
President%20Jakaya%20Mrisho%20Kikwete%20inauguration%20Kigamboni%20Bridge%20construction%20in%20Dar%20Es%20Salaam.jpg

Kaanzisha ujenzi wa flyover ya TAZARA
Kajenda UDOM
Kajenga Muhimbili Mlonganzila Hospital
1638410338150.jpeg

Ameaisisi JK Cardiac Institute
Kejenga barabara za lami kuunganisha na Tabora-Kigoma (japo kuna sehemu wata-share sifa na JPM kwani kwa miaka 5 ya kwanza ya JK kasi ilikuwa ndogo sana chini ya Mramba, Chenge na Kawambwa. Kasi imeonokena term ya pili JPM aliporudishwa ujenzi)
Kajenga Dar Airport Terminal 3
Kajenga daraja la Kikwete
1638409928543.jpeg

JK ni mtani wangu, kuna ambayo wengi watamlaumu naomba nisiweke hapa, ila kwa uchache yako ambayo alifanya na tunaweza ku-bank kwa hayo.
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Kuna mambo kadha wa kadha hayakuwa sawa wakati wa JK ila haimaanishi hakuna landmark yoyote ambayo imeachwa.
Kwa uchache, JK kafanya yafuatayo makubwa na yenye hadhi/kumbukumbu njema
Kajenga daraja la Kigamboni (daraja la Nyerere)
View attachment 2029924
President%20Jakaya%20Mrisho%20Kikwete%20inauguration%20Kigamboni%20Bridge%20construction%20in%20Dar%20Es%20Salaam.jpg

Kaanzisha ujenzi wa flyover ya TAZARA
Kajenda UDOM
Kajenga Muhimbili Mlonganzila Hospital
View attachment 2029925

Ameaisisi JK Cardiac Institute
Kejenga barabara za lami kuunganisha na Tabora-Kigoma (japo kuna sehemu wata-share sifa na JPM kwani kwa miaka 5 ya kwanza ya JK kasi ilikuwa ndogo sana chini ya Mramba, Chenge na Kawambwa. Kasi imeonokena term ya pili JPM aliporudishwa ujenzi)
Kajenga Dar Airport Terminal 3
Kajenga daraja la Kikwete
View attachment 2029923

JK ni mtani wangu, kuna ambayo wengi watamlaumu naomba nisiweke hapa, ila kwa uchache yako ambayo alifanya na tunaweza ku-bank kwa hayo.
Kwao bagamoyo kajenga nini?
 
Kwao bagamoyo kajenga nini?
JK alikuwa Rais wa Tanzania. Kuna barabara ya lami kutoka mwenge ilipanunuliwa mpaka Tegeta na kupigwa mkeka mpaka Bagamoyo ili mzee awe anawahi kijini Msoga.
Tushamlaumu kwa mengi sana ambayo tulipigwa changa la macho ikiwemo mmoja wa waziri wake kwenda UK kusaini mkataba hotelini;
Ila watu wa njia ya Bagamoyo watamshukuru kwa huo mkeka wa Mwenge-Bagamoyo ambayo leo gari nyingi za Tanga, Moshi na Arusha zinapita

JK%2Bakikata%2Butepe%2Bwakati%2Bwa%2Buzinduzi%2Bwa%2Bbarabara%2Bya%2BNew%2BBagamoyo%2Bkuanzia%2BMwenge%2Bhadi%2BTegeta.JPG

Mambo mengi ya uhakika kwenye ujenzi aliyafanya kwa kumpa JPM rungu ili yakamilike kwa wakati.
Ndio maana kwenye kumbukumbu nyingi za ufunguzi JPM anatokea kama waziri wa kisekta.
 
Sawa nimekuelewa.kwao alijenga Barabara tu MOJA.
Hata Barabara ya bagamoyo-chalinze kashindwa kujenga
Barabara ya bagamoyo-kibaha kashindwa kujenga.
 
Habari Wana JF,

Kuna hoja nyingi sana zinasukuma kujengwa bandari kubwa ya Bagamoyo.

Mradi huu ukipata nguvu sana wkt wa JK. Haukukamilika wkt wake.

Sasa umerejea kwa kasi kiasi cha kudhorotesha hata miradi mingine.

Binafsi ukiniuliza, nitakwambia JK ndio kila kitu kwenye huu Mradi. Hadi muda huu.

SWALI: JK alishafanya mradi gani mkubwa, ukabaki kuwa ni Mali ya Watanzania.?

Hivi Wana JF wote mlikuwa "watoto wachanga" wkt anasema gesi mtwara lazima itoke. Na hadi watu wakachapwa, huko Mtwara kwamba itatoka tu kwa manufaa ya nchi yote!
Hamkumbuki hotuba ya JK akijenga hoja hilo jambo la gesi.?!

Au wote humu mlikuwa watoto?!

SASA UKWELI: Je, leo ile gesi ni kwetu Watanzania?!.

(Nyerere hakuwa mjinga kuepuka dhambi ya kuuza migodi yetu)

Je, leo JK ndio aaminike kwenye ishu ya bandari ya Bagamoyo?!

JK huyu huyu ambae wkt wa Mwinyi aliwahi kuwa Waziri wa Nishati, Madini na Maji.....hadi Leo maji ni mgao Dsm.

Ni kheri nimsikilize Mzee Mangula kuliko JK mara mia.

JK & Co tuachie Bagamoyo yetu.

Mama Samia, watch out! Hii ndio hesabu ya mwisho ya Wachina.

(Tz ndio yenye ARDHI zaidi kusini mwa jangwa la Sahara).

TUMEKWISHA...!!
Tungekuwa na katiba kama ya South Africa JK ilibidi muda huu awe Jela..
 
Malaika wa Chato hakufaa kuwa Rais wa nchi yenye upendo kama Tanzania. Amezalisha sumu ambayo kama juhudi kubwa isipofanyika, Tanzania itaingia kwenye rekodi sawa na Burundi na Rwanda. Ndio maana Mungu akaona amalizane naye mapema. Yaani mtu anauwezo wa kuandika yote haya lakini hajui kama ni huyo Kikwete ndiye bomba alilojenga la Gesi kutoka Mtwara ndilo linaloleta ahueni ya umeme kwa sasa. Mtu hajui kwamba kama si usambazaji wa mkongo uliofanywa na Kikwete, asingejidai na internet hii aliyonayo sasa. Na huenda mtoa mada alisoma shule ya kata au alisoma UDOM au anaandika utumbo wake akiwa ndani ya mwendokasi au mjombaake yuko Mloganzila au yuko Moi aionayo sasa, yet hajui kama yote hayo ni matunda ya Kikwete.

Kuna watu mlihadithiwa historia ya nchi hii ila rudini kwa waliowahadithia wawamalizie stori. Kwa mnaotoka mikoa ya pembezoni, Kikwete ndiye aliyejenga hizo barabara zote kuanzia kuanzia Masasi hadi Sumbawanga hadi huko Chato kwa Malaika wenu.

Mpeni heshima yake Kikwete, wengine kwa akili zenu msingeweza kupata alama za kuendelea na masomo kama si shule za Kata za Kikwete.
 
Back
Top Bottom